Mkuu kwa walio wengi siasa ni ajira,na siasa ni biashara kubwa.
Ebu chukulia Mwalimu Nyerere akiwa mwalimu pale Pugu secondary.
Wakaja matajiri Rupia,Sykes na wengine kuwa wanampa kazi ya kuandika barua kwa kizungu ya kudai uhuru wa Tanganyika, aipeleke Umoja wa Mataifa New York Marekani.
Baada ya kazi nzuri, alikilimiwa na matajiri hao mavazi,gari,nyumba,bima,nk hakurudi Pugu kufundisha, akaja down town Dar kula kuku. Hadi kifo chake alijikita kwenye siasa kama mtaji.
Ndio maanake vyeo au teuzi za siasa huthaminiwa kuliko kazi halisi za umma.Ni nadra kusikia mwananchi anaenda mahakamani kushtaki kutopandishwa cheo cha walimu lakini katika siasa kila jambo linawezekana.