Je, Shekilango na Urafiki ndio Stendi mpya za Mabasi yaendayo mikoani?

Kinachokukera ni nini?

Abiria atoke mjini hadi mbezi umbali wote huo na ictoshe nauli ya boda/uber alipie, huoni kuwa kuna shida hapo!!! Abiria anatokea kanda ya ziwa anawasili ucku unategemea aanze kutafuta usafiri wakumpeleka mjini huoni iyo ni risk sana, kuna kuibiwa au kuuwawa kabisa.


Acha wivu kijana, kama huna ofisi pale kuwa mpole tu.
 
Tunarudi tulipotoka.pole pole in voice
 
Wabongo tunapenda sana kuoneana huruma hili ni suala jema ila kwa upande mwingne ni upumbavu mkubwa
Stand imejengwa kwa mapesa meng tena ukute niya mkopo arafu wanatokea wajinga wachache wenye mabasi wanakataa kufuata utarabibu mtu akiongea km mtoa mada hapa anaonekana mnafiki ametumwa
Sawa stand iko mbal na Jiji sawa atukatai ila sasa vyanzo vya uchumi vimeongezeka sabu
**** mtu wa boda atapata
Taxi atapata. Na ata bajaji na daladala wote watapata pesa kwa kusogeza abiria stand mpya
 
Ukweli ni kuwa mtoa mada hajui alisemalo.
Basi zote lazima ziingie stendi ya Magufuli. Haijalishi imetoka Shekilango, kariakoo au magomeni.

Mapato ya serikali yapo pale pale.
 
Hizo hesabu zako sisi hatuna! Kawafundishe wengine.
 
Kakaeni huko dunia kwa kweli, mtuachie nchi yetu.
 
Sijui Kama wanawazaga Kuna watu inabidi watoke Kiganboni, Mbagala Chanika kufuata standi ya Mbezi Kama unasafiri na familia ukichukua taxi ni nauli mbili za kwenda mikoani
 
Hesabu za kiamani na za uonevu, mimi natoka Kigoma na Advanture na familia ya watu 8 eti tuchukue Bajaj hiyo hela imebaki kweli
Ngoja Treni ya SGR ianze kama tutashuka Magufuli, ukitoka Kigoma unashuka Morogoro unapanda Express mpaka Bandarini huko mabasi kibao
Au Mabasi yatembee usiku tu asubuhi unahamia mwendo kasi
 
Tatizo lipo wapi?kule mbezi pia gari zipo tena nyingi tu..
Mbezi terminal ipo mwisho wa jiji...kuanzia kutoa huduma shekilango na urafiki ni msaada mkubwa kwa wengi ..ukizingatia saa 12.00 asubuhi gari inaanza safari.
 
Hesabu za kizamani na za uonevu, mimi natoka Kigoma na Advanture na familia ya watu 8 eti tuchukue Bajaj hiyo hela imebaki kweli, angalieni na wenzanu kuna siku za matatizo kwa hiyo tusisafiri sio?
Ngoja Treni ya SGR ianze kama tutashuka Magufuli, ukitoka Kigoma unashuka Morogoro unapanda Express mpaka Bandarini huko mabasi kibao
Au Mabasi yatembee usiku tu asubuhi unahamia mwendo kasi
 
mkuu basi za lindi na mtwara zinaanzia sudan temeke zinamalizia mbagala ni route ya miaka mingi
 
Kwa Jjiji kubwa kama Dar linatakiwa tuwe na vituo vya mabasi ya mikoani zaidi ya kimoja. Jiji la Dar linayakiwa kuwa na 'terminal' kwenye kila Manispaa ili kupunguza gharama kwa wasafiri. Hebu fikiria mtu anayeishi Chanika na anasafiri kwenda Mwanza, inampasa kuondoka Chanika saa ngapi ili awahi Mbezi saa 11.30 asubuhi?

Vv
 
Atoke Kigamboni au Vikindu aende kukata ticket Mbezi huu ni usumbufu tu. Kampuni kuwa na ofisi muhimu sana popote pale kuharahisisha huduma kama ambavyo wamerahisishiwa watu wa Kimara na Mbezi kwa stend ya Magufuli.
Muwe mnasoma hoja vizuri, jamaa hazungumziii kukata tiketi, hoja ya msingi hapa na baadhi ya mabasi kutopitia kabisa Mbezi Bus Terminal, zinapandisha abiria hapo Urafiki na kupita juu kwa juu.
 

Mbona hakuna airport kila wilaya hapa Dar es salaam na bado watu wanawahi usafiri wa ndege!!?? Lame excuse

Unataka kusema mtu wa bunju au bagamoyo akiambiwa ndege inaondoka saa 11 alfajiri bado atechelewa kufika airport?
 
Mbona hakuna airport kila wilaya hapa Dar es salaam na bado watu wanawahi usafiri wa ndege!!?? Lame excuse

Unataka kusema mtu wa bunju au bagamoyo akiambiwa ndege inaondoka saa 11 alfajiri bado atechelewa kufika airport?
1. Wengi wanaoenda kupanda ndege wana usafiri binafsi/uwezo wa kukodi aina yoyote ya usafiri kuwafikisha airport kwa wakti. Usifananishe abiria wa ndege na wa bus.

2. Serikali yetu imekosa maono (long term plan) kwenye hili swala la stendi, sio kwa dar peke yake bali kwa mikoa mingi. Swala la kwamba kila mji unapopanuka stendi kuu inasogezwa nje ya mji (ref. Dsm, Mwanza, Dodoma, Moro nk) ni ukosefu wa mipango mizuri. Ina maana hata hiyo Magufuli siku mji ukikua nayo itakuja kusogezwa mwisho itafika Chalinze kabisa. Wanasahau kwamba kila unaposogeza stendi mbali na wananchi, unawaongezea gharama kubwa na usumbufu, ambayo ni kinyume kabisa na lengo la kua na serikali.

Terminal inatakiwa iwe KATIKATI ya mji, sehemu ambayo inafikika kirahisi na watu kutoka pande zote. Period. Huwezi kua unahamisha hamisha terminal kila baada ya miaka michache huo ni ukosefu wa mipango. Hoja ya kwamba katikati ya mji hakuna nafasi ni hoja mfu, nafasi ipo kubwa sana chini ya ardhi unaweza kuweka terminal ya ukubwa wowote unaopenda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…