Je, Serikali ikinyimwa mkopo wa elimu na Benki ya Dunia kutatokea nini?

Mfumo wa elimu CCM ni kuelimisha wachache ili wapate wapiga kura wengi. 💪🏾Kudumu chama cha mapinduzi
 
Aliyeharibu ni aliyekuja kutoa tamko kwamba "watoto waliopata mimba hakuna kurudi darasani" .
Maana kila mtu anajua hata zamani watoto wengi waliopata mimba shule ilikua inaishia pale pale wachache sana ndio walikua wanaendelea..
Jamaa angekaa kimya sidhani kama kingebadirika kitu.
 
Bila haya wapiga debe wanawafanya Watanzania wajinga wakati wao ndio wajinga.
Nini kilichotokea serikali iliponyimwa pesa za MCC? Hamsemi. Hizo pesa za WB nazo mnalilia!
Nguruwe mwitu ana tabia ya ajabu. Akikimbizwa na mbwa, halafu ana mbio, akimuacha anasahau hatari inayimkabili. Anaanza kula nyasi.
1. Kila leo tunajisifia makusanyo makubwa ya mapato ya serikali,
2. Majukwaani tunadai kutekeleza miradi kwa pesa zetu za ndani,
3. Deni la taifa linazidi kupaa, na
4. Wananchi wako hoi kiuchumi!
Tunajitambua?
 
Kwani kuna nini mpaka serikali yetu tukufu, iushikilie bango huu mkopo wa WB??

Barrick si wanatupa kishika uchumba??

Makusanyo ya ndani yamevunja rekodi??

Yaani linakuwa suala fikirishi SANA 2020


Everyday is Saturday.............. 😎
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…