Je, Serikali ikinyimwa mkopo wa elimu na Benki ya Dunia kutatokea nini?

Je, Serikali ikinyimwa mkopo wa elimu na Benki ya Dunia kutatokea nini?

Labda kama kweli wamenusa matumizi tofauti ya huu mkopo.
Vinginevyo hizi kelele hazieleweki.
Wanaopata mimba ni asilimia chache sana ya wasichana lakini wasichana wengi hawaendelei kielimu kwa sababu ya mazingira ya shule zetu.
Na si hilo tu, kuna issue pia za kisheria na kijamii msichana akipewa mimba akiwa shuleni wanakuwa disturbed kwa hicho kipindi chote, kuwarudisha tu shuleni haitakuwa jibu.

Kama hoja ni mahitaji maalum,
wenzetu walemavu kwenye suala la elimu wanapitia uzoefu mgumu sana. Wengine huko sekondari wanachanganywa hata hawaelewi. Kama tunajali sana kutobagua elimu, je hili nalo limezingatiwa?

Kama hoja ya matumizi fedha hizi kwa ajili ya kampeni za kisiasa, hili laweza kuwa muhimu kuzingatiwa maana CCM wana uzoefu wa kutumia pesa bila taratibu haswa kipindi cha kampeni. Rejea EPA na ESCROW.

Mi naona hivyo, kelele zisizo na mwelekeo wenye kuleta tija pande zote na mwishoe naamini hayo kuna vitu tunafichwa. Na kama tunafichwa na huu ni mkopo WB wabaki na pesa zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mfumo wa elimu CCM ni kuelimisha wachache ili wapate wapiga kura wengi. 💪🏾Kudumu chama cha mapinduzi
 
Aliyeharibu ni aliyekuja kutoa tamko kwamba "watoto waliopata mimba hakuna kurudi darasani" .
Maana kila mtu anajua hata zamani watoto wengi waliopata mimba shule ilikua inaishia pale pale wachache sana ndio walikua wanaendelea..
Jamaa angekaa kimya sidhani kama kingebadirika kitu.
 
Mimi ninashindwa kuelewa hizi kelele kuhusu uwezekano wa serikali kupatiwa mkopo wa elimu au la na Benki ya Dunia.

Kinachonishangaza zaidi ni kuona jinsi ambavyo baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali/CCM wanalumbana na wanaharakati na baadhi ya viongozi wa upinzani hasa Zitto Kabwe kuhusu uhalali wa kupewa mkopo au la!

Nikipongeze sana Chama kikuu cha upinzani (CHADEMA) kwa kukaa kando katika malumbano haya ambayo kwa mtazamo wangu hayana mantiki yoyote katika jamii.

Nadhani CHADEMA wameelewa jinsi ambavyo suala la Mimba za utotoni na kuendelea na masomo linavyohitaji uangalifu mkubwa katika kulipatia ufumbuzi kisiasa. Hata sheria ya ndoa nchini bado ina mabishano mengi kutokana na mila na desturi ambazo bado ni sehemu ya maisha katika jamii nchini.

Ukichunguza utagundua wananchi wengi wanadhani sio vizuri mwanafunzi aliyepata mimba, akajifungua halafu akarudi tena kwenye darasa lenye wanafunzi wasio na watoto na kuendelea na masomo. Haishangazi kuona watu wengi wanapinga kwa sababu wananchi wengi nchini bado ni conservative lakini pia imani za dini zinakataza msichana kupata Mimba kabla ya kuolewa.

Wanaharakati na baadhi ya viongozi wa upinzani hasa Zitto wanaona ni sawa mwanafunzi aliyepata mimba ya utotoni na kujifungua lazima arudi tena kwenye darasa lenye wanafunzi wasio na watoto baada ya kujifungua na kuendelea na masomo.

Ieleweke kuwa moja ya sharti muhimu la kupata mkopo huo ni kuhakikisha wasichana wanapewa kipaumbele katika kupata elimu. Hii ni pamoja na wale ambao watapata mimba za utotoni.

Serikali imesema haiwezi kuruhusu wasichana waliozaa wasome darasa moja na wasichana ambao hawajazaa bali itawajengea shule zao na watasoma kwa miaka 2 badala ya minne kwa elimu ya sekondary (O-level) na kama watafaulu watakutana na wanafunzi wengine A-level.

Thamani ya mkopo ni dola za Kimarekani milioni 500. Hata hivyo, hizi pesa hazitolewi kwa mkupuo bali zitatolewa kidogo kidogo kwa miaka 7. Hii ina maana kuanzia 2020-2026.

Hapa chini ni Jedwali linaloonyesha jinsi ambavyo pesa zitatolewa kama mkopo utakubaliwa.
View attachment 1337756
Kama Mkopo utatolewa basi kwa mwaka huu wa fedha tutaletewa jumla ya dola za Kimarekani milioni 8.52 tu.

Ni aibu kwa pande zote hasa serikali kulumbana kupata mkopo badala ya kulumbana jinsi ya kukusanya mapato ya ndani na matumizi yake! Huu ni mkopo for God's sake!

Ni bora angalau malumbano haya yangekuwa ni kuhusu msaada (grant) kwa sababu hauna malipo kama ilivyokuwa kwenye Msaada (grant) wa thamani ya dola za kimarekani milioni 500 uliokuwa utolewe na serikali ya Marekani kupitia kitengo cha Millennium Challenge Corp (MCC) ambao ulisitishwa mwaka 2016.

Je, huu mkopo ukitolewa, nani atanufaika na nani hatanufaika?

Je, huu mkopo usipotelewa, nani atanufaika na nani hatanufaika?

Swali la msingi la kujiuliza, Baada ya MCC kusitishwa mwaka 2016 kilitokea nini? Jibu ndilo litatoa jibu la maswali yaliyoko juu.

Haya ndio maswali muhimu ya kujiuliza?
Bila haya wapiga debe wanawafanya Watanzania wajinga wakati wao ndio wajinga.
Nini kilichotokea serikali iliponyimwa pesa za MCC? Hamsemi. Hizo pesa za WB nazo mnalilia!
Nguruwe mwitu ana tabia ya ajabu. Akikimbizwa na mbwa, halafu ana mbio, akimuacha anasahau hatari inayimkabili. Anaanza kula nyasi.
1. Kila leo tunajisifia makusanyo makubwa ya mapato ya serikali,
2. Majukwaani tunadai kutekeleza miradi kwa pesa zetu za ndani,
3. Deni la taifa linazidi kupaa, na
4. Wananchi wako hoi kiuchumi!
Tunajitambua?
 
Kwani kuna nini mpaka serikali yetu tukufu, iushikilie bango huu mkopo wa WB??

Barrick si wanatupa kishika uchumba??

Makusanyo ya ndani yamevunja rekodi??

Yaani linakuwa suala fikirishi SANA 2020


Everyday is Saturday.............. 😎
 
Back
Top Bottom