Je, siku ya kwanza kutongoza/kutongozwa ilikuwaje?

Je, siku ya kwanza kutongoza/kutongozwa ilikuwaje?

Karibuni Wana jukwaa tukumbushane tukio hili ambalo ni gumu kusahaulika kwenye maisha ya mtu.
Pia kuonyesha utofauti wa aina ya utongozaji wa zamani na sasa [emoji23][emoji23]
Dhumuni la uzi huu ni kufurahi pamoja na kuondoa mawazo yasiyo msingi. Karibuni Sana[emoji120]
Nilitumia kadi ya mpiga kura kumtia mrembo nyavuni.
 
Wanasema hata uwe kauzu vipi huwezi kujamba wakati unatongoza,, ila mimi nilijamba aiseh Nashukuru ilikua in silence mode halafu haikunuka kabisa [emoji23][emoji28][emoji1]

Tupo school hapo, kuna demu ana asili ya kiarabu jina lake Latifa. Huyu mtoto tulikutana kwenye mchezo wa volleyball. Yeye na wenzake walikua hawajui so wakawa wananyanyasika sana. Mzee mzima nikawa nawatetea lakini sababu kubwa ni huyu Latifa.
Katika kujali kwangu mtoto akatokea kunielewa. Lakini mzee mzima nilikua mgumu (hip hop) sana. Kitu pekee nilikua nawaza wakati huo ni kupiga chetezo kanisani na kuishabikia Man u ya Sir Alex.

Washkaji wananiambia dogo anakuelewa lakini me sina habari domo lote limejaa gundi. Kiukweli nilikua nampenda lakini nikitaka niende nafikiria hadhi yangu na uzuri wake + mabishoo wa shule wanaomtongoza basi naishia kukata tamaa, kifupi nilijidharau sababu she was so hot shule nzima.

Wanangu wakaona isiwe tabu maana wameni push wapi nimegoma wakaamua wanisakizie. Siku moja mapindi yameisha tupo free, jamaa angu mmoja akamfuata mtoto akaja nae mimi nilikua sina habari. Ghafla nikashangaa mtoto huyu hapa, jamaa nae alivyo na mbwembwe akamwambia Latifa naomba umsikilize kwa makini ndugu yangu huyu mpe nafasi usije ukamuua bure halafu akasepa.

Huku nyuma akaacha kivumbi na hapo sasa ndo ilikua balaa, mapigo ya moyo yakaanza kwenda faster, kiswahili kikageuka kingereza [emoji23] kikawa hakipandi kabisa ni kama nacho kilikuja na meli. Na mtoto alivyokua anajiamini muda wote ananiangalia usoni, ukicheki macho meupe kama Selena Gomez, basi mimi nguvu ndo zikawa zinaniisha kabisa kilichofuatia hapo mpaka leo nikikumbuka hua nacheka sana

[emoji125][emoji125][emoji125][emoji125]
 
Back
Top Bottom