Je, Scholarship ni mbinu ya kutengeneza Vibaraka hasa wa Kisiasa?


Andiko lako zuri na ni fikirishi sana.
Ukisoma kitabu cha John Perkins named The Confession of Economic Hit-man na kama umetizama series named Covert Affairs inayoelezea National Clandestine Services moja ya idara ya kijasusi CIA kuna jambo la kujifunza.

John Perkins alikuwa na interest kufanya kazi na NSA, wao wakaona ana potential kubwa kufanya nae kwenye private interprise kwa maslahi yao makubwa unlike angebaki NSA. Na hata baada ya kusema ukweli wamekanusha kuwa hawamtambui ana anadanganya ila ukisoma between the lines ya nini kaandika vs nini kinatokea kwenye nchi za dunia ya 3, unapata kujua nini Perkins anatuasa.

Covert affairs inaonesha namna CIA imejira operatives na assets. Na kwenye level ya assets ni watu wa kawaida hawana day to-day involvement na majukumu ya CIA, ila unaona namna gani contacts ya operatives na assets inatengenezwa na mambo yaliyokusudiwa yanafanyika kutimiza lengo la idarani.

Nataka kuamini hata sisi hapa wakubwa wanaondesha nchi wako vizuri sana, ila kuna maeneo nadhani hawajafanya vya kutosha ikiwamo economic intelligence and economic security.

Haiwezekani na haingii akilini nchi kama Comoro jirani na Tanzania unakuata basic consumables anatoa India, China na Tanzania iko very close halafu nikinukuu alichowahi kusema mwandazake, tuna PhD 18 BoT achilia mbali walioko hazina, vyuo vikuu na kwingineko.
Kama tungewekeza kwenye economic intelligence, kwa kuzingatia all skills za how it takes tuwe at the cutting age ya basic consumables ili tuifikie hata SADC tu, nchi hii watu wangefurahia kuishi. Ila sasa, kama ulivyotoa maelezo, sijui tunafeli wapi?

Nihitimishe kwa mfano midogo miwili, umesema vema scholarships nyingi wanapewa watoto wa wazeiya. Wakienda wanarejea na vyeti ila kichwani inakuwa kawaida sana. Masihi hakuzaliwa nyumba ya Herode, alitokea kwenye Nazareth ila alifanya maajabu sana na akawa chanzo cha imani ya Ukristo, wenye uelewa watanielewa.

Farao alipopata ndoto ya masuke 7 manono yakimezwa na masuke 7 manyonge, the ng'ombe 7 wenye afya wakemezwa na ng'ombe 7 waliokonda; Farao alihangaika sana kujua nini ni suluhu ya ndoto ile.
Alietoa tafsiri ni Yusuf aliekuwa mfungwa; tukizungumza kwa lugha rahisi Yusuf alikuwa outsider kwenye governance system ya Egypt. Yet ndie alikuja na tafsiri ya how to develop 14 years food reserve and distribution system sio kwa Egyptians pekee, ila hata wageni nje ya Egypt njaa ikitokea. Nakuelewa unaposema akili ya kitaa, sio kila Profesa anayo. Kuna IQ ambayo watu wanayo, wame-develop skills zao outside the governance settings ila kama wakiombwa kuwa sehemu ya kuijenga nchi hii wanaweza kuwa na mchango mkubwa sana bila kuathiri nafasi za waliopo.

Kuna wakati waliopo wanaogopa kuwa out-shined, na hapo ndipo umasikini wa fikra unapoanzia. Wao wana majukumu yao mengi na wakisikia kuna new brain inaleta solution wanataka kudesa ili wafanye wao ili sifa wapate wao, bahati mbaya huwa ukidesa in the absence ya mwenye DNA ya project whicg leads to solution, ukiondoka kama ni Mwanza kwenda Dar, ukifika Ilula mpakani mwa Mwanza na Shinyanga ramanani inapotea au kama waenda Mwanza toka dar, ukifika round about ta Msamvu, unapotea njia. Na kama utafika badala ya safari kuchukua muda mfumpim wazungu wanasema "it will take forever".
7 years za wingi wa chakula ilikuwa muhimu sana kwa Yusuf kujenga food reserve system, kuweka ulizi, kuweka madawa ya kuzuia chakula kisibanguliwe ili miaka 7 sio tu wananchi wasife ila hata wanyama wasife.

Imagine leo msimu mmoja tu mvua zimechelewa, tumeanza kuaswa kutumia vema nafaka, wanyama wanakufa; wakati kuna watu karne nyingi BC, walikuwa na reserve ya 7 years za ukame. Wenye akili na wafahamu.

Jioni njema.

F
 
Nadhani huelewi mleta mada scholarship ni nini?

Mfano Serikali kupitia body ya mikopo hukopesha watu wasome maskini hiyo in scholarship ulichoeleza kwenye hili hata hujagusa

Scholarship namba mbili hulipiwa rare proffession ambazo vyuo vya ndani havitoi na hazipo na nchi inahitaji ya ndani au nje au dunia sababu ya wanafunzi kukwepa kusomea kutokana na ugumu wa hayo masomo wale waliotayari hupewa scholarship

Tatu Scholarship nyingi hutolewa kwa wavumbuzi na wenye outstanding performance iwe masomo nk kuwa in future waweza saidia nchi au dumia


Hizo scholarship zingine ni za vibaka na matapeli ohh tunatoa scholarship za mashoga kufundisha ushoga vyuoni nk wanawapiga pesa wachangiaji na kiduchu ndio wanasomeshea

Iwe dini ,sijui yatima ,mazingira magumu nk mfadhili lazima apige pesa .
 
Hakuna DINI potofu. DINI ni moja tu safi--imani kwa Mungu. Upotofu hauko kwenye DINI, bali uko kwa mwanadamu ambaye ameamua kujichagulia uelekeo wake mwenyewe. Akili ya mwanadamu ndiyo imejaa matongotongo yanayomzuia kumwona Mungu kwa mtazamo halisi.
 
Hakuna DINI potofu. DINI ni moja tu safi--imani kwa Mungu. Upotofu hauko kwenye DINI, bali uko kwa mwanadamu ambaye ameamua kujichagulia uelekeo wake mwenyewe. Akili ya mwanadamu ndiyo imejaa matongotongo yanayomzuia kumwona Mungu kwa mtazamo halisi.
Dini ni njia ya mwanadamu kumtafuta na kumfahamu Mungu wake.
Kama umekili kwamba mwanadamu ana akili yenye matongotongo, basi njia yake (ya kumfahamu Mungu) lazima itakua na makandokando.

Kusema dini iko straight wakati akili ya binadamu haiko straight nadhani sio sahihi sana.

Na ushahidi wa hilo upo. Ushahidi huo ni DINI NYINGI. Na kibaya zaidi aliye kwenye dini A, Anaseme yule aliye kwenye dini B amepotoka. Wa dini C anamshutumu wa dini D. Ni vurugu tupu.

Sioni straightness katika mkanganyiko huu.
 
Ngoja nitafute hivi vitabu niongeze maarifa.
 
Watumishi wa Umma au waTanzania
Inawezekana, binafsi nilichojifunza na ambacho ni kweli kabisa 80% watumishi wa serikali yetu ni vilaza, hivyo hata vision ya nchi huwa ngumu, wengi wa watumishi wetu hawana uwezo wa kuchambua mambo kikawaida tu.
 
Tatizo unang'ang'ana na njia za wanadamu na kuacha DINI ya Mungu. DINI ni safi haina upotofu. Huko ndiko tunapaswa kuifuata njia. Umeelewa?
 
Tatizo unang'ang'ana na njia za wanadamu na kuacha DINI ya Mungu. DINI ni safi haina upotofu. Huko ndiko tunapaswa kuifuata njia. Umeelewa?
"Dini ya Mungu" ni dini ipi ?

Ninavyojua mimi ni kwamba dini ni jambo la kibinadamu kumuelekea Mungu. Sio jambo la kimungu kumuelekea binadamu. Kama ninakosea kwenye uelewa naomba kufahamishwa.

Haya hiyo dini ya Mungu kwa mujibu wako ni ipi ?
Uislam,
Ukristo
Hindu
Budha
Au dini za kiafrika ?

Na hata ukisema moja kati ya hizo hapo juu ndio dini ya Mungu, haifuti ukweli kwamba hizo zinazobakia nazo pia ni "dini".
Vinginevyo uwe mgeni kabisa hapa duniani, yaani ndio unawasili muda huu kwaiyo hujui yanayoendelea kuhusu dini na hata ukasema ipo dini moja tu.

Kumbuka hoja hapa sio "ni ipi dini ya kweli". Hoja ni duniani kuna dini zaidi ya moja ama la, maana mzizi wa mjadala huu ni kwamba sisi waafrika kuna dini fulani na fulani tuliletewa kutoka kwa wenzetu weupe. (Kama umefuatilia mada toka mwanzo).
 

Soma kwa kutafakari nilichoandika. Nimesema, na hapa nakariri tena, kwamba DINI ni moja tu ya Mungu, na ndiyo dini ya kweli, safi. Usiniwekee midomoni mambo ambayo sijayatamka.

Pia, tofautisha kati ya mitazamo na mafundisho na mapokeo ya wanadamu na DINI ya Mungu ya kweli ambayo kimsingi ina-transcend miapaka ya mitazamo na fikra za wanadamu, rangi, hali, hadhi na maeneo ya kijiografia.

Nilisema hapo mwanzo DINI ya Mungu haina mipaka na wala si lazima wakati wote mtu afundishwe na mtu mwingine ili aifahamu.

Please, never call apples mangoes!
 
Uwe na asubuhi njema mkuu.
 
Mkalimani wetu leo anatafasiri lugha ya Kifaransa ndani ya Ikulu tena mbele ya Rais na Mabalozi wa mataifa ya nje. Lakini Kifaransa kinaonekana kumpiga chenga kidogo anakaa kimya na mabalozi wanacheka . Ila yote kwa yote anajitahidi https://t.co/3deNOCrKgt

Jana tulijadili hapa.

Muda sio mrefu, mkalimani akafanya tofauti na matarajio ya wengi.
 


Ngoja tufatilie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…