Je, Serikali ya Awamu ya sita ni Tawi la Serikali ya Awamu ya Nne?

Je, Serikali ya Awamu ya sita ni Tawi la Serikali ya Awamu ya Nne?

Mambo mengi yanayoendelea kwenye Serikali ya Awamu ya sita mengi yanashabihiana na yaliyokuwa yanafanyika kwenye Serikali ya Awamu ya Nne. Mfano uteuzi katika nafasi mbalimbali sura nyingi ni zile za Awamu ya Nne.

Ubadhirifu wa mali za umma hazijibiwi kabisa au hazifanyiwi suluhisho. Fedha zinarudi kwa watu binafsi baadhi na mambo mengine mengi yanashabihiana na yaliyokuwa yanafanyika kwenye Serikali ya Awamu ya Nne.

Je, hili ni Tawi lake? Karibuni kwa mjadala kuhusu hili na nini tushauriane.
Unauliza JIBU?
 
Ni setikali kamili
Lakini kichwa cha serikali ana mambo yake anayoyaelewa mwenyewe.

Tuishi naye hadi tutakapomstaafisha kwa kura zetu hapo 2025
 
kuna watu bado mmezungukwa na koti la ujamaa kwny akili zao. Waasisi wenyewe wa Ujamaa China na Urusi sasa hivi wanazalisha Mabilionea kuliko Mabepari

Sent from my SM-G9500 using JamiiForums mobile app
Ubepari uwepo sawa,lakini sio ukwasi wa wizi wa mali ya umma upewe jina la ubepari,na wanaopinga huo wizi eti wajamaa,
 
Haiwezeni watu waonekani hawafai katika Serikali ya Awamu ya Tano halafu waonekane wanafaa kwenye Serikali ya Awamu ya sita kama si kulindana na kuendekeza ubadhirifu wa mali za umma.
Hii awamu ya Samia itaacha kovu kubwa kweli kweli kwenye historia ya Tanzania. Na-predict kuwa ndiyo awamu itakayosababisha mabadiliko ya mfumo yatokee kwani upigaji ni wa kiwango cha juu. Nasikia mama mwenyewe ameshakuwa bilionia sasa hivi. Biashara ya madawa ya kulevya imeshamiri na Kinana yupo.
 
Ni suala la muda tu. Msemaji wa Tanesco alikiri kuwa kuna upungufu wa umeme thats why umeme unatolewa kwa mgao.

Sasa Ile kauli ya Waziri Biteko kuwaambia Tanesco wafanye wafanyavyo ili umeme upatikane hapo ndiyo mission inaenda kutimia, utasikia ishu ya dharula ya umeme, hapo ndiyo hao wakina IPTL na Symbion ndiyo wata take advantage.

Hili draft linachezwa kwa ustadi mkubwa na mafisadi. Watu wanataka kurudisha pesa zao.
Tena kwa kasi sana kurudisha pesa zao
 
Ajira sasa zinapatikana kwa kujuana na si kwa kuangalia sifa za elimu. Wakubwa wanajipendelea kwa kujiongezea maslahi. Teuzi nazo ni kwa kujuana. Mtumishi wa umma anatamba kwa ukwasi alioiba kwenye hazina ya umma aliyoaminiwa kusimamia. Mifano ipo kwenye ripoti ya CAG na Mkataba wa DPWorld una harufu ya upigaji.
 
Pigia kabisa mstari. ➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖
Hilo ulilouliza ni jibu. Na siyo swali. Na hata huu mgao wao wa umeme wa sasa, unaweza kuta una jambo nyuma ya pazia. Muda si mrefu utashangaa akina IPTL, Agreco, Richmond, Dowans, Symbion, na wengineo wengi; wamerejeshwa kinyemela.
Hayo pia wananchi tuyapinge kama suala la Bandari na DP world.
 
Mambo mengi yanayoendelea kwenye Serikali ya Awamu ya sita mengi yanashabihiana na yaliyokuwa yanafanyika kwenye Serikali ya Awamu ya Nne. Mfano uteuzi katika nafasi mbalimbali sura nyingi ni zile za Awamu ya Nne.

Ubadhirifu wa mali za umma hazijibiwi kabisa au hazifanyiwi suluhisho. Fedha zinarudi kwa watu binafsi baadhi na mambo mengine mengi yanashabihiana na yaliyokuwa yanafanyika kwenye Serikali ya Awamu ya Nne.

Je, hili ni Tawi lake? Karibuni kwa mjadala kuhusu hili na nini tushauriane.
Role model wake ni wa awamu ya nne.
 
Awamu mbili za hovyo sana, japo ya nne "sikuifaidi sana"!
 
Tumbuatumbua ya sasa ni kama maigizo tu. Ni kulindana kwa kwenda mbele kama ilivyokuwa Awamu ya Nne.
 
Acha pesa zirudi mtaani tupate mabilionea wapya, watengeneze ajira kwa wingi...uchumi usonge
 
Back
Top Bottom