Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
JE SCHOLARSHIP NI MBINU YA KUTENGENEZA VIBARAKA WA KISIASA?
Anaandika Robert Heriel.
Scholarship inaweza kuwa na maana nyingi, mojawapo ni kumsaidia mtu/mwanafunzi kirasilimali aweze kupata elimu Fulani; Rasilimali hiyo inaweza kuwa Fedha, au mahali pa kuishi(makazi), au chakula, au vitendea kazi vya kujifunzia.
Mara nyingi kama zote Scholarship hutolewa Kwa sababu kadhaa, zipo sababu za wazi na zile sababu za siri/nyeti ambazo mtoa scholarship hazitaji Mwanzoni.
Zipo scholarship zinazotolewa na Makundi Yafuatayo;
1. Mtu binafsi
2. Kampuni au shirika
3. SERIKALI
Mtu binafsi Kama Mimi na Wewe tunaweza kutoa scholarship Kwa wanafunzi wengine. Hata hivyo hatuwezi kukataa ukweli kuwa Scholarship haitolewi burebure.
Wapo watu waliopewa Scholarship wakasome ili waje kuoa/kuolewa na mtoto wa mtoa Scholarship. Wengine hutoa scholarship Kwa kusomesha watoto Yatima lakini katika hao Yatima wapo ambao baadaye hupewa majukumu Fulani huko mbeleni wakishafanikiwa kimasomo, huingizwa kwenye aidha mambo ya Siasa, au kuajiriwa katika sekta nyeti ili walinde maslahi ya waliowasomesha. Hata hivyo si lengo langu Kueleza scholarship za watu binfasi.
Pia makampuni, taasisi na mashirika makubwa hutoa scholarship Kwa watu wake Kwa lengo la kuimarisha future ya kundi husika.
Zipo taasisi za Kidini, hutoa scholarship na kuhakikisha zinapenyeza watu wao katika Sekta nyeti ndani ya serikali au katika makampuni na mashirika mengine. Vyama vya Kisiasa navyo hutoa Scholarship Kwa baadhi ya wanachama wake. Hata hivyo ni kawaida Kwa chama kimoja kinaweza kumsomesha mwanachama wa chama kingine pasipo chama husika kujua, kisha baadaye kumtumia mtu huyo katika kuangusha chama hasimu. Mfano, CCM inauwezo wa kumsomesha mwanachama wa CHADEMA bila CHADEMA kujua, mwanachama huyo akaenda mpaka Ulaya huku akiendelea kushiriki Kwa Hali na Mali na shughuli za CHADEMA mpaka kufikia kuaminika, alafu mwisho wa siku akipewa Madaraka makubwa au yanayokaribia ukubwa hukiteteresha Kama sio kukiangusha chama, hiyo ni kawaida kisiasa. Hata hivyo sina lengo pia la Kueleza Jambo hili.
Scholarship zitolewazo na serikali ndio lengo langu kuu katika andiko hili. Kila serikali inanamna yake ya kujiimarisha katika siku za usoni, moja ya mbinu za kufanya hivyo ni Kutoa Scholarship Kama sehemu ya kuwekeza Kwa watu Kwa maslahi ya siku zijazo.
Serikali nyingi za Afrika ikiwemo nch yetu mara nyingi huwapa Scholarship watoto wa viongozi bila kuangali na kufuata vigezo muhimu.
Scholarship Kwa maslahi ya Future ya nchi inapaswa ifuate na kutafuta watu wenye vigezo maalumu. Nitataja Kwa uchache;
1. Wenye Akili na Maarifa ya juu Kabisa
Sio akili za Darasani Bali hata akili za Mtaani, akili za kuongoza watu Kwa kutumia Akili. Zingatia ukiona nguvu kubwa inatumika sehemu ujue akili ndogo imetumika, na ukiona akili nyingi inatumika ujue nguvu ndogo itatumika.
Kiongozi anayetumia nguvu kubwa ujue akili yake huwa kisoda.
2. VIPAJI NA KARAMA ZA JUU
Mtu mwenye kipaji iwe uimbaji, uchoraji, Machale na maono, Hesabu, kipaji cha lugha, kujua lugha ngeni Kwa wepesi, kuchezea computer na masuala yote ya IT, Ubunifu wa Teknolojia mpya au zilizopita kuziboresha, n.k.
Hawa ndio wanapaswa kupewa Scholarship Kwa maslahi ya nchi.
3. UZURI NA MVUTO WA MAUMBILE
Wanawake wazuri kupitiliza, na vijana wenye mvuto ni muhimu Sana kupewa scholarship hasa kwenye ishu za intelejensia ya nchi.
Kwa Wazungu wao Kwa kulijua hili ndio maana wakaanzisha MASHINDANO YA WALIMBWENDE ambayo hujulikana Kama MISS WORLD ambayo Kwa nje yanaonekana ni sehemu ya kukuza vipaji vya fasheni na uanamitindo lakini ajenda za ndani kabisa ni tofauti.
Hawa walimbwende wanaoshinda, wengi wao huzikimbia nchi zao, na kutokomea nchi za baridi huko Ulaya. Husomeshwa na Wale wasio na akili za darasani hupewa majukumu Fulani na kupewa mitaji ya pesa na connection kubwa kubwa.
Warembo hawa baadaye wengi wao hata hapa nchini tunajua wanashobokewa na kuolewa na vigogo Kama sio wafanyabiashara Wakubwa. Bado hujaelewa what next? 😀😀 Wakubwa mmeelewa.
Tusikubali wanawake Wazuri kupitiliza WA nchi hii watumike na watu wa nchi zingine.
Sitaki kuelezea baadhi Yao ambao huweza kuingizwa kwenye biashara hatari na nyeusi ambazo ni jinai kubwa hapa nchini. Biashara za madawa ya kulevya ambazo warembo wetu huweza kutumika Kama Punda kuzitoa upande mmoja wa nchi kwenda nchi zingine.
Hata hivyo ni lazima warembo hawa wajiingize katika mapenzi mazito na vigogo wa nchi husika, utashangaa Mrembo mkali Grade one wa nchi yetu akiingia katika penzi zito na Rais au kigogo wa nchi Fulani, nchi hiyo hata wamkamate huyu mrembo hawawezi kumfanya kitu sababu tayari ana-connection ya moja Kwa moja na vigogo wa nchi hiyo.
Tuachane na haya.
4. WATU WENYE KARAMA ZA UCHUNGAJI NA USHEIKHE NA UGANGA
Kundi hili ni nyeti Kwa sababu ni kimbilio na waovu na Wema.
Scholarship ni muhimu Kwa kundi hili kuliweka mahususi Kwa mipango ya siku zijazo.
Nani asiyejua hata hapa nchini wapo viongozi tena wa ngazi ya Urais kabisa walitoka hapa nchini kwenda mpaka Nigeria Kwa TB Joshua, unafikiri mtu Kama anashida akifika Kwa mganga au mchungaji au Sheikhe hatasema mambo yote kusudi asaidiwe?
Hapa nchini ni nadra Sana Kwa Kiongozi mkubwa wa Kisiasa au wakurugenzi WA makampuni au mashirika makubwa kutojihusisha na Uganga, ama wachungaji wakubwa au masheikhe wakubwa. Wengi WA watu au vigogo wakubwa lazima wawe na mganga wanayemtegemea au mchungaji au Sheikhe. Hilo pia Kwa Majambazi, wezi na wafanya dili HATARI.
Tukiachana na watu wenye sifa hizo.
Mataifa makubwa ya Ulaya, hutumia watu niliowataja hapo juu kuzitawala nchi ZETU.
Vijana wanasomeshwa, wanasoma na kufunzwa hasa namna ya kuwa kibaraka mtiifu. Kisha akihitimu shahada ya kwanza, huja nchini na kuanzisha viprogramu vyake vya hapa na pale.
Kisha huenda tena kusoma na kuchukua degree ya pili mpaka yatatu. Alafu anarudi.
Baadhi Yao hupewa majukumu ya kijamii Kwa kuanzisha vishirika visivyo vya kiserikali Kwa kulenga moja ya mambo Yafuatayo;
1. Kutetea haki za wanawake
2. Kutetea mashoga na wasagaji au mapenzi ya mtu na mnyama
3. Kutetea Demokrasia inayozua ghasia na kuchafua Amani ya nchi.
4. Kutafiti na kuwa consultant wa mambo ya kiuchumi na kupewa nyenzo zote. Hapa utaona vita katika tenda za serikali utashangaa nyingi zinashikiliwa na makampuni ya kigeni ingawaje makampuni mengine huwa na majina ya Watanzania Kama Geresha tuu. Yaani utashangaa Mimi Taikon namiliki Kampuni kubwa lakini kumbe nyuma yangu wapo mabeberu.
5. Kutetea maslahi ya Wazungu hasa kwenye mikataba inayopitishwa bungeni. Miongoni mwa mambo mengine.
Ukiachana na hayo;
Scholarship huweza kuathiri sekta nyeti Kama usalama wa taifa, Bunge na mahakama.
Siku zote hakuna kitu cha Bure.
Ushauri:
Serikali inapaswa iwe Makini Sana katika Jambo hili.
Nipumzike sasa!
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
DAR ES SALAAM