JE single Father nae anaruhusiwa kuowa Binti kigoli ambaye ni mgeni kwenye ntansinia ya mapenzi?

JE single Father nae anaruhusiwa kuowa Binti kigoli ambaye ni mgeni kwenye ntansinia ya mapenzi?

Salam kwenu wakuu!

Twende kwenye mada husika, yupo mwamba moja yeye ana umri wa miaka 39 saivi, na hadi sasa ana watoto 6, wanne mama tofauti tofauti, na wawili mama moja huyo ndo waliishi nae km 8yrs, wakaachana, hao wengine jamaa alipita tu, ss baada ya kuachana na huyu alieishi nae (japo hakumwoa,waliishi tu) jamaa amepata Binti swala 5 tena kigori na sasa jamaa anataka kufunga zile pingu zinazoitwa za maisha, swali linakuja je huyo jamaa hata kuwa ameingia chaka kuowa Binti mdogo na timu aliyonayo maana ana 23 umri huyo Binti na upande wa Binti hata kuwa hajatendewa haki kuingia Kwa mwanaume Mwenye tayari timu ya watoto? Kuusu kipato Cha jamaa ni normal tu mpambanaji, hii imekaaje wakuu?
Sasa akioa si atapoteza sifa ya kuwa single father?
 
Miaka 23 sio binti mdogo, uyo tayari ni mwanamke mtu mzima. Kuhusu idadi ya watoto alioanao jamaa kama uyp mwanamke anayo iyo taarifa na amekubali kuolewa nae basi hakuna shida kabisa.

Suala la bikira linawabana zaidi wanawake. Ndio maana kijamii na kiroho mwanaume anaweza kuwa na wake wengi lakini mwanamke hawezi kuwa na waume wengi.
 
Back
Top Bottom