Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 37,630
- 47,434
Siku ya tarehe 23 Aprili, 2022 Rais Samia alishiriki utiaji saini wa makubaliano ya kibiashara baina ya kampuni ya Taifa Group na kampuni ya Northern feed co.
Mkataba huo wenye thamani ya Dola milioni 500 sawa na trilioni moja za kitanzania utakua katika uzalishaji wa soya, ngano , sukari etc.
Anayeonekana kusaini makubaliano hayo ni Bwn. Rostam Aziz ambaye ndiye mmiliki wa Kampuni hiyo.
Bwn. Rostam Aziz ambaye ndiye mmiliki wa kampuni ya Taifa Gas alikuwepo pia katika delegation ya Rais iliyokwenda Kenya na kuingia makubaliano ya kuisambazia Kenya Gesi.
Kwakua Bwn. Aziz sio sehemu ya Serikali utiliwaji saini wa makubaliano hayo ni jambo binafsi zaidi kuliko la kisiasa.
Uwepo wa Rais ambaye ni nembo ya mamlaka ya Nchi katika jambo binafsi unaleta ukakasi kidogo kwani sisi wananchi hatuna taarifa zozote za umiliki wowote wa Serikali iwe kwa hisa au kwa namna yoyote katika kampuni hiyo.
Hivyo basi kama Tanzania ina shares katika kampuni ya Taifa Group ni vyema tukaambiwa ama la tueleweshwe kuhusiana na uwepo wa kampuni hii katika ziara za Rais na ulazima wa Taifa kuhusishwa katika mambo binafsi ya kampuni hii.
www.jamiiforums.com

Kenya: Rais Samia afungua kongamano la wafanyabiashara nchini Kenya, Rostam Aziz atema madini ukumbi mzima wamshangilia
Rais Samia amefungua kongamanano la wafanyabiashara nchini Kenya ambalo limehusisha pia wafanyabiashara kutoka Tanzania. Rostam Aziz ametaka uwepo wa uwiano mzuri wa kibiashara kati ya Kenya na Tanzania badala ya nchi moja kuwa msambazaji wa mali ghafi na mwingine akiwa muuzaji wa finished...