Je, rungu la Spika wa Bunge (Mace) lilikuwepo wakati akina Halima Mdee wanaapishwa

Je, rungu la Spika wa Bunge (Mace) lilikuwepo wakati akina Halima Mdee wanaapishwa

Inaitwa SIWA, sio rungu! Mnh....mambo mengine kama ushirikina Wallah!!!!
 
Ibara ya 68 ya katiba inasema hivi;

Kila Mbunge atatakiwa kuapishwa katika Bunge kiapo cha uaminifu kabla hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge; lakini Mbunge aweza kushiriki katika uchaguzi wa Spika hata kabla hajaapishwa.

Mamlaka ya Spika ni lile rungu. Bila rungu maana yake bunge halipo.

Akina Halima Mdee na wenzake wameapa majuzi.

Je, lile rungu lilikuwepo?
Ki-ccm ccm watakujibu kwamba waliapishwa ndani ya viunga vya bunge na rungu lilikuwepo ndani hivyo hakuna kosa hapo. Tunawajua vizuri ccm hawakosi hoja bila kujali hoja hiyo ina maana ama haina maana.
 
Hachana na mambo ya Rungu mkuu haya majamaa ni majizi sana yasoheshimu katiba so ivyo ni vitu very negligible to them
 
Mbunge anaapishwa na Spika sio na Bunge.....uwepo Wa Siwa/mace maana yake bunge linaendelea.

Hapakuwa na bunge pale hivyo sio mace haitakiwi kuwepo.

Kanuni ya bunge inasema....sio lazima mbunge aapishiwe bungeni ila ni lazima aapishwe na Spika.
 
Wameshakuambia wenzake siwa ndiyo bunge.

Kama haikuwepo hakukuwa na bunge.
Bunge ni watu hiyo siwa ni sanamu. Kwani ni mthamini sanamu kuliko mtu? Kwahiyo siwa ikiwepo bila watu ndo linakuwepo bunge?
 
Mbunge anaapishwa na Spika sio na Bunge.....uwepo Wa Siwa/mace maana bunge linaendelea.
Hapakuwa na bunge pale.
Kanuni ya bunge inasema....sio lazima mbunge aapishiwe bungeni ila ni lazima aapishwe na Spika.
Soma katiba niliyoi quote.

Katiba ni kubwa kuliko hata sheria, achilia mbali kanuni.

Na upunguze ukilaza
 
Kuna tofauti ya Bunge na ukumbi wa Bunge

Mbunge sharti aaapishiwe bungeni sio ukumbi wa Bunge

Hata angeapishwa kwny canteen ile ya Bunge bado 'inaswihi tu'

Katika sheria Kama tafsiri italeta utata Kati ya laugha ya kiswahili au kiingereza basi ya kiingereza itafuatwa. Unaelewa maana ya National Assembly we mswahili?
 
Sheria huwa inafasiriwa kwa liberal sio literal meaning
Katika sheria Kama tafsiri italeta utata Kati ya laugha ya kiswahili au kiingereza basi ya kiingereza itafuatwa. Unaelewa maana ya National Assembly we mswahili?
 
Hii ngoma ni droo Aliye uza dhahabu feki na kupewa noti bandia

Mdee kapeleka hati feki

Ndugai kaapisha kifeki

Vigezo na masharti vizingatiwe

Dunia ina Wazoom
 
Kumbe Ndugai wakati anawaapisha wale wanawake 19 naye "hakuwa na Rungu"
 
Ibara ya 68 ya katiba inasema hivi;

Kila Mbunge atatakiwa kuapishwa katika Bunge kiapo cha uaminifu kabla hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge; lakini Mbunge aweza kushiriki katika uchaguzi wa Spika hata kabla hajaapishwa.

Mamlaka ya Spika ni lile rungu. Bila rungu maana yake bunge halipo.

Akina Halima Mdee na wenzake wameapa majuzi.

Je, lile rungu lilikuwepo?
Ule ni sawa na ramli kwa waganga wa kienyeji waliapishwa kihuni huni tu kama wabunge mamluki
 
Back
Top Bottom