Je, Serikali ya Magufuli kuwatosa Wapalestina? Netanyahu anakuja Afrika ya Mashariki

Je, Serikali ya Magufuli kuwatosa Wapalestina? Netanyahu anakuja Afrika ya Mashariki

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
17,047
Reaction score
63,206
Tunamjua Rais wetu, akipewa heshima kubwa ya kubumba (charm offensive) au kusifiwa basi ataenda extra mile hadi kuichanachana misingi iliyowekwa na watangulizi wake.

Sote tunafahamu kuwa sera ya nchi yetu kuhusu mgogoro wa Wapalestina na Waisrael ni kusimama na Wapalestina ili wapate haki yao, ya kuwa huru katika nchi yao lakini wakati huo huo tukitambua haki ya utaifa wa Israel.

Baada ya raisi Magufuli kuingia madarakani alionekana kubadili msimamo wetu wa sera yetu ya nje kwa kuachana na Kuwa upande wa Sahara magjaribi na kuikumbatia Morocco ambayo ni wakoloni wanaoikalia Sahara magharibi. Hii ilitokana na ujio wa mfalme wa Morocco hapa nchini mwetu aliyeahidi misaada kadhaa ikiwemo ujenzi wa mpira. Yaani tulibadili msimamo wa nchi yetu wa toka mwalimu kwa sababu ya uwanja wa mpira na kutokana na bwana mkubwa kupewa heshima ya kutembelewa na mfalme!!

Leo hii Netanyahu anakuja Uganda, miongoni mwa mambo anayokuja kuzungumza ni:

1) Uganda ikubali vipesapesa ili ikubali kuwapokea ndugu zetu, weusi wenzetu wanaofukuzwa Israel kama Mbwa. Yaani watu waliokimbilia Israel kama wakimbizi wa kiuchumi basi wasakwe, wawe deported na nchi zilizokubali kuwapokea ni Rwanda na Uganda, in exchange ya Rwanda na Uganda kuwapokea watu hao ni kupewa vipesapesa na ushirikiano mwingine kutoka Israel.

Ni uwendawazimu hizi nchi zinachokifanya!!. Badala ya kuitaka Israel iheshimu mikataba ya kimataifa juu ya Immigrants mbalimbali wakiwemo Illegal immigrants zenyewe zimekubali kuwa mercineries wa Israel kufanya dirty job kwa niaba ya Taifa hilo kwa malipo ya vipesapesa vidola vichache. Sisi watsnzania tukaetae hilo!

2) Pili Netanyahu anakuja Afrika ya Mashariki, kuziomba nchi hizi zikubaliane na plan ya dhulma ya Trump katika kumega ardhi ya Wapalestina kule West bank ns kulimilikisha Taifa la Israel. Netanyahu anataka hizi nchi ziiunge mkono Israel kwenye Umoja wa Mataifa, anataka hizi nchi zibariki dhulma, uonevu dhidi ya Wapalestina.

Lakini pia anataka kuwa kama zitashindwa kusimama waziwazi dhidi ya Uonevu wa Israel basi zi ABSTAIN kwenye kura ambazo Wapalestina wanaitisha kwenye UN ili kupata uungwaji mkono wa mataifa mbalimbali duniani juu ya madhila wanayopitia.

Netanyahu anataka kutununua ili tuuze ile sense yetu ya haki, na msimamo wenye heshima ya utu ili tuwatose wapalestina.

Netanyahu anataka kuja na package za ushirikiano wa ulinzi na nchi hizi ili kuwalainisha viongozi wetu hawa. Na maadamu viongozi wetu hawa wanapenda haya. mambo ya kudukuadukua, basi si ajabu Netanyahu akawaahidi kuwa yupo tayari kuwapa tekinolojia hiyo in exchange ya kuwatosa Wapalestina wanaonyanyaswa.

Kitu kingine, hata hili zuio la greencard ya kuingia marekani huenda ni ujumbe Trump anatuma kwetu kuwa tusipokubaliana na American foreign policy juu ya huu mgogoro wa Palestina na Israel basi Trump atatuminya, Jiulize kwa nini wametarget nchi mbili influential Mashariki mwa Afrika (Tanzania) na Magharibi mwa Afrika (Nigeria), Trump anataka kutumia hii escalation ya kidiplomasia kama BLACKMAIL kwetu kununua uungwaji mkono wetu kidiplomasia kwenye UN.

Hii ishu ya Makonda ni bosheni tu, kwani Makonda wamemjua leo? Makonda ametumika kama boogeyman, na kwa kuwa Wamarekani wanajua hatumpendi huyo kijana basi nao wamepitia mlemle ili kutupumbaza kumbe huku behind the scene wanaipiga nchi yetu pressure ili tuunge mkono mipango ya Trump na Netanyahu.

Hapa kuna karata za Geopolitics zinataka kuchezwa ili Mmarekani apate uungwaji. mkono in exchange ya sisi kumpa ushirikiano katika mgogoro wa Israel Palestina

Netanyahu anakuja kuwapa viongozi wetu wa ukanda huu saundi ili wasitende haki kwenye hii ishu maana baada ya Kiongozi wa Palestina kuikataa plan ya Trump, anataka iende UN ili kupata resolution kwenye UN general assembly ya uungwaji mkono. Sasa Netanyahu anakuja kutushawishi tuwatose wapalestina

USHAURI WANGU KWA SERIKALI
1. Mpango wa Trump, Kushner na Netanyahu juu ya kutwaa ardhi ya wapalestina kupitia ile wao wanaita deal of the century ni mpango ww dhulma, tusibariki dhulma hii.

2. Tuendelee na msimamo unaoungwa mkono na Nchi nyingi duniani kuwa resolutions mbalimbali za UN ikiwemo security council juu ya mgogoro wa Oalestina na Israel ziheshimiwe

3. Tusikubali kuuza haki, kuunga mkono waonevu kwa sababu ya vipesapesa, misaada ya hapa na pale, sisi tuendelee kuunga mkono msimsmo wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mzalendo wa Afrika ya Kusini Baba Nelson Mandela waliosimama bila kuyumba kutetea wapalestina

4. Tusimame na nchi zote penda haki. kama vile Vatican na nyingine zinazotaka wapalestina wapewe haki yao.

Huu mgogoro siyo wa kidini, maana huko Palestina kuna wapalestina Wakiristo na Waislamu na wote wanakula msoto mkali chini ya Waisrael

Naomba tu serikali yetu isiyumbishwe na Netanyahu, bali isimamie misinginya haki
 
Tunawahitaji wayahudi Zaidi kuliko wapalestina.

Kwa hiyo unauza utu wako kwa visenti vidogo unavyopewa?
Ndugu zako Falasha walikaribishwa Israel kutoka Ethiopia wakiwaita ni ndugu zao lakini mwisho walinyimwa haki zote na mpaka wanawake wakafungwa vizazi kabisa je hilo nalo unaona sawa?
Kweli kila mtu ana maoni yake dunia hii


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Magu lazima awatose Wapalestina. Hilo linajulikana mbona. Wayahudi ndiyo wamempa mitambo ya kudukua na waziri wao wa Ulinzi ndiye alikuja kukamilisha deal
 
Kwa mfano Tanzania ikikataa kuunga mkono hayo "mawazo yako" kama ni ya kweli, Israel na marekani waathirika vipi? Ebu acha uongo wako hapa, unakuja kirejareja kumsafisha makonda?
 
Kila nchi INA angalia national interests, utu pekee haimo kwenye "strategic interests" yaani tukatae kushirikiana na Israel kijeshi, kiuchumi sababu ya utu? Umesoma wapi wewe IR?

Tuna kitu gani zaidi ya kuomba
Kuna mataifa mangapi duniani ambayo unaweza kushirikiana nao kwa misingi bora?



Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Mkuu mbona tayari tuwaunga mkono Israel..leo hii wana ubalozi wao apa na sisi tunao pale makao makuu ya Israel - Jerusalem!!
Mwl.Nyerere alikataa ilo lakini mzalendo kasema lazma tuwakubali wana wa Israel na kuwatosa ndugu zetu wa Palestinia
 
Tuna kitu gani zaidi ya kuomba
Kuna mataifa mangapi duniani ambayo unaweza kushirikiana nao kwa misingi bora?



Sent from my iPhone using Tapatalk
Marekani na Israel ndio wanao influence global politics, ndio maana hata mataifa ya ulaya linapokuja suala LA Israeli wana kuwa makini sana, Sababu Baba ya dunia, Marekani ndio analilinda hilo taifa!
 
Vipi kuhusu wenye wazo au nia ya kuwafuta, au kuwaondoa wapalestina kule palestine unawaombea dua ya namna gani?
... hakuna mwenye wazo wala nia ya kuifuta Palestina. Wameombwa mara kadhaa waishi kwa amani na Israel bahati mbayo ndio hivyo tena - kibri! Hawataki!
 
Wale wana ulterior motives, kuna kitu wanataka kutoka kwetu ili tuwape au tuwafanyie.

Makonda japo ana mambo ya hovyo lakini safari hii ametumiwa na mabeberu kama mbuzi wa kafara!
Ukiona marekani na Israel wanamsifia kiongozi wenu, ujue hamuna kiongozi hapo

Tuungane kuwapinga kwa lolote wanalotaka kuifanyia nchi yetu, tusibague matukio.
 
Kwani kuna madhara gani endapo tukimuunga trump mkono
 
Tanzania ilianza kuwatosa Wapalestina kabla Magufuli hajawa rais.

Sent using Jamii Forums mobile app

Haijawahi kuwatosa Wapalestina ila tu ilianza kuanzisha uhusiano na Israel(Kushirikiana na Israel katika baadhi ya mambo haikumaanisha kuwa against wapalestina, maana voting records zetu kwenye UN ziliendelea kuwa vilevile) Ila alipoingia JPM kuna shift ya voting style ilitokea in favor ya Israel tofauti na zamani kuanzia kwa JKN hadi JK
 
Marekani na Israel ndio wanao influence global politics, ndio maana hata mataifa ya ulaya linapokuja suala LA Israeli wana kuwa makini sana, Sababu Baba ya dunia, Marekani ndio analilinda hilo taifa!

Kweli kabisa Hilo halina ubishi
Lakini bado ni taifa dhalimu pia


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Back
Top Bottom