Je, siku ya kwanza kutongoza/kutongozwa ilikuwaje?

Je, siku ya kwanza kutongoza/kutongozwa ilikuwaje?

Wanasema hata uwe kauzu vipi huwezi kujamba wakati unatongoza,, ila mimi nilijamba aiseh Nashukuru ilikua in silence mode halafu haikunuka kabisa [emoji23][emoji28][emoji1]

Tupo school hapo, kuna demu ana asili ya kiarabu jina lake Latifa. Huyu mtoto tulikutana kwenye mchezo wa volleyball. Yeye na wenzake walikua hawajui so wakawa wananyanyasika sana. Mzee mzima nikawa nawatetea lakini sababu kubwa ni huyu Latifa.
Katika kujali kwangu mtoto akatokea kunielewa. Lakini mzee mzima nilikua mgumu (hip hop) sana. Kitu pekee nilikua nawaza wakati huo ni kupiga chetezo kanisani na kuishabikia Man u ya Sir Alex.

Washkaji wananiambia dogo anakuelewa lakini me sina habari domo lote limejaa gundi. Kiukweli nilikua nampenda lakini nikitaka niende nafikiria hadhi yangu na uzuri wake + mabishoo wa shule wanaomtongoza basi naishia kukata tamaa, kifupi nilijidharau sababu she was so hot shule nzima.

Wanangu wakaona isiwe tabu maana wameni push wapi nimegoma wakaamua wanisakizie. Siku moja mapindi yameisha tupo free, jamaa angu mmoja akamfuata mtoto akaja nae mimi nilikua sina habari. Ghafla nikashangaa mtoto huyu hapa, jamaa nae alivyo na mbwembwe akamwambia Latifa naomba umsikilize kwa makini ndugu yangu huyu mpe nafasi usije ukamuua bure halafu akasepa.

Huku nyuma akaacha kivumbi na hapo sasa ndo ilikua balaa, mapigo ya moyo yakaanza kwenda faster, kiswahili kikageuka kingereza [emoji23] kikawa hakipandi kabisa ni kama nacho kilikuja na meli. Na mtoto alivyokua anajiamini muda wote ananiangalia usoni, ukicheki macho meupe kama Selena Gomez, basi mimi nguvu ndo zikawa zinaniisha kabisa kilichofuatia hapo mpaka leo nikikumbuka hua nacheka sana

[emoji125][emoji125][emoji125][emoji125]
Nyota mbili luteni
 
Nakumbuka nikiwa standard six kuna kamkaka sijui nikaite katoto maana wote tulikua na miaka 11, yaan alikua kila nikimuangalia ananikonyeza bas mimi nikawa sipendi yan.

Siku akajiloga akaniandikia barua ya kunitongoza yaan nliipeleka moja kwa moja kwa mama angu huku nalia kilio kama kuna msiba[emoji1][emoji1].. naulizwa shida nini apo siwez hata kuongea, nkaelezea hadi ya kukonyezwa darasani.. basi mama angu akaniambia twende tumfuate kwao maana alikua ni jirani tu..

Aisee yule mtoto alipigwa na kaka ake hatari, na ndio ilikua mara yake ya mwisho kunisemesha... Ht nikikutana nae leo hii huwa hawez hata kunisalimia, mimi nikimuona huwa natamani kucheka[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
😂😂😂 we Dada una roho mbaya sana hata kama ilikuwa ni utoto "Unaipeleka barua kwa mama ako huku unalia kama msiba kisa umetongozwa" 🙂🙂🙂 ni uzandiki wa hali ya juu
 
Wazo la kwanza kunijia kichwani na lilikuwa likinitia hofu ni "akinikataa je"
mengine wala haikuwa shida.
 
Back
Top Bottom