Je, rungu la Spika wa Bunge (Mace) lilikuwepo wakati akina Halima Mdee wanaapishwa

Je, rungu la Spika wa Bunge (Mace) lilikuwepo wakati akina Halima Mdee wanaapishwa

Spika aliwaapisha vile akiwa anajua kuwa wale sio wabunge kwani hawakufuata njia halali na ilikuwa ni makosa ya kikatiba kuwaapisha ndani ya Bunge kitu ambacho mbele ya safari angeweza kutakiwa kujibu mashtaka ya kuvunja katiba, lakini pia aliangalia uteke teke wa watu kutokufuata sheria kulivyokithiri naye akaamua kupita humo humo kwani leo hapo alipo hakuna wa kumfanya lolote

Kwa ufupi kwa sheria zetu za bunge pamoja na katiba yetu iliyopitwa na wakati wale Covid 19 sio wabunge halali na ndio maana wakatumia gereji kuwaapisha bila wao kuligundua hilo wakiwa na mwanasheria Halima Mdee
 
Ibara ya 68 ya katiba inasema hivi;

Kila Mbunge atatakiwa kuapishwa katika Bunge kiapo cha uaminifu kabla hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge; lakini Mbunge aweza kushiriki katika uchaguzi wa Spika hata kabla hajaapishwa...
Kifungu gani kinasema Mamlaka ya Spika yanategemea uwepo wa Rungu?
 
Kuna tofauti ya Bunge na ukumbi wa Bunge

Mbunge sharti aaapishiwe bungeni sio ukumbi wa Bunge

Hata angeapishwa kwny canteen ile ya Bunge bado 'inaswihi tu'
Inshort pale gereji walipoapishwa hao waasi hapakua na sifa yoyote ya kuitwa bunge.
 
Bila kuwepo SIWA,maana yake bunge halijakamilika,
Kwa hiyo kina Mdee waliapishwa na nwenyekiti wa kamati ya bunge na siyo sipika.

Kwa hiyo kama spika angekumbuka kuleta siwa pale nje ingekuwa halali?
 
Sasa kama hakukuwa na bunge maana yake kiapo chao ni batili, ilikuaje sasa kamati kuu ya Mbowe ikawakuta na hatia ya kuapa kuwa wabunge bila ya ridhaa ya Chama
Wameshakuambia wenzake siwa ndiyo bunge.

Kama haikuwepo hakukuwa na bunge.
 
Mbona akiwa anapita mitaani anatambulika ni Spika mkuu? Kwa taarifa yako Spika akishachaguliwa na wabunge anakuwa Spika haijarishi iwepo SIWA ama la. Ila kama ungeniambia Mkutano wa Bunge lazima iwepo hiyo SIWA at least ningekuamini kwa mbaliii nikibukua sheria hapa ili kujua maana ya Bunge kisheria ni nini? Lakini naamini wanasheria walioko Ofisi ya Bunge watakuwa wanajua zaidi yetu ndiyo maana waliamua hivyo.
Nazungumzia execution of the powers of the Speaker of the National Assembly. Hili hufanyika mahali maalum (Bungeni); mbele ya wajumbe wenye sifa maalum (wabunge); na kwa utaratibu maalum (Siwa, kanuni, etc.).
 
Ibara ya 68 ya katiba inasema hivi;

Kila Mbunge atatakiwa kuapishwa katika Bunge kiapo cha uaminifu kabla hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge; lakini Mbunge aweza kushiriki katika uchaguzi wa Spika hata kabla hajaapishwa...
Boss kanuni ilibadilishwa na bunge la 11 now inasomeka mbunge anatakiwa kuapa mbele ya Spika sio mbele ya bunge mbona ishu ni simple tu?
 
Back
Top Bottom