Je, siasa ni biashara kwa baadhi ya wapinzani?

britanicca

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Posts
16,295
Reaction score
33,994
Huwezi ukawa serious unataka mabadiliko Utapokea Rushwa toka chama tawala.

Huwezi kuwa serious unahubiri mabadiliko ukapokea maelekezo toka chama tawala nani agombeee na Nani asigombee.

Huwezi kuwa serious kabisa unataka mabadiliko ukapokea maelekezo ni lini udai haki zako wakati ni haki inatakiwa kudaiwa muda wowote.

Narudia watanzania mabadiliko yatakuja Ila si kwa vyama vyenye damu ya chama tawala na itachukua almost 30 more years kupata mabadiliko ya kweli.

Britanicca.
 
Naunga mkono hoja, siasa ni biashara kubwa duniani kwa nchi masikini, hapa Tanzania siasa ndio the most lucrative business!

Kuna watu wanaingia kwenye siasa kwa ajili ya kwenda kuwatumikia wananchi, na kuna watu wanaingia kwenye siasa ili kupiga ma dili tuu!, hawa ndio wanaofanya siasa biashara, its the most paying business!.


Hili la biashara ya siasa, nimelisema hapa Angalizo kwa Wanasiasa hamahama; Japo ni haki yenu lakini msisahau fadhila. Kuweni watu wa shukrani, mtabarikiwa sana, vinginevyo karma Itawahusu! niliwachambua makundi matatu ya wanasiasa.
 
Miaka 30 mbali. Natabiri vitu viwili vinaweza kutokea Nchini. Maandamano na vurugu yasiokuwa na uratibu wowote yatakayotoa CCM madarakani au Jeshi kuchukua Nchi kwa style ya Zimbabwe.
 
Inasikitisha sana
 
Inawezekana hata hapo ulipokadiria ni jirani sana kwasababu ili mabadiliko ya kweli yatokee nilazima ile generation ambayo ilikuwepo kabla na baada ya haya mambo ya democracy kuanza itoke yote kwenye system... ukiangalia sasa hivi watu wengi wanaotamani mabadiliko ya kweli ni hii generation mpya ambayo na yenyewe kwa kiasi kikubwa ikiingia kwenye system inapoteza nguvu.
 
Huwezi ukawa serious unataka mabadiliko Utapokea Rushwa toka chama tawala

Huwezi kuwa serious unahubiri mabadiliko ukapokea maelekezo toka chama tawala nani agombeee na Nani asigombee,

Huwezi kuwa serious kabisa unataka

Hivi Tanzania hii mtu anataka mabadiliko ili iweje?
WATU WANATAKA MABADILIKO KUELEKEA KWENYE HAKI (siyo haki sawa laaaaa...bali kuwa na haki kwa wote)
 
KAMBOWE NI KAHUNI TOKA KANA MIAKA 13y
 
Hivi Tanzania hii mtu anataka mabadiliko ili iweje?
We una miaka mingapi? Ungependa Tanzania iendelee kuwa jinsi ilivyo?
Rushwa Kila sekta
Ubadhilifu wa fedha za umma
Huduma za jamii chini ya kiwango
Elimu mbaya na mbovu!

Ningetandika ukurasa wa kutosha ila siku hizi mi ni mvivu wa kuandika
 
Hapo mwisho umemaliza kwa uchungu sana. Watu wanaona lengo lao ni mabadiliko la uchumi binafsi sasa kwa namna ilivyo njia ya mabadiliko ilivyo na miba basi ni bora kuiendea ya uchumi binafsi ambapo inawezekana kwa kujijenga kipinzani
 
Siasa ni biashara kubwa sana duniani. Mwanasiasa yeyote asikudanganye eti anakutumikia. Anatumikia tumbo lake na watoto wake. Mengine yote wanafanya ili kuhalalisha uwepo wao hapo walipo.
 
Hiyo unayoita “rushwa toka chama tawala” ni pesa ya umma toka Hazina ya taifa. Na chama tawala ni serikali kiuhalisia; ni chama dola (state party).

Hivyo, weka mada hii katika maudhui sahihi (right context). Hii ni biashara kati ya serikali na (?) kwa ajili ya (?).
 
Siasa ni biashara kama biashara zingine... Ndo maana dunia nzima wanasiasa wamegubikwa na skendo za ubadhirifu wanaoufanya katika kufanikisha biashara zao....
 
Kwani kwa chama Tawala ni nini ?

Hakuna mabadiliko yoyote hapa wala pengine kinachoweza kubadilisha hali hii ni kuwa na Taasisi imara za kuweza kuibua madudu sababu madudu yanatokea, yalitokea na yataendelea kutokea

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…