Je, Salim Kikeke ataendelea kuendesha mijadala ya kisiasa na viongozi wa vyama vya upinzani?

Je, Salim Kikeke ataendelea kuendesha mijadala ya kisiasa na viongozi wa vyama vya upinzani?

Habari ya wote humu ndani kama

kichwa kinavojieleza hapo juu,salim kikeke ni moja ya watangazaji nguli wa mda mrefu wa masuala mbalimbali yanayohusu mambo mbali mbali kuhusu nchi yetu hata alipokuwa BBC.
Baada ya kutoka huko ughaibuni kikeke alikuja na kuendelea kazi yake ya utangazaji na media za hapa kwetu nyumbani Tanzania kwa kipindi chote hicho hajawahi kuonyesha mlengo wowote wa kichama hivyo kumwezesha kukutana na kufanya mijadala kadha wa kadha na viongozi wa vyama mbali mbali.

SIku za hivi karibuni tumeshuudia chama cha mapinduzi kimeanza mchakato wa ndani ya chama wa watia nia ngazi za ubunge na udiwani kuchukua fomu na kurejesha katikati mwa zoezi hilo pia salim kikeke ameonekana akichukua fomu ya kutia nia kugombea nafasi ya ubunge kupitia CCM katika moja ya jimbo la mkoa wa kilimanjaro.

Je salim kikeke ataendelea kuendesha hio mijadala ilhali tayari yeye ameshaonyesha tayari ni mwanachama wa CCM.

karibu tujadili kwa hekima

Natanguliza shukrani.
Ataendelea na biashara nyingine. Halafu tatizo la viongozi wa CCM wakishaona ni mwenzao wanakuwa hawako serious na wewe tena. Hata kuhojiwa na wewe wanaona haina uzito tofauti na mtangazaji ambaye hawajui itikadi yake.
 
Back
Top Bottom