Je, Serikali ikinyimwa mkopo wa elimu na Benki ya Dunia kutatokea nini?

Halafu naona focus iko ktk kuadhibu watoto wa kike. Kwanini hakuna usawa ktk kutoa adhabu kwa wavulana wanaojaza mimba wanafunzi wenzao?
Mkuu ningependa kukutaarifu wavulana wanao wapa mimba wanafunzi wenzao wanafungwa jela.
Nina ushahidi wa hili jambo, vijana wenzetu wawili walifungwa jela kwa kuwapa mimba wasichana wawili ambao wote walikuwa darasa moja miaka hiyo.
 
JokaKuu siasa chafu ndiyo inaongoza. Kwanini? Kwani tangu zamani wakati wa Nyerere wasichana waliokuwa wanapata mimba walikuwa wanaruhusiwa kuendelea na masoma kama kawaida? Mbona mimi najua wasichana wengi tu waliozaa wakiwa shuleni kipindi cha awamu ya kwanza na walifukuzwa shule na wakatumia njia nyingine kuendelea na masomo baada ya kujifungua? Tena bora siku hizi kuna alternative nyingi lakini kipindi kile kusoma tena wakati umeshfukuzwa shule ilikuwa ngumu. Hata upimaji wa mimba mashuleni ulikuwepo, tena sana tu. Zitto na hawa wanaharakati wengine wote wamesomea kwenye haya mazingara! Kwanini leo waibuke na kusema serikali haiwatendei haki? Hapa wametumia hasira zao kwa awamu ya tano kupinga kitu ambacho siyo kigeni! Kama ulivyosema hata mimi nakubali hili suala linahita utafiti wa kina na wa kulishughulikia ni sisi wenyewe. Hata kama serikali itakubalina na wanachotaka benki ya dunia, bila sisi kama nchi kufanya ulichosema tunaweza kujikuta tumekuza zaidi hili tatizo.

Mkuu nimeheshimu mawazo yako maana kwa sehemu kubwa yana mantiki tena ya wazi. Ila naona hapo ulipochomeka kuhusu Zito kama hujaweka sawa. Ni kweli bank ya dunia imemsikikiza Zito ndio ikaacha kutoa huo mkopo bila kujiridhisha na hali halisi? Kama bank ya dunia inaweza kumsikiliza Zito na kutii, unataka kusema akienda kutaka mkopo kwa ajili ya nchi tutapewa? Kama umeamua kujenga hoja, hebu baki kwenye sababu za msingi, na sio kuokota maoni ya siasa chafu na kuja kuchafua maoni yako mazuri. Huyo Zito ametajwa sana ili kuficha ukweli pindi tukinyimwa huo msaada ionekane ni yeye, lakini ukweli uko wazi hao bank ya dunia hawakutegemea maombi ya Zito kusisitisha huo mkopo.

Ukweli ni lugha za rais kuhusu hao wanafunzi waliopata mimba umepelekea maamuzi ya WB. Kibaya zaidi hata maofisa wa serikali hawakuonyesha kutumia lugha za kurekebisha alichoongea rais wetu. Katika mazingira hayo unategemea hao WB wachukue hatua gani? Alichofanya Zito ni kusoma tu mazingira halisi ya maamuzi ya hicho kikao, na yeye akatupia karata yake humo humo. Kilichotugharimu kwenye huu mkopo ni kiburi cha kijinga, na kiburi hiki kinalazimishwa kuwa ni ishara ya uzalendo. Kwa mtazamo wangu hata tukikosa huu mkopo tutaendelea hivyo hivyo, bali kutakosekana hela ambayo ingeweza kuongeza nguvu kwenye upande huo.
 
Mkuu ningependa kukutaarifu wavulana wanao wapa mimba wanafunzi wenzao wanafungwa jela.
Nina ushahidi wa hili jambo, vijana wenzetu wawili walifungwa jela kwa kuwapa mimba wasichana wawili ambao wote walikuwa darasa moja miaka hiyo.

..tuna sheria kali.

..lakini tatizo halionekani kupungua.

..Nini kifanyike?
 
Mimi ninashindwa kuelewa hizi kelele kuhusu uwezekano wa serikali kupatiwa mkopo wa elimu au la na Benki ya Dunia.

Kinachonishangaza zaidi ni kuona jinsi ambavyo baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali/CCM wanalumbana na wanaharakati na baadhi ya viongozi wa upinzani hasa Zitto Kabwe kuhusu uhalali wa kupewa mkopo au la!

Nikipongeze sana Chama kikuu cha upinzani (CHADEMA) kwa kukaa kando katika malumbano haya ambayo kwa mtazamo wangu hayana mantiki yoyote katika jamii.

Nadhani CHADEMA wameelewa jinsi ambavyo suala la Mimba za utotoni na kuendelea na masomo linavyohitaji uangalifu mkubwa katika kulipatia ufumbuzi kisiasa.

Ukichunguza utagundua wananchi wengi wanadhani sio vizuri mwanafunzi aliyepata mimba, akajifungua halafu akarudi tena kwenye darasa lenye wanafunzi wasio na watoto na kuendelea na masomo. Haishangazi kuona watu wengi wanapinga kwa sababu wananchi wengi nchini bado ni conservative lakini pia imani za dini zinakataza msichana kupata Mimba kabla ya kuolewa.

Wanaharakati na baadhi ya viongozi wa upinzani hasa Zitto wanaona ni sawa mwanafunzi aliyepata mimba ya utotoni na kujifungua lazima arudi tena kwenye darasa lenye wanafunzi wasio na watoto baada ya kujifungua na kuendelea na masomo.

Ieleweke kuwa moja ya sharti muhimu la kupata mkopo huo ni kuhakikisha wasichana wanapewa kipaumbele katika kupata elimu. Hii ni pamoja na wale ambao watapata mimba za utotoni.

Serikali imesema haiwezi kuruhusu wasichana waliozaa wasome darasa moja na wasichana ambao hawajazaa bali itawajengea shule zao na watasoma kwa miaka 2 badala ya minne kwa elimu ya sekondary (O-level) na kama watafaulu watakutana na wanafunzi wengine A-level.

Thamani ya mkopo ni dola za Kimarekani milioni 500. Hata hivyo, hizi pesa hazitolewi kwa mkupuo bali zitatolewa kidogo kidogo kwa miaka 7. Hii ina maana kuanzia 2020-2026.

Hapa chini ni Jedwali linaloonyesha jinsi ambavyo pesa zitatolewa kama mkopo utakubaliwa.
View attachment 1337756
Kama Mkopo utatolewa basi kwa mwaka huu wa fedha tutaletewa jumla ya dola za Kimarekani milioni 8.52 tu.

Ni aibu kwa pande zote hasa serikali kulumbana kupata mkopo badala ya kulumbana jinsi ya kukusanya mapato ya ndani na matumizi yake! Huu ni mkopo for God's sake!

Ni bora angalau malumbano haya yangekuwa ni kuhusu msaada (grant) kwa sababu hauna malipo kama ilivyokuwa kwenye Msaada (grant) wa thamani ya dola za kimarekani milioni 500 uliokuwa utolewe na serikali ya Marekani kupitia kitengo cha Millennium Challenge Corp (MCC) ambao ulisitishwa mwaka 2016.

Cha kujiuliza, Baada ya MCC kusitishwa mwaka 2016 kilitokea nini? Nani alinufaika na nani hakunufaika?

Je, huu mkopo ukitolewa, nani atanufaika na nani hatanufaika?

Je, huu mkopo usipotelewa, nani atanufaika na nani hatanufaika?

Haya ndio maswali muhimu ya kujiuliza?
Acha wakae na vihela vyao. Sisi ni dona kantri.
Hela ya kununua Dreamliner nyingine tunayo.
 
Heko umeeleza vizuri sana. Ila kwa kuongezea hawa mabeberu wanakupa mkopo au msaada wakiwa na lengo la kukufanya tegemezi. Wakiona umetumia vizuri hela na lengo lao halijatimia wanakuzushia jambo wanafuta msaada. Ndio ilivyotokea kwa MCC ya wamarekani. Huu mkopo wa benki ya dunia sisi wenyewe tunaweza kua na hela hizo na kama wanaendelea na masharti ya kipuuzi haijalishi wakibaki na hela zao. Lengo lao ni kutufarakanisha kwa kuwatumia vibaraka wao kina zitto na lissu
 
Mkuu ningependa kukutaarifu wavulana wanao wapa mimba wanafunzi wenzao wanafungwa jela.
Nina ushahidi wa hili jambo, vijana wenzetu wawili walifungwa jela kwa kuwapa mimba wasichana wawili ambao wote walikuwa darasa moja miaka hiyo.
Mtoto akizaliwa atamuuliza mama yake baba yuko wapi mama atasema yuko jela kwa kosa la kuzaliwa wewe mtoto atasema inamaana kuzaliwa Mimi ni kosa? Nae mtoto atailaumu jamii
 
..tuna sheria kali.

..lakini tatizo halionekani kupungua.

..Nini kifanyike?
Ni kweli sheria kali tunahitaji mjadala mpana na tafiti za kina kupunguza tatizo.
Tusisahau Marekani wana sheria kali na hukumu yake ni kifo lakini watu bado wanauwa, hatujasikia watetezi wa haki za binadamu wa Marekani wakiomba serikali yao inyimwe ushirikiano wa kiuchumi na taasisi za kimataifa.
 
Kuna umri ambao watoto hupitia changamoto ya miili yao kubadilika. Lazima tuwaandae kupambana na hali hiyo.

..Kuna umri ambao watoto hujaribu mambo mbalimbali na kufanya makosa mengi. Kwa mfano wako wanaojaribu sigara, pombe, udokozi, mapenzi, etc etc. Watoto wanahitaji kuongozwa vizuri ktk umri huo.

..Binafsi nashauri viongozi wetu na wadau wakae pamoja na kushauriana kuhusu suala hili.
Nashindwa kuwaelewa watz wa leo. We una umri gani?? Isijekuwa una miaka 20 tu unajiona mwenye hekima sana. Hao watoto wamezaliwa leo katika muhula huu wa awamu ya 5?? Kwa nini suala hili mlivalie njuga kiasi hiki?? Namuunga mkono rais kuwa; Hatuna shule za kuwaweka hao wamama wenye watoto wao. Kama wakiamua kuzaa basi waendelee kuzaa. Tena hata hao waliowajaza mimba natamani wasiguswe ili waje kulelea hao watoto wao.
Hatuna haja ya kujadiliana bali iwe hivyo. Kwisha and full stop. Mwisho wa mjadala. Lazimatufike mahali tujue kuwa; Mikopo yenye masharti mwisho wake ndio huo. Kulamba viatu vyao. Tunauuza utu wetu mchana peupeee. Hebu turudi nyumbani kujadili namna ya kutafuta pesa zetu wenyewe. Tanzania tumebarikiwa mno mno. Tuna mbuga za wanyama kuliko popote duniani. Badala ya kuzitangaza tunaenda kutangaza sura za mawaziri wetu. Tanzania tuna madini ambayo hayatakaa yaishe. Badala ya mikataba ya kutuinua sisi tunaenda kupatana nao kwa mapato kiduchu. Acheni hizo dhahabu zikae humo ardhini haziozi. Tuna gas asilia ujazo wa kufa mtu. Badala ya kuigema tunaenda kuwaita wachina kuja kujizolea.
Huo mkopo usije kama wanatuwekea masharti ya kipuuzi. Hatutakufa njaa
 
Unamawazo mazuri,naomba nikukumbushe kwann serikali imegusha eneo baya...wote wamelia.....kwamwezi serikali inapeleka ruzuku shule zamsingi nchi zima..kila kijiji kunashule na vijiji viko karibia 19000..ruzuku yenyewe ni 50000.sasa chukua 50000x 19000 utaona serikali kuhusu huo mkopo hatakama nikwaawamu kunapahala wasipopewa itakua kituko piga ua wanaomba isitokee kutopewa....ushauriwangu serikali yangu iongezee wizara ,iitwe wizara ya elimu msingi.....secondary nayo iundiwe wizara...lakini vijiji navyo viundiwe wizara.....lasivyo tunazidi kupotea serikali iliyosema inaweza kudoneti kwenye nchi nyingine inalia lia kunyimwa mkopo tena imeshindwa kujiwekea bajeti yandani kwenye elimu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona wagumu kuelewa ninyi? Sawa ilikuwa hivyo, ulimi uliponza kichwa. Awamu ya 5 imwkuwa na maneno mengi ya kutafuta misifa bila kutafakari kwanza unatoa Nini mdomoni, kwa Nani na impact yake Ni Nini. Kwani miaka yote iliyopita watoto walikuwa wanafukuzwa wa mimba, lakini initiative binafsi wanarudi shuleni Mambo yanaendelea. Kilichofanya awamu hii kuropoka hadharani ilikuwa kutafuta misifa au? Ina Sasa imeshakuwa Soo. Inabidi Sasa hiyo awamu iliyotamka hayo hadharani iyengue kauli hizo, yaani Sasa irasmishe watiwa mimba kurudi shureni bila masharyi, hakuna namna Tena vinginevyo mkopo no

We ndio umeongea ukweli, hizo hadithi za kusema eti Zito ndio kazui huo mkopo ni kutaka kutupotezesha ukweli. Zile kauli za kibabe na kiburi cha kijinga ndio matokeo yake haya.
 
Nashindwa kuwaelewa watz wa leo. We una umri gani?? Isijekuwa una miaka 20 tu unajiona mwenye hekima sana. Hao watoto wamezaliwa leo katika muhula huu wa awamu ya 5?? Kwa nini suala hili mlivalie njuga kiasi hiki?? Namuunga mkono rais kuwa; Hatuna shule za kuwaweka hao wamama wenye watoto wao. Kama wakiamua kuzaa basi waendelee kuzaa. Tena hata hao waliowajaza mimba natamani wasiguswe ili waje kulelea hao watoto wao.
Hatuna haja ya kujadiliana bali iwe hivyo. Kwisha and full stop. Mwisho wa mjadala. Lazimatufike mahali tujue kuwa; Mikopo yenye masharti mwisho wake ndio huo. Kulamba viatu vyao. Tunauuza utu wetu mchana peupeee. Hebu turudi nyumbani kujadili namna ya kutafuta pesa zetu wenyewe. Tanzania tumebarikiwa mno mno. Tuna mbuga za wanyama kuliko popote duniani. Badala ya kuzitangaza tunaenda kutangaza sura za mawaziri wetu. Tanzania tuna madini ambayo hayatakaa yaishe. Badala ya mikataba ya kutuinua sisi tunaenda kupatana nao kwa mapato kiduchu. Acheni hizo dhahabu zikae humo ardhini haziozi. Tuna gas asilia ujazo wa kufa mtu. Badala ya kuigema tunaenda kuwaita wachina kuja kujizolea.
Huo mkopo usije kama wanatuwekea masharti ya kipuuzi. Hatutakufa njaa

..kila Mtz anatakiwa apatiwe nafasi ya kujiendeleza kielimu mpaka pale uwezo wake utakapokemea.

..Pia naona tumejielekeza zaidi ktk kuadhibu wanaopata mimba, badala ya kutafuta mbinu na kuchukua hatua zitakazosaidia kupunguza mimba.
 
Hakuna anayetaka mtu azuiwe kuipata elimu. Ndo maana ni sheria kila mtoto aandikishwe shule ikifika umri wake. Tena hakuna aliyejielekeza kwenye adhabu bali tunataka msichana anayejijua kuwa kuvua pichu yake iwe kwa kudanganywa au kwa kiherehere chake akiipata mimba shule ndio mwisho. Mzazi wake hatapoteza pesa yake kumsomesha mke wa mtu.
Msichana akiisha kuonja mautamu hayo ya kukojolewa hata mtihani hatasoma bali ni kulala kwa mwalimu tu kesho apewe majibu.
Acheni kuutetea huu ujinga. Wazungu wanataka kutamaliza kwa kulambishwa visukari hivi.
Huyo msichana asiyejua kuwa ngono ni chanzo cha matatizo ni nani?? Je, ni wasichana wote wanatoa pichu zao kila siku?? Huoni huruma wale wanaotembea kwa miguu toka Jangwani hadi Magomeni wakati wenzao wanapelekwa na kurudishwa na magari ya wapenzi wao?? Acheni kuwatetea
 
Mkuu nimeheshimu mawazo yako maana kwa sehemu kubwa yana mantiki tena ya wazi. Ila naona hapo ulipochomeka kuhusu Zito kama hujaweka sawa. Ni kweli bank ya dunia imemsikikiza Zito ndio ikaacha kutoa huo mkopo bila kujiridhisha na hali halisi? Kama bank ya dunia inaweza kumsikiliza Zito na kutii, unataka kusema akienda kutaka mkopo kwa ajili ya nchi tutapewa? Kama umeamua kujenga hoja, hebu baki kwenye sababu za msingi, na sio kuokota maoni ya siasa chafu na kuja kuchafua maoni yako mazuri. Huyo Zito ametajwa sana ili kuficha ukweli pindi tukinyimwa huo msaada ionekane ni yeye, lakini ukweli uko wazi hao bank ya dunia hawakutegemea maombi ya Zito kusisitisha huo mkopo.

Ukweli ni lugha za rais kuhusu hao wanafunzi waliopata mimba umepelekea maamuzi ya WB. Kibaya zaidi hata maofisa wa serikali hawakuonyesha kutumia lugha za kurekebisha alichoongea rais wetu. Katika mazingira hayo unategemea well saidhao WB wachukue hatua gani? Alichofanya Zito ni kusoma tu mazingira halisi ya maamuzi ya hicho kikao, na yeye akatupia karata yake humo humo. Kilichotugharimu kwenye huu mkopo ni kiburi cha kijinga, na kiburi hiki kinalazimishwa kuwa ni ishara ya uzalendo. Kwa mtazamo wangu hata tukikosa huu mkopo tutaendelea hivyo hivyo, bali kutakosekana hela ambayo ingeweza kuongeza nguvu kwenye upande huo.
Mkuu nimeheshimu mawazo yako maana kwa sehemu kubwa yana mantiki tena ya wazi. Ila naona hapo ulipochomeka kuhusu Zito kama hujaweka sawa. Ni kweli bank ya dunia imemsikikiza Zito ndio ikaacha kutoa huo mkopo bila kujiridhisha na hali halisi? Kama bank ya dunia inaweza kumsikiliza Zito na kutii, unataka kusema akienda kutaka mkopo kwa ajili ya nchi tutapewa? Kama umeamua kujenga hoja, hebu baki kwenye sababu za msingi, na sio kuokota maoni ya siasa chafu na kuja kuchafua maoni yako mazuri. Huyo Zito ametajwa sana ili kuficha ukweli pindi tukinyimwa huo msaada ionekane ni yeye, lakini ukweli uko wazi hao bank ya dunia hawakutegemea maombi ya Zito kusisitisha huo mkopo.

Ukweli ni lugha za rais kuhusu hao wanafunzi waliopata mimba umepelekea maamuzi ya WB. Kibaya zaidi hata maofisa wa serikali hawakuonyesha kutumia lugha za kurekebisha alichoongea rais wetu. Katika mazingira hayo unategemea hao WB wachukue hatua gani? Alichofanya Zito ni kusoma tu mazingira halisi ya maamuzi ya hicho kikao, na yeye akatupia karata yake humo humo. Kilichotugharimu kwenye huu mkopo ni kiburi cha kijinga, na kiburi hiki kinalazimishwa kuwa ni ishara ya uzalendo. Kwa mtazamo wangu hata tukikosa huu mkopo tutaendelea hivyo hivyo, bali kutakosekana hela ambayo ingeweza kuongeza nguvu kwenye upande huo.
Well said!
 
Heko umeeleza vizuri sana. Ila kwa kuongezea hawa mabeberu wanakupa mkopo au msaada wakiwa na lengo la kukufanya tegemezi. Wakiona umetumia vizuri hela na lengo lao halijatimia wanakuzushia jambo wanafuta msaada. Ndio ilivyotokea kwa MCC ya wamarekani. Huu mkopo wa benki ya dunia sisi wenyewe tunaweza kua na hela hizo na kama wanaendelea na masharti ya kipuuzi haijalishi wakibaki na hela zao. Lengo lao ni kutufarakanisha kwa kuwatumia vibaraka wao kina zitto na lissu

Si kila mtu ni juha humu ndani, acha upotoshaji usiokuwa na maana yoyote. Taja siku waliyotoa mkopo/ misaada kisha wakaona hawajafanikiwa kisha wakafuta. Pesa za MCC serekali yetu ilizakataa baada ya wao kutaka utaratibu ufuatwe kutokana na kilichotokea uchaguzi wa Zanzibar. Hizo pesa za MCC zilitoka muda wote wa JK na miradi kadhaa ya umeme na barabara ilitekelezwa kwa pesa hizo. Hao MCC. Wanakosa gani kuhoji ule uhuni wa uchaguzi wa Zanzibar kushughulikiwa? Ni nani ambaye hajui kuwa uchaguzi ule matokeo yalipinduliwa kwa faida ya ccm?

Wote mlioishiwa hoja mnataja Zito na Lissu ili kuwapata wenye uwezo mdogo wa kupambanua mambo. Tunajua fika ni kwanini WB wamesitisha huo mkopo. Mnaweza kuwataja kina Zito na Lisu ili kutopoteza maboya, lakini hatudanganyiki.
 
Hakuna anayetaka mtu azuiwe kuipata elimu. Ndo maana ni sheria kila mtoto aandikishwe shule ikifika umri wake. Tena hakuna aliyejielekeza kwenye adhabu bali tunataka msichana anayejijua kuwa kuvua pichu yake iwe kwa kudanganywa au kwa kiherehere chake akiipata mimba shule ndio mwisho. Mzazi wake hatapoteza pesa yake kumsomesha mke wa mtu.
Msichana akiisha kuonja mautamu hayo ya kukojolewa hata mtihani hatasoma bali ni kulala kwa mwalimu tu kesho apewe majibu.
Acheni kuutetea huu ujinga. Wazungu wanataka kutamaliza kwa kulambishwa visukari hivi.
Huyo msichana asiyejua kuwa ngono ni chanzo cha matatizo ni nani?? Je, ni wasichana wote wanatoa pichu zao kila siku?? Huoni huruma wale wanaotembea kwa miguu toka Jangwani hadi Magomeni wakati wenzao wanapelekwa na kurudishwa na magari ya wapenzi wao?? Acheni kuwatetea

..naona uko zaidi kwenye kuadhibu badala ya kuzuia au kuepusha wanafunzi na vishawishi vya ngono.

..hoja yangu ni kuwa, is there anything we can do, in addition to adhabu kali tulizonazo, ili kuepusha mimba mashuleni?

..Ikifika mahali msichana na mvulana wakavua nguo zao za ndani maana yake ni kwamba kama wazazi, walezi, waalimu, na jamii tumechelewa ktk kuwaongoza watoto hao.

..Pia kama jamii tunawasaidiaje waliopata mimba ili waendelee na masomo, kama wanapenda kuendelea, au kuwapatia mafunzo ya aina nyingine yatakayowawezesha kujitegemea na kuwa productive?
 
Ni kweli sheria kali tunahitaji mjadala mpana na tafiti za kina kupunguza tatizo.
Tusisahau Marekani wana sheria kali na hukumu yake ni kifo lakini watu bado wanauwa, hatujasikia watetezi wa haki za binadamu wa Marekani wakiomba serikali yao inyimwe ushirikiano wa kiuchumi na taasisi za kimataifa.

Mkuu una maoni mazuri, lakini hapo ulipotoa mfano wa huko Marekani kuwa kuna uhalifu na haujawahi kusikia watetezi wa haki za binadamu wakitaka serikali yao inyimwe ushirikiano wa kiuchumi, naona kama unalazimisha hii hoja yako yenye uzuri baadhi ya sehemu ikose nguvu. Marekani ni nchi inayoendeshwa kwa mifuko tena imara, kwenye nchi yao mifumo ina nguvu kuliko mtu. Huku kwetu kuna watu wana kinga za kisheria kutoshtakiwa kwa lolote, kibaya zaidi mwenye hiyo kinga anatumia pia madaraka yake kuzuia mashitaka ya kisheria kwa watu wa genge lake, na hata baadhi ya sheria kufanya kazi. Marekani katiba ndio inaongoza nchi, hapa kwetu katiba inatekelezwa kwa utashi wa rais aliye madarakani. Hebu achana na huo mfano wa Marekani kwa kuifananisha na nchi ambayo bado kuna elimu ya watu kutumia choo.
 
Mimi ninashindwa kuelewa hizi kelele kuhusu uwezekano wa serikali kupatiwa mkopo wa elimu au la na Benki ya Dunia.

Kinachonishangaza zaidi ni kuona jinsi ambavyo baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali/CCM wanalumbana na wanaharakati na baadhi ya viongozi wa upinzani hasa Zitto Kabwe kuhusu uhalali wa kupewa mkopo au la!

Nikipongeze sana Chama kikuu cha upinzani (CHADEMA) kwa kukaa kando katika malumbano haya ambayo kwa mtazamo wangu hayana mantiki yoyote katika jamii.

Nadhani CHADEMA wameelewa jinsi ambavyo suala la Mimba za utotoni na kuendelea na masomo linavyohitaji uangalifu mkubwa katika kulipatia ufumbuzi kisiasa.

Ukichunguza utagundua wananchi wengi wanadhani sio vizuri mwanafunzi aliyepata mimba, akajifungua halafu akarudi tena kwenye darasa lenye wanafunzi wasio na watoto na kuendelea na masomo. Haishangazi kuona watu wengi wanapinga kwa sababu wananchi wengi nchini bado ni conservative lakini pia imani za dini zinakataza msichana kupata Mimba kabla ya kuolewa.

Wanaharakati na baadhi ya viongozi wa upinzani hasa Zitto wanaona ni sawa mwanafunzi aliyepata mimba ya utotoni na kujifungua lazima arudi tena kwenye darasa lenye wanafunzi wasio na watoto baada ya kujifungua na kuendelea na masomo.

Ieleweke kuwa moja ya sharti muhimu la kupata mkopo huo ni kuhakikisha wasichana wanapewa kipaumbele katika kupata elimu. Hii ni pamoja na wale ambao watapata mimba za utotoni.

Serikali imesema haiwezi kuruhusu wasichana waliozaa wasome darasa moja na wasichana ambao hawajazaa bali itawajengea shule zao na watasoma kwa miaka 2 badala ya minne kwa elimu ya sekondary (O-level) na kama watafaulu watakutana na wanafunzi wengine A-level.

Thamani ya mkopo ni dola za Kimarekani milioni 500. Hata hivyo, hizi pesa hazitolewi kwa mkupuo bali zitatolewa kidogo kidogo kwa miaka 7. Hii ina maana kuanzia 2020-2026.

Hapa chini ni Jedwali linaloonyesha jinsi ambavyo pesa zitatolewa kama mkopo utakubaliwa.
View attachment 1337756
Kama Mkopo utatolewa basi kwa mwaka huu wa fedha tutaletewa jumla ya dola za Kimarekani milioni 8.52 tu.

Ni aibu kwa pande zote hasa serikali kulumbana kupata mkopo badala ya kulumbana jinsi ya kukusanya mapato ya ndani na matumizi yake! Huu ni mkopo for God's sake!

Ni bora angalau malumbano haya yangekuwa ni kuhusu msaada (grant) kwa sababu hauna malipo kama ilivyokuwa kwenye Msaada (grant) wa thamani ya dola za kimarekani milioni 500 uliokuwa utolewe na serikali ya Marekani kupitia kitengo cha Millennium Challenge Corp (MCC) ambao ulisitishwa mwaka 2016.

Cha kujiuliza, Baada ya MCC kusitishwa mwaka 2016 kilitokea nini? Nani alinufaika na nani hakunufaika?

Je, huu mkopo ukitolewa, nani atanufaika na nani hatanufaika?

Je, huu mkopo usipotelewa, nani atanufaika na nani hatanufaika?

Haya ndio maswali muhimu ya kujiuliza?
Mimi kitu sijaelewa kwa upande wa watu wanaotaka wanafunzi wenye kupata mimba waendelee, je na adhabu ya miaka 30 jela kwa mtia mimba ifutwe? Maana ukiruhusu hilo la mama kurudi darasani maana yake umehalalisha wanafunzi kupewa mimba.
 
Back
Top Bottom