Je, Serikali iko tayari kumuwekea ulinzi Ole Sabaya?

Acha wamgawane nyama huyu jamaa hana hata aibu ila siku akienda Kanisani kusema hadharani alitumia madaraka na umri wake ulimsukuma kufanya mambo ya kijingw

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Sidhani kama kuna kanisa litampokea huyu jamaa , maana amehujumu hadi Masista wa kanisa
 
Je, kengeza aliyemuua chacha wangwe na kufanya jaribio la kumuua Tundu lisu anaulinzi? Pia mkifanya uchaguzi wa mwenyekiti mwingine wa NGO yenu mtujulishe.
Hizi ndo akili za CCM..... idiots mmeshindwa kuwahakikishia watanzania huduma ya umeme na maji ya uhakika miaka 60 ya uhuru
 
Kwani makonda anaishije mpaka sabaya ashindwe kuishi mpaka awekewe ulinzi.
 
Sijawahi kusikia wala kuona mshitakiwa amekiri kuhusika na makosa ya kesi za jinai akaachiwa huru kwa Plea Bargain acha mbali mwenye kesi 7 za jinai, ambazo ni pamoja na Uhujumu Uchumi, matumizi mabaya ya madaraka na Uongozi wa genge la Majambazi ati kaachiwa huru baada ya kukiri makosa yote hayo - Only in Tanzania
Plea Bargain ni special kwa watu wakubwa tu Budah, moja ya condition yake ni kukili kosa. Hivi L.O.S kisheria yuko sahihi na mahakama pia iko sahihi. NB: Hakuna plea Bargain ya lower class.
 
Hao unaosema wampe ulinzi mara utasikia wanakata rufaa hawajaridhishwa na hukumu
. Hahahaa usicheze na hii nchi
 
Uraiani anakumudu. Ondoa shaka!!
Hata hivyo, akiguswa Hata unyoya, wanajua wataanzia wapi kumpata aliyemgusa. Kwa haraka naona ni nani anatakiwa kuwa na wasiwasi.
 
Na kulingana na sheria zetu, huyu jambazi haruhusiwi kugombea cheo CHOCHOTE KILE au kuteuliwa.
 
Naandika hii si kwa ubaya, nia yangu ni njema kabisa.

Zipo taarifa kwamba Ole Sabaya ameachiwa huru baada ya kukiri makosa, katika uleule mpango tulioutilia mashaka wa Plea bargain, Sabaya amekiri mbele ya Mahakama, pamoja na mengine mengi, amekiri kumsumbua kwa uonevu wa kumsingizia uongo Mfanyabiashara wa kimataifa Alex Swai na kumwibia pesa zake kwa mamilioni.

Nampongeza Sabaya kwa kukiri makosa yake hadharani, tunaamini huko mbele atakiri mengi ikiwemo kuweka chumvi kwenye Magari ya Freeman Mbowe na kuyaharibu.

Ole Sabaya kijana aliyelindwa na Magufuli kwa udi na uvumba hata katika makosa ya wazi ya kijinga sana. Ametenda uovu mwingi sana. Sabaya alimiliki vikundi vya kiharamia vya kupora, kudhulumu, kuiba, kunyanyasa, kupiga na kuna tuhuma za kubaka pia, achilia mbali kuingia Bar kunywa vinywaji na kula nyama bila kulipa yeye na kundi lake.

Sabaya aliyatenda haya huku akilindwa na vyombo vya dola akiwemo OCD wa Hai aliyeitwa Mpina, ulinzi huu aliopewa kwenye uharamia wake alipewa kwa vile alikuwa DC.

Sasa leo anaachiwa akiwa Raia wa kawaida tu huku lundo la watu aliowadhulumu, kuwatesa na kuwapora wakiwa bado wangalipo na wakiwa kwenye maeneo yaleyale aliyowadhulumia, Sabaya alitenda unyama wake mwingi Arusha na Kilimanjaro.

Je, masuala ya ulinzi wake akiwa uraiani yamezingatiwa?

Kama ana busara aanze maisha mapya hata Tandahimba huko, ila wa Tanzania si walipa visasi, nature itamhudumia.
 
Awekwe ulinzi kwani yale Maguvu aliyokuwa nayo yameyeyuka,🤔.Kwani Jela aling'olewa nywele🤔
 
Back
Top Bottom