Wanabodi,
Aina Tatu za Wanasiasa
Kuna Aina Tatu za wanasiasa haha hama, Wahamaji Vyama, 1.The Genuine, 2. The Frustrated Gold Diggers, na 3. The Survivals wenye Njaa Wanaotaka Kushibishwa!.
1. Wahamaji Genuine
Hawa ni wanasiasa wa ukweli, wameingia kwenye siasa for very genuine reasons, na wanafanya genuine politics, wanaongozwa na principles, na falsafa, hivyo hujiunga na chama sio kufuata watu bali kufuata falsafa na itikadi, ikifikia mahali chama kimebadili malengo au itikadi, watatoa ushauri wa nini cha kufanya, wasiposikilizwa, wanaweza ama kujaribu kufanya mapinduzi ya ndani kama kina Zitto, Prof.Kitila na Mwigamba, ama wanaamua kujitoa rasmi kama Dr. Slaa, na hawa genuine wakiisha hama, siku wanahama, ama wanaaga rasmi kwa kuandika barua kama Lawrence Masha na kusema sababu, ama kwa kuitisha press conference na kutapika nyongo Kama siku ile ya Dr. Slaa pale Serena. Na baada ya pale, kamwe hutakaa uwasikie wakitukana chochote kuhusu kule walikotoka. Uliisha wahi msikia Masha au Dr. Slaa akikashifu Chadema?.
2. The Frustrated Gold Diggers.
Hawa ni wanasiasa wazuri tuu wenye uwezo wa uongozi, ila wameingia kwenye siasa za tamaa, sio kwa ajili ya kuongoza na kuwatumikia wananchi, bali wameingia kwenye siasa kusaka fursa, ikitokea wakakataliwa kuteuliwa na kukatwa, hawa huhama chama kwa hasira za kukosa uteuzi, hivyo hujiunga na chama chochote kitakachowapatia fursa za uteuzi, lakini mapenzi yao bado yako kwenye vyama vyao vya asili, na hawa kamwe hutakaa uwasikie wakitukana vyama vyao. Kundi hili ni kundi la Dr. Slaa alipohama CCM kujiunga Chadema. Waliokatwa CCM wote walihamia Chadema, akiwemo Lowassa na genge lake. Hutakaa uwasikie wakitukana au kukashifu kule walikotoka, kwasababu wanajua siasa hazitabiriki, kuna leo na kesho.
3. The Survivals wenye Njaa Wanaotaka Kushibishwa!.
Hawa ni wanasiasa wanaoingia kwenye siasa ili tuu kusaka fursa, kwao siasa ndio ajira yao, tatizo lao ni njaa, hivyo wako tayari kufanya lolote ali mradi mkono uende kinywani. Hawa wanaitumikia siasa kwa kutumia the law of the jungle ambapo ni "struggle for existence, survival is for the fittest". Hivyo wanasiasa wa aina hii, lengo lao ni survival tuu, ili kusavive, moja ya sifa zao kuu ni kujikomba komba sana, na siku wakihama, hutukana sana kule walikotoka. Hawa ni kama mwanamke mala.. anayejiuza, hawezi kumkataa mteja yoyote alimradi amefika bei!.
Wengi wa hawa wabunge na madiwani wanaojitoa Chadema na kuhamia CCM, ni kundi la hawa wanasiasa njaa, wanaofanya biashara ya umala...wa kisiasa. kinachowakimbiza Chadema sio siasa bali ni njaa tuu za uoga wa 2020, hivyo ni kama wanawake mala.. wanaojiuza miili, kuna baadhi wametongozwa au kujitongozesha kwa tamaa tuu ya dau dogo la kushawishiwa ikiwemo kuhongwa ahadi za wao kusimamishwa tena kuwa wagombea wa CCM katika uchaguzi wa marudio, au chaguzi zijazo. Wanasiasa wa aina hii mimi niliwaita ni wanasiasa mala.. wa kisiasa, ni wanasiasa wa hovyo, sababu zilizowafanya wahame, mimi nimeziita ni siasa za kijinga.
Kinondoni na Siha, tusikubali ujinga huu! hata Mwl. Nyerere alikataa ujinga wa CCM, 1995 akachagua upinzani! - JamiiForums
Kuhusu wahamaji wa aina hii, niliwahi kuyazungumza haya
Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law!, Kuendelea Kuitumia ni Ujinga?, Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!.
Jee Kwa Vile Wanasiasa Hama Hama Hawa, Wanavibeza Vyama Vyao Walikotoka, Jee Vyama Navyo Viwabeze?.
Jibu ni hapana, niliwahi kuutoa ushauri huu kuhusu hawa viongozi hama hama na nilishauri hivi
CHADEMA mjitafakari msiwabeze wahamaji, wana hoja za msingi. Adui wenu mkuu sio CCM! Lazima mbadilik
Paskali.