Je, Serikali ya Awamu ya sita ni Tawi la Serikali ya Awamu ya Nne?

Je, Serikali ya Awamu ya sita ni Tawi la Serikali ya Awamu ya Nne?

ONDOA "Je" uliyoanza nayo. Na mwisho ONDOA "?" na badala yake weka alama .
 
Mambo mengi yanayoendelea kwenye Serikali ya Awamu ya sita mengi yanashabihiana na yaliyokuwa yanafanyika kwenye Serikali ya Awamu ya Nne. Mfano uteuzi katika nafasi mbalimbali sura nyingi ni zile za Awamu ya Nne.

Ubadhirifu wa mali za umma hazijibiwi kabisa au hazifanyiwi suluhisho. Fedha zinarudi kwa watu binafsi baadhi na mambo mengine mengi yanashabihiana na yaliyokuwa yanafanyika kwenye Serikali ya Awamu ya Nne.

Je, hili ni Tawi lake? Karibuni kwa mjadala kuhusu hili na nini tushauriane.
Unauliza matako ya mbwa ilhali mkia unauona wewe vipi mkuu?
 
Awamu ya 6 ni akisi ya awamu ya 5
Ni bas tu Mungu aliwai kumuondoa mapema kumuepusha na aibu ila ndo tulikua tunaelekea ni bas tu kawai kuruka kwenye bas wakat bado liko kwa safari
 
hata ya awamu ya tano ilikuwa tawi la awamu ya tatu sema tu tawi lenyewe likakonyolewa kwa mabadiliko ya Tabia nchi

Sent from my SM-G9500 using JamiiForums mobile app
Kuna wakati nahudhunika sana..sio mabadiliko ya tabia nchi. Nikiona haya ya sasa, pengine ni mabadiliko ya tabia watu.

Watu wanajipanga bwana...watu wana project zao bwana...ila sasa zimefeli.

Awamu ya tatu, uchumi ulianza kuonyesha mwanga wa kukua...na awamu ya tano, ubabe na kuendeleza miundombinu kwa gharama yoyote. na vitu vilionekana.

Ila mwenye macho haambiwi tazama...muda unazidi kuongea. Tutaandika vitabu na vitabu vya hizi project zilizofanyika.

Pengine watoto na mihimili imara ya uongozi wa Taifa letu itaibuka na watakuwa wamejifunza.

Kitu ambacho nina uhakika nacho ni kimoja tu..Tanzania sio mali binafsi ya watu fulani wachache. wataibuka watu wema na kuongoza wengine kuelekea nchi ya ahadi...ya maziwa na asali. Kwa sasa, nina mashaka kama huko ndio tunakoelea
 
kuna watu bado mmezungukwa na koti la ujamaa kwny akili zao. Waasisi wenyewe wa Ujamaa China na Urusi sasa hivi wanazalisha Mabilionea kuliko Mabepari

Sent from my SM-G9500 using JamiiForums mobile app
Sio ujamaa mkuu...tunataka uongozi bora. Mwizi awajibishwe. Mtu anayetumia madaraka ya umma vibaya awajibishwe. Anayefanya kazi zake na kupata alindwe.
Ujamaa ulituletea shida. Ukosefu wa nidhamu na ulafi wa mali ya umma ukifanywa na wachache pia utatuletea shida. Hili boti linatuhusu sote. Hakuna namna lazima tujue namna ya kubebana ili tufike
 
Tumefika mahali ambapo wizi wa kura unaonekana wa maana kuliko kupata kura za halali. Sifa ya Msimamizi wa uchaguzi ni yule mahiri kwa kuiba kura ili watawala wabaki madarakani.
 
Sio ujamaa mkuu...tunataka uongozi bora. Mwizi awajibishwe. Mtu anayetumia madaraka ya umma vibaya awajibishwe. Anayefanya kazi zake na kupata alindwe.
Ujamaa ulituletea shida. Ukosefu wa nidhamu na ulafi wa mali ya umma ukifanywa na wachache pia utatuletea shida. Hili boti linatuhusu sote. Hakuna namna lazima tujue namna ya kubebana ili tufike
Uongozi bora sio kuchukia Individuals wenye ukwasi.

Sent from my SM-G9500 using JamiiForums mobile app
 
Mambo mengi yanayoendelea kwenye Serikali ya Awamu ya sita mengi yanashabihiana na yaliyokuwa yanafanyika kwenye Serikali ya Awamu ya Nne. Mfano uteuzi katika nafasi mbalimbali sura nyingi ni zile za Awamu ya Nne.

Ubadhirifu wa mali za umma hazijibiwi kabisa au hazifanyiwi suluhisho. Fedha zinarudi kwa watu binafsi baadhi na mambo mengine mengi yanashabihiana na yaliyokuwa yanafanyika kwenye Serikali ya Awamu ya Nne.

Je, hili ni Tawi lake? Karibuni kwa mjadala kuhusu hili na nini tushauriane.
Sio tawi ni pete na kidole.
 
Haiwezeni watu waonekani hawafai katika Serikali ya Awamu ya Tano halafu waonekane wanafaa kwenye Serikali ya Awamu ya sita kama si kulindana na kuendekeza ubadhirifu wa mali za umma.
 
Back
Top Bottom