Je, Serikali iko tayari kumuwekea ulinzi Ole Sabaya?

Naandika hii si kwa ubaya, nia yangu ni njema kabisa.

Zipo taarifa kwamba Ole Sabaya ameachiwa huru baada ya kukiri makosa, katika uleule mpango tulioutilia mashaka wa Plea bargain, Sabaya amekiri mbele ya Mahakama, pamoja na mengine mengi, amekiri kumsumbua kwa uonevu wa kumsingizia uongo Mfanyabiashara wa kimataifa Alex Swai na kumwibia pesa zake kwa mamilioni.

Nampongeza Sabaya kwa kukiri makosa yake hadharani, tunaamini huko mbele atakiri mengi ikiwemo kuweka chumvi kwenye Magari ya Freeman Mbowe na kuyaharibu.

Ole Sabaya kijana aliyelindwa na Magufuli kwa udi na uvumba hata katika makosa ya wazi ya kijinga sana. Ametenda uovu mwingi sana. Sabaya alimiliki vikundi vya kiharamia vya kupora, kudhulumu, kuiba, kunyanyasa, kupiga na kuna tuhuma za kubaka pia, achilia mbali kuingia Bar kunywa vinywaji na kula nyama bila kulipa yeye na kundi lake.

Sabaya aliyatenda haya huku akilindwa na vyombo vya dola akiwemo OCD wa Hai aliyeitwa Mpina, ulinzi huu aliopewa kwenye uharamia wake alipewa kwa vile alikuwa DC.

Sasa leo anaachiwa akiwa Raia wa kawaida tu huku lundo la watu aliowadhulumu, kuwatesa na kuwapora wakiwa bado wangalipo na wakiwa kwenye maeneo yaleyale aliyowadhulumia, Sabaya alitenda unyama wake mwingi Arusha na Kilimanjaro.

Je, masuala ya ulinzi wake akiwa uraiani yamezingatiwa?
Acha roho mbaya.
 
Sijawahi kusikia wala kuona mshitakiwa amekiri kuhusika na makosa ya kesi za jinai akaachiwa huru kwa Plea Bargain acha mbali mwenye kesi 7 za jinai, ambazo ni pamoja na Uhujumu Uchumi, matumizi mabaya ya madaraka na Uongozi wa genge la Majambazi ati kaachiwa huru baada ya kukiri makosa yote hayo - Only in Tanzania
 
Nenda kakae wewe jela
 
Huyo anayetaka kumdhuru Sabaya aende akatolewe utumbo uliojaa Mbege na Konyagi.
 
Sijawahi kusikia wala kuona mshitakiwa amekiri kuhusika na makosa ya kesi za jinai akaachiwa huru kwa Plea Bargain acha mbali mwenye kesi 7 za jinai, ambazo ni pamoja na Uhujumu Uchumi, matumizi mabaya ya madaraka na Uongozi wa genge la Majambazi ati kaachiwa huru baada ya kukiri makosa yote hayo - Only in Tanzania
Inashangaza sana ! Lakini tumeambiwa humu kuna mwenye tuzo kwenye Jukwaa la Sheria Pascal Mayalla nina uhakika atakuja kulitolea ufafanuzi
 
Back
Top Bottom