Je, Serikali ya Tanzania ni Mbia wa Kampuni ya Taifa Group?

Je, Serikali ya Tanzania ni Mbia wa Kampuni ya Taifa Group?

Watanzania tutambue kuwa sekta binafsi ndiyo mwajiri mkuu wa waTanzania kwa kutoa ajira nyingi kuliko serikali kuu na serikali za mikoa / halmashauri za wilaaya.

Sekta binafsi ndiyo mlipaji mkuu wa kodi na anachangia pakubwa ktk mfuko wa kodi .

Hivyo serikali yoyote makini ni lazima ifanye kazi na sekta binafsi ili kuleta mabadiliko makubwa chanya ya kiuchumi

https://www.tanzaniaweb.com › JPM...
JPM apania kutengeneza mabilionea watanzania

29 Sept 2020 — “Tunataka uchumi wa Watanzania, tunataka mabilionea Watanzania,” alieleza jana Rais Magufuli, alipohutubia mkutano wake wa mkubwa
 
Hayo makubaliano ni internal affairs za kampuni husika Rais wa nchi hana nafasi katika internal afairs za private company.
Lakini nadhani inafaa pia utambue kwamba, sasa hivi, hawa ndio wanaoendesha serikali

Maamuzi hayawezi kufanyika huko serikalini bila ya hawa kuhusishwa. Hali ndiyo hiyo.

Wakati wa uchaguzi utakapofika, hawa ndio watakaoamua nani atakuwa mshindi. Watatumia kila raslimali iliyopo kuhakikisha kuwa hilo linatokea.

Katiba mpya, hawa hawataruhusu kwa njia yoyote iwepo kabla hawajaimarika zaidi kutokana na ufadhiri wa serikali inayowajenga.

Sasa basi, watu, na hasa wananchi ni lazima walitambue hili kungali mapema. Na bahati mbaya iliyopo, ni kwamba upinzani unaotegemewa kuwaongaza wananchi kuyakataa haya, nao unaegemea upande huo huo. Samia atakuwa amewawahi; sasa sijui watakimbilia wapi?
 
Mkuu, kupoteza huko kwa hisa, haina maana kwamba ziliingia serikalini. Check your facts.
Hajapoteza hisa yoyote bado ni kampuni yake kilichofanyika ni mabadiliko ya jina tu toka Mihan Gas kwenda Taifa Gas.

Hapa swali langu linagusia pia Taifa Group.

Je serikali anahisa huko mpaka Rais wetu atuwakilishe kwenye utiwaji saini wa makubaliano yake na kampuni nyingine??
 
Mkuu, kupoteza huko kwa hisa, haina maana kwamba ziliingia serikalini. Check your facts.
Hisa zilichukuliwa na serikali sikumbuki tu ile doc niliweka wapi kuna list za kampuni zote ambazo serikali ina hisa taifa gas ni moja wapo
 
Kuanzia mwishoni mwaka jana imekuwa ni kipindi kizuri sana kwa Rostam;
1) Williamson Diamond mine(Mwadui) - $15M
2)Tigo na Zantel (Partnership na Axian) - $100M
3) Mkataba na Northern Feed Company - $500M
4) Tancoal Energy ?
 
In principle serikali inahangaikia 1. CAPITAL INFLOW, 2. EMPLOYMENT TO BE CREATED, 3. TECHNOLOGY TRANSFER, 4. TAX REVENUE FROM CORPORATE AND EMPLOYEES TO BE EMPLOYED Nk
 
Hajapoteza hisa yoyote bado ni kampuni yake kilichofanyika ni mabadiliko ya jina tu toka Mihan Gas kwenda Taifa Gas.

Hapa swali langu linagusia pia Taifa Group.

Je serikali anahisa huko mpaka Rais wetu atuwakilishe kwenye utiwaji saini wa makubaliano yake na kampuni nyingine??
Sina uhakika kama kuna great thinker wa kukujibu maswali unayojaribu kuyadodosa, labda wapo na hawako interested na mjadala.

Pili, sidhani kama unaotuuliza haya maswali "wengi wetu" tunaelewa nini hasa lengo la haya maswali yako. Hivyo sitarajii majibu ambayo ni facts unless waje wanaoelewa na wapate hamu ya kulijadili hili. Binafsi sielewi chochote hivyo siwezi kujibu chochote.

Btw, umebadilika sana mkuu!
 
target za 2025 hizo hangaya anajisogeza kwa kingmaker kinara aliepewa kazi ya kuhakikisha nani anakuwa rais tanzania katika kila uchaguzi. msiwabeze wanaosema nchi ishauzwa hii.
 
Sina uhakika kama kuna great thinker wa kukujibu maswali unayojaribu kuyadodosa, labda wapo na hawako interested na mjadala.

Pili, sidhani kama unaotuuliza haya maswali "wengi wetu" tunaelewa nini hasa lengo la haya maswali yako. Hivyo sitarajii majibu ambayo ni facts unless waje wanaoelewa na wapate hamu ya kulijadili hili. Binafsi sielewi chochote hivyo siwezi kujibu chochote.

Btw, umebadilika sana mkuu!
Nashukuru kwa kunielewa mkuu.

Wapo wachache wanaoelewa ila wanapotosha kwa makusudi.

Na wapo wasioelewa kuwa wanapotosha kwa kutokuelewa kwao.

Nafahamu hilo tunakwenda nao hivyo mdogo mdogo tu, ukweli utakuwa wazi sio mbali sana.
 
Lakini nadhani inafaa pia utambue kwamba, sasa hivi, hawa ndio wanaoendesha serikali

Maamuzi hayawezi kufanyika huko serikalini bila ya hawa kuhusishwa. Hali ndiyo hiyo.

Wakati wa uchaguzi utakapofika, hawa ndio watakaoamua nani atakuwa mshindi. Watatumia kila raslimali iliyopo kuhakikisha kuwa hilo linatokea.

Katiba mpya, hawa hawataruhusu kwa njia yoyote iwepo kabla hawajaimarika zaidi kutokana na ufadhiri wa serikali inayowajenga.

Sasa basi, watu, na hasa wananchi ni lazima walitambue hili kungali mapema. Na bahati mbaya iliyopo, ni kwamba upinzani unaotegemewa kuwaongaza wananchi kuyakataa haya, nao unaegemea upande huo huo. Samia atakuwa amewawahi; sasa sijui watakimbilia wapi?
Umeandika mambo ya msingi sana mkuu.

Asante.
 
Taifa Group ilikuwa ni ya RA na mwendazake kama ilivyo Vodacom (Lupaso, Chatoguy na Jaji fulani), Bagamoyo Sugar (Chatoguy na SSB).
Swali ni nani atachukua hisa za mwendazake kwenye miradi ya ubia?
Nilikuwa nahisi hiki kitu pia hapo kwenye Taifa Gas, mwendazake na RA ule ukaribu wao ulikuwa unanipa maswali mengi saana.
 
Rostam Aziz anaonekana hapo kwa sababu alikuwa mmoja wa wajumbe wa kibiashara wa Tanzania katika ziara hiyo huko Marekani
 
Rais ni wa wote. Nimekupa mifano ya watu ambao kazi zao zinaishia ndani ya serikali tu au shughuli za umma tu ambao ni hao kama Katibu Mkuu Kiongozi.
Lakini Rais, Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, kazi zao haziishii kwenye shughuli za umma tu. Zinaenda beyond.
Kuna zile kazi kuu 3 za Rais:
1. Mkuu wa nchi
2. Mkuu wa Serikali
3. Amiri Jeshi Mkuu.
Sasa hapo alikuwa akitekeleza kazi namba 1.
Kwa kukazia tu, hata nami nikiwa na jambo langu naweza kumwalika rais akaja kufungua/kuwa mgeni rasmi.
 
Siku ya tarehe 23 Aprili, 2022 Rais samia alishiriki utiaji saini wa makubaliano ya kibiashara baina ya kampuni ya Taifa Group na kampuni ya Northern feed co.

Mkataba huo wenye thamani ya Dola milioni 500 sawa na trilioni moja za kitanzania utakua katika uzalishaji wa soya, ngano , sukari etc.

Anayeonekana kusaini makubaliano hayo ni Bwn. Rostam Aziz ambaye ndiye mmiliki wa Kampuni hiyo.

Bwn. Rostam Aziz ambaye ndiye mmiliki wa kampuni ya Taifa Gas alikuwepo pia katika delegation ya Rais iliyokwenda Kenya na kuingia makubaliano ya kuisambazia Kenya Gesi.

Kwakua Bwn. Aziz sio sehemu ya Serikali utiliwaji saini wa makubaliano hayo ni jambo binafsi zaidi kuliko la kisiasa.

Uwepo wa Rais ambaye ni nembo ya mamlaka ya Nchi katika jambo binafsi unaleta ukakasi kidogo kwani sisi wananchi hatuna taarifa zozote za umiliki wowote wa serikali iwe kwa hisa au kwa namna yeyote katika kampuni hiyo.

Hivyo basi kama Tanzania ina shares katika kampuni ya Taifa Group ni vyema tukaambiwa ama la tueleweshwe kuhusiana na uwepo wa kampuni hii katika ziara za Rais na ulazima wa Taifa kuhusishwa katika mambo binafsi ya kampuni hii.

View attachment 2199343

Kuna kitu
 
Back
Top Bottom