Nimesikitika sana, Nyerere, mtu aliyeweza kutuibia alivyotaka kama Mobutu alivyoiba Congo, lakini kwa uadilifu mkubwa akaishi maisha simple tu, kwa muktadha wa kiongozi wa taifa, leo hii amekuja kusingiziwa wizi kijinga hivi.
Nyerere ana makosa mengi, kifalsafa, kisiasa, lakini hili la wizi bado sijaliona.
Alipofariki Nyerere, alikuja Mama Gracia Machel, mke wake Mandela, mwanzo kabisa, akitaka kuwa karibu na mjane Mama Maria Nyerere msibani.
Basi yule Mama akapelekwa Msasani kwa Nyerere.
Alipofika Msasani, alivyopaona pako simple vile, na jina la Nyerere alivyolijua limevuma dunia nzima miaka na miaka kwamba Nyerere ni bonge la giant katika siasa za dunia, yule Mama akaona bila shaka hapa si kwa Nyerere, hii ni government guest house tu nimeletwa kupumzika kabla ya kufika kwa Nyerere.
Mama Gracia Machel akasema jamani nipelekeni kwa Nyerere nataka kufika mara moja nikae na Mama Maria, msinicheleweshe.
Watu wakamwambia Mama mbona umeshafika kwa Nyerere ndiyo hapa.
Yule Mama alivyopaona pako simple ilikuwa kama hajaamini hapo ndiyo kwa Nyerere.
Nyumba ya Butiama ya Nyerere aliyojengewa na jeshi ndani kuna viti vya plastiki. Vile viti wanavyoweka watu kukalia nje kwenye bar kunywa pombe, viko ndani Wazanaki wanakalia. Kama vile si nyumbani kwa rais.
Sasa mtu kama huyo aibe hela afanyie nini?