Je, Serikali ya Magufuli kuwatosa Wapalestina? Netanyahu anakuja Afrika ya Mashariki

Israel ni Taifa teule la Mungu kwenye Biblia tumeambiwa ukiwabariki utabarikiwa ukiwalaani utalaaniwa? Kwenye hili namuunga Mkono raisi wetu. Tumefaidika nini na wapalestina hadi Leo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mauwaji yanayoendelea nchini ndiyo yanatukabili. Wabunge wanashitakiwa wanakaa magerezani wanapigwa risasi hadharani. Hakuna anayeshikiliwa kwa kutaka kumuua mbunge. Leo limetolewa tamko la kumuua Zitto, mpaka mchungaji wenu akawaombea ili mfanikiwe kwa azimio lenu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tushasaidia sana yan
Alaf hakuna lolote tuliolipata.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Diplomasia yetu ya uchumi inaruhusu
 
Duniani mataifa yanaangalia maslahi, hayo mengine ni siasa tu. Kipindi kile Nyerere alikuwa hana namna kwani issue ya mafuta ilikuwa ikimtesa sana.

Lkn leo baada ya kuwa dhahiri kuwa miongo kadhaa ijayo mafuta hayatakuwa dili tena ushawishi wa mataifa ya kiarabu unaanza kupungua. Ndo maana yake.
 
Mkuu mbona tayari tuwaunga mkono Israel..leo hii wana ubalozi wao apa na sisi tunao pale makao makuu ya Israel - Jerusalem!!
Mwl.Nyerere alikataa ilo lakini mzalendo kasema lazma tuwakubali wana wa Israel na kuwatosa ndugu zetu wa Palestinia


Mimi katika hili naingia mkono msimamo wa Serekali.

Waarabu wanatutumia sana waafrika katika kuunga mkono harakati zao lakini linapokuja suala la kusaidia Afrika juu humu hakuna kitu.Nchi nyingi za kiarabu ni wazalishaji wa mafuta hawana package za kusaidia Afrika hasa nchi maskini sana sana labda kujenga kusikitika kama Col Gaddaf
 
Unajua maana ya values kama vile:

Compassion, justice, honesty, care for the weak, na respect to humanity dignity?

Bandiko lako namba moja ni zuri, ila ni kama wali mzuri ulioamua kuutia mawe, hapo ulipoanza kusema hata Makonda kachukuliwa hatua na Marekani kwa ajili ya hayo matarajio yao! Ni vyema ukalinda uzuri wa bamdiko lako bila kuchanganya na upotoshaji.
 
Matatizo yako ni jinsi ulivyo anza hii mada yako itapata support ndogo. Ungeongelea Palestine peke yake tungekuelewa.
 
Falasha waliukana uafrika, ni ndugu zao wayahudi!
 
Hawajatoswa, sisi hatufungamani na siasa za upande wowote, waje Wayahudi poa waje Wapelistina wanakaribishwa, wote binadamu kama sisi na hakuna ujinga wa kudai taifa teule!
 
Tatizo watu wengi hufikiri kuwa kwa kuwa karibu na wahuni hawa wa Kiisraeli ndiyo watapata baraka zile alizoahidiwa Abraham baba wa imani. Hilo chaka wanaloingizwa hawataweza kuamini macho yao kuwa, Netanyahu maarufu kama "Bibi" ni mpiga "deal" na kibaraka mkubwa wa Marekani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Netanyahu anataka kutununua ili tuuze ile sense yetu ya haki, na msimamo wenye heshima ya utu ili tuwatose wapalestina.
Relax brother!
Hizi ni zama za diplomasia ya uchumi,hatuwezi kuwatosa wapalestina,lakini hatuwezi kuacha fursa za kiuchumi na kisayansi toka kwa mayahudi
Anachofanya Magufuli ni kuimarisha tu uhusiano
Jkt iliundwa na nyerere kwa kufuata mfumo wa Israel
Israeli wana program ya kufunza makomandoo na mashushushu mpaka leo
Acha sasa watupe teknolojia ya kulima kisasa kwenye eneo dogo sana tena milimani
 
Kitabu kinasema atakaye ilaani Israel Naye atalaaniwa atakaye ibariki naye atabarikiwa. Unajua Maana yake?
 

Diplomasia ya uchumi haimaanishi tuunge mkono Ujambazi na Unyang'anyi.
 
Hao wapalestina wanatusaidia nini zaidi ya kuleta ugaidi na kujitoa mhanga.?!
 
[QUOTE="Missile of the Nation, post: 34327884, member: 490108nchi ya Diplomasia ya uchumi haimaanishi tuunge mkono Ujambazi na Unyang'anyi.
[/QUOTE]

Tanzania haijabadili msimamo wake wa kuungaa mkono sahara magharibi na palestina kujitawala
Siku zote tunaamini katika kupata ufumbuzi utakayoipa palestina taifa lake
Kuitambua morocco au Israel hakumaanishi kwamba tumeitosa sahara magharibi au palestina
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…