Je ratiba kama hii ina afya kwa timu husika ?

Je ratiba kama hii ina afya kwa timu husika ?

Nehemia Kilave

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2022
Posts
1,414
Reaction score
3,118
Habari jf ,mfano hii ni Ratiba ya viporo ya Simba Sc ,Yanga nao ratiba tight .Kuna haja TFF ratiba zao kuzi review vizuri .
IMG-20240129-WA0015.jpg

Na hii hapa ni fixture ya Yanga.

Tarehe 2/2
Kagera vs Yanga

Tarehe 5/2
Yanga vs Dodoma

Tarehe 8/2
Yanga vs Mashujaa

Tarehe 11/2
Prisons vs Yanga
 
Habari jf ,hii ni Ratiba ya viporo ya Simba ScView attachment 2886973
Hiyo sio ratiba ya viporo vya Simba pekee bali ndio ratiba ya ligi kuu na imepangwa kwa timu zote.

Hii hapa ni fixture ya Yanga.

Tarehe 2/2
Kagera vs Yanga

Tarehe 5/2
Yanga vs Dodoma

Tarehe 8/2
Yanga vs Mashujaa

Tarehe 11/2
Prisons vs Yanga
20240129_141210.jpg
 
Tuliposema TFF ni Wahuni mkawatetea, Mechi ya Tanzania na Tanzania B ilikuwa na faida gani kama si kuumiza timu? Simba ina Mechi 5 ndani ya siku 13.
Mechi 5 siku 13 umepataje? Simba na Yanga wote watacheza kila baada ya siku tatu. Hivyo katika siku 10(February 3-12) simba itacheza michezo minne. Hivyo hivyo kwa Yanga nao katika siku 10( February 2-11) watacheza michezo minne. Sasa mnalalamika kipi hapo?
 
Tuliposema TFF ni Wahuni mkawatetea, Mechi ya Tanzania na Tanzania B ilikuwa na faida gani kama si kuumiza timu? Simba ina Mechi 5 ndani ya siku 13.
Pitia fixture vizuri mkuu, hii ratiba haijaikandamiza Simba. Tatizo mleta uzi kaandika uzi akijua ratiba ipo hivyo kwa Simba pekee. Ila ratiba ipo hivyo hivyo hata kwa Yanga wote wanacheza idadi sawa ya mechi na pia watacheza kwa gap la siku sawasawa.
 
Kuna mda mwingi ulitumika vibaya madhara yake ndio haya
 
Mnaosubiria Simba kufungwa...endeleeni kuota....
 
Mechi 5 siku 13 umepataje? Simba na Yanga wote watacheza kila baada ya siku tatu. Hivyo katika siku 10(February 3-12) simba itacheza michezo minne. Hivyo hivyo kwa Yanga nao katika siku 10( February 2-11) watacheza michezo minne. Sasa mnalalamika kipi hapo?
Mleta mada kaweka Simba kama reference. Hakuna popote nikipoonyesha nalalamika sababu Simba ana ratiba ngumu peke yake. Unaniuliza nimepataje Mechi 5 ndani ya siku 13? January 31 Simba anaanza FA kabla ya Feb 3 kuendeleza ligi.
 
Kitendo cha kusema Simba ndani siku 13 ana michezo 5 ni wazi ulishangaa ya Simba hukujipa wasaa kuangalia ratiba kwa timu zingine pia wakati kimsingi hakukuwa na tofauti baina yao.
Yanga anacheza tarehe 30 FA Dar kisha tarehe 2 anatakiwa Kaitaba acheze na Kagera. Na anacheza back to back michezo minne ya ligi kila baada ya siku tatu. Kuna tofauti gani na Simba hapo?
 
Back
Top Bottom