Marekani na kwinginepo unaweza kukuta mtu anatokea labda lecturer katika chuo anateuliwa au anachaguliwa kushika wadhifa kwenye serikali au bunge.Akimaliza muda wake mara nyingine anarudia kazi yake ya awali.
Lakini Dr.Nyerere licha ya kutaka aitwe Mwalimu sikumsikia kurudi kazi ya ualimu he thought ualimu ni under dog.
Si kweli kwamba kulikuwa na uhaba wa wananchi kufanya kazi yake ndio maanake alijilimbikiza miaka 27 ya uraisi hadi alipofarakana na IMF akalazimika kujingatua kinamna.
Mfano mzuri wa kuigwa barani Afrika ni wa mfungwa Nelson Mandela alisota jela miaka 27 akipasua mawe Robbins Island lakini alivyoachiwa huru alitawala South Africa kipindi kimmoja cha miaka minne tu licha ya wananchi wake na dunia kutaka aendelee.
Kugangania madaraka kwa kisingizio cha yeye ndio mwenye vision tu ya kuongoza nchi ni ulafi na uwoga wa kuachia madaraka. Unaanza kuwa Raisi at 32 years unaendelea nao for official 27 years na mingine over 10 years kama Baba wa taifa.ni ufalme au usultan kwa njia nyingine.