Je, rungu la Spika wa Bunge (Mace) lilikuwepo wakati akina Halima Mdee wanaapishwa

Je, rungu la Spika wa Bunge (Mace) lilikuwepo wakati akina Halima Mdee wanaapishwa

MdogoWenu

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2009
Posts
554
Reaction score
916
Ibara ya 68 ya katiba inasema hivi;

Kila Mbunge atatakiwa kuapishwa katika Bunge kiapo cha uaminifu kabla hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge; lakini Mbunge aweza kushiriki katika uchaguzi wa Spika hata kabla hajaapishwa.

Mamlaka ya Spika ni lile rungu. Bila rungu maana yake bunge halipo.

Akina Halima Mdee na wenzake wameapa majuzi.

Je, lile rungu lilikuwepo?
 
Walichanganyikuwa Hadi wakasahau kuweka SIWA,
Kumbuka SIWA ndiyo bunge,Kama hakuna SIWA hakuna bunge,

Leo baada ya kujua walisahau kuweka siwa ,wanajuta.

Kwani siwa huwa linatumika popote?
 
Siwa liko pale kwa mujibu wa sheria na kanuni; no one is supposed to be above the law. Mamlaka ya Spika yanakamilika in the presence of Siwa.

In the absence of Siwa tunamwona Ndugai hatumwoni Spika na kinyume chake.
Mbona akiwa anapita mitaani anatambulika ni Spika mkuu? Kwa taarifa yako Spika akishachaguliwa na wabunge anakuwa Spika haijarishi iwepo SIWA ama la. Ila kama ungeniambia Mkutano wa Bunge lazima iwepo hiyo SIWA at least ningekuamini kwa mbaliii nikibukua sheria hapa ili kujua maana ya Bunge kisheria ni nini? Lakini naamini wanasheria walioko Ofisi ya Bunge watakuwa wanajua zaidi yetu ndiyo maana waliamua hivyo.
 
Back
Top Bottom