amani iwe kwenu,
Kwa wale wote mliowahi kuwa karibu na David Kafulila Kwa nyakati na sehemu tofauti tofauti nje na ndani ya siasa mtusaidie kujibu maswali haya,
1. Je, ni kweli kwamba huyu Kafulila anachukia rushwa kwa moyo na kwa nguvu zake zote kama tunavyoambiwa?
2. Je, ni kweli kwamba Kafulila hajawahi kupiga dili lolote la pesa tangu akiwa Mbunge, RAS, RC na sasa PPP-Center kama tunavyoambiwa?
3. Je, ni kweli kwamba Kafulila alikataa zaidi ya TZS 3bilioni za Escrow mwaka 2014 kama tunavyoambiwa?
4. Je, ni kweli kwamba Kafulila anachukia Ufisadi na Mafisadi toka ndani ya moyo wake kama tunavyoambiwa?
5. Je, ni kweli kwamba huyu jamaa hajawahi kuhusishwa na Kashfa za rushwa au ufisadi kipindi chote Cha utumishi wake Serikalini kama tunavyoambiwa?
6. Je, ni kweli kwamba Kafulila alirudisha chenji ya TZS 2bil kutoka katika TZS 6bil alizopewa kujenga Makao Makuu ya Mkoa wa Songwe kama tunavyoambiwa?
7. Je, ni kweli Kafulila alipoteza ndoa kwa sababu ya maisha duni anayoishi kama tunavyoambiwa?
Comment ziwe fupifupi