Je, simu gani inafaa kutengeneza kwa ajili ya kutengeneza content za biashara?

Kyatile

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2017
Posts
1,741
Reaction score
1,588
Habari wanabodi.

Nina duka la nguo na nataka kuanza kuandaa content kwa ajili ya kumarket biashara yangu.

Kwa wenye uzoefu nisaidieni kujua ni simu gani kwa bajeti ya 2.5M itanipatia simu nzuri yenye kutoa video bora?

Je ninunue Samsung S26 Ultra mpya au Used iPhone 16/17 pro max au google pixel?
 
Kwa hiyo bajeti nunua used 16 Pro Max 256GB ndio all rounder kwenye business posts.

Usinunue Pixel ina picha nzuri ila video stability mbaya na quality yake mbaya uki-share kwenye social media platforms hasa WhatsApp.

Samsung somehow ni better balanced kwa matumizi binafsi ila kibiashara bado iPhone ni better option. Picha zake ni sawa na video ni bora zaidi. Haipotezi quality sana kwenye sharing ya pics na videos.
 
Ni bora kununua camera kuanzia canon 5d mark3 itakupa kitu bora zaidi kwa bajeti yako hiyo
Naelewa lakini limitations za camera ni kwamba haiwezi kutuma video wala picha kwenye mitandao ya kijamii hivyo itanilazimu kununua simu yenye uwezo mzuri. Kwa bajeti yangu hiyo nataka ninunue simu ambayo itakamilisha kila kitu, in future nitanunua camera.
 
Unaweza tumia camera kufanyia mambo yako then unaamishia kwenye simu saizi mambo ni rahisi sana bwashee
 
Ni bora kununua camera kuanzia canon 5d mark3 itakupa kitu bora zaidi kwa bajeti yako hiyo
Camera ili ikupe kitu bora inabidi ujifunze kuitumia na uwe na muda wa kutosha.
Simu ni sekunde kadhaa unapiga picha/video na kutuma hapo hapo.

Assume unauza viatu mtu yuko mkoani anakwambia hicho kiatu cheusi ulivhopost una kingine rangi ya beige cha size 43? Unasema ndio anakwambia piga picha unitumie nione, mwenye simu anapiga picha anatuma. Wewe na Canon yako unaanza ku-mount madude gani sijui na ukimaliza uhamishie kwa simu. Hapo una wateja na mambo kibao.

Camera zinatumika kwenye biashara zisizo na varieties nyingi. Unauza spares za magari kama ni fuel filter fulani ni hiyo tu, kama ni oil ya Oryx ni hiyo hiyo. Camera ni kwa kurekodi bidhaa zote ukawa unapost, au kufanya content kubwa mara kadhaa tu.
 
Je ataweza kua na uwezo wa kununua kila toleo kwa mwaka husika maana camera za simu hizi zinakuja kila mwaka wanabadili matoleo
 
Hata camera zina matoleo kila mwaka. Hiyo Canon 5d Mk III uliyopendekeza ilitolewa 2012. Nimemshauri kulingana na bajeti yake hata angekuwa na bajeti ndogo ningemshauri kuanzia iPhone 13 Pro.
 
Ni kweli ila camera toleo lake linadumu kwa muda mrefu kulinganisha na cm kwa iPhone 13 pro ni best
 
Back
Top Bottom