Ahlan wa sahlan
Naiomba serikali ifunge hizi ofisi uchwara zilizopo hapa maeneo ya shekilango na Urafiki. Mabasi ya mikoani yamekuwa hayaendi tena kupaki stendi ya Magufuli pale Mbezi badala yake yamekuwa yakijazana maeneo ya Shekilango na Urafiki nyakati za Alfajiri na Mchana. Najiuliza ile stendi ya mabilioni pale Mbezi imejengwa kwa ajili ya kina nani?
Wahusika mpo na mnalifumbia mamcho jambo hili.Stendi imekuwa ikikosa mapato ya getini kwa abiria wanaoingia ndani ya stendi kutokana na watu sasa kumiminika kwenda maeneo ya Urafiki na Shekilango.
Wito wangu kwa serikali ni kuhakikisha mnazifunga mara moja ofisi hizi uchwara za haya mabasi hapa Shekilango na urafiki kwani hawa jamaa wameshageuza eneo hili kuwa ni terminal
Mfanyabiashara yeyote, huwa anawaza kusogeza huduma kwa wateja wake, hata serikali ina mlengo huo huo wa kusogeza huduma kwa wananchi, vinginevyo TRA,Mahakama, hospitali, Kituo cha Polisi, mabenki n.k vyote hivyo vingekua ni sehem moja tu mkoa mzima, tungeona kungekua na mabalaa ya kutosha hizo huduma ambavyo zingekua. Imagine wote hao wange waza kama ulivyo waza wewe
Bado principles za demand and supply zina apply hapo... wateja wangi wapo nje ya mbezi (wapo scatterd) na kuna makampuni zaidi ya Buku yote yanafanya kazi hiyo hiyo kwa ushindani wa hali ya juu mpaka yameamua kujiongeza kuwafuata wateja walipo, tuwashukuru sana, vinginevyo biashara hizo zitakufa. Watu wakianza kupanda private cars zinazo anzia jiran na wanako kaa kutakua na biashara ya mabasi? Tuwaze kwa akili...Kila mtu anaangalia wepesi wa upande wake, abiria na mwenye basi.
Ni roho mbaya na akili ya kipumbavu tuu, kutaka kila kitu kianzie mbezi na kiishie mbezi. Watu wamejaa kigamboni, Mbagala Chamazi Mvuti, Mbweni Bunju B, Mwananyamala Msasani, na kwingineko...wote hao unataka waamke saa 8 usiku kukimbizana na maboda boda kwenda mbezi kusumbuliwa na wapigadebe??
Viongozi wetu walitaliwa wawaze kwa akili kubwa sana, mji kama dar unao kua kila siku unatakiwa kuwa na stand zaidi ya moja na stendi zote ziwe huru kwa mabasi yote kuchagua kwenda kupakia na kushusha abiria depending na route zao, na hiyo italeta chachu hata ya ukuaji wa makampuni ya mabasi ambapo nayo kwa nature ya mazingira na katika kuongeza kipato yatalazimika kuwa na mabasi mengi ili yawepo kila ilipo stand kwa kurahisisha huduma kwa wateja, na itapunguza kero, kama mabasi ya kwenda sehem yoyote yanapatikana jirani na alipo mteja.
Mtu wa mbagala anaenda mbeya asipate tabu wakijengewa stand kubwa saana pale mwembe yanga kuna tatizo gani??? ule uwanja pale umekaa tu wahuni wanavutia bangi na kucheza mpira, Serikali iweke stand pale itawasaidia wananchi wa maeneo yote kuanzia temeke, kigamboni mpaka chanika. Uwanja wa mpira watafute sehem nyingine uwanja wa mpira ni mita 100 tuu mpaka 200.
Nimeizungumzia sana mbagala, kigambon mpaka chanika kwasababu ndo wahanga wengi wapo, maskini na huko ni mbali sana na ilipo stand ya Magufuli..
Hiyo stand ya mbez haina msaada wala nini acha watu wajitafutie wepesi wao wa maisha. inakera sana umetoka safari ndefu mfano Mwanza, Mbeya unaingia mbezi saa tatu usiku hadi saa saba usiku halafu unako enda ni Chamazi, Mbagala na mabasi yaishie mbezi.