Je, Sokoine alikufa kwa ajali ya gari, Au aliuawa kwa kupigwa risasi 18 kifuani?

labda alikuwa hapendi show off
Ukizama sana kwenye falsafa unakuwa mtu wa kupenda knowledge, ideas, vitabu, kuliko kupenda kulimbikiza mali.

Kwa hivyo, kwa mtu kama Nyerere, kupigania uhuru wa nchi ya Tanganyika na kuweka muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, na kujenga Umoja wa Kitifa katika nchi hii ni mafanikio makubwa kuliko utajiri wowote wa mali.

Hebu fikiria hivi. Kuna mamilionea kibao duniani.

Lakini, kuna watu wangapi wameanzisha nchi?
 
Dube wala hakukaa jela miaka yote hiyo. Mara baada ya kuhukumiwa alirudishwa kwao Afrika Kusini miaka ile ile ya 80 kabla akina Mandela hawajachukua nchi.
 
Nyerere hakuanzisha nchi bali alizaliwa akakuta tayari kuna nchi na ina mipaka yake japo iliwekwa na mabeberu. Aliikuta nchi ambayo tayari lugha ya Kiswahili ilishawaunganisha watu wa makabila mbalimbali. Aliikuta nchi ambayo watu wake hawakuwa na ukabila na wanaoleana. Aliporudi nchini kutoka masomoni Uingereza tayari aliwakuta akina Abdul Sykes na wenzake wameshaanzisha TAA na inafanya vizuri. Hata jina la TANU ni pendekezo la Sykes. Wenzake walimwamini na kumpa uongozi japo aliwageuka baadaye. Mchango wa Mwalimu kwa uhuru wa nchi hii ni mkubwa sana na hatuwezi kuupuuza lakini kuamini eti alianzisha nchi kama unavyosema huo ni upotoshaji.
 
Dube wala hakukaa jela miaka yote hiyo. Mara baada ya kuhukumiwa alirudishwa kwao Afrika Kusini miaka ile ile ya 80 kabla akina Mandela hawajachukua nchi.

13 ni jumla ya mvua alizopigwa. Kuna tofauti ya mvua alizopigwa na alizokaa naamini.

Sidhani angeweza kurudishwa Afrika kusini ya makabiliano, labda japo ya akina Mandela.
 
Alikuwa Tsar Nicholaus Alexander na familia yake waliuawa na Bolsheviks baada ya kuchukua nchi baada ya mapinduzi ya Oktoba 1917. Waliuawa kinyama sana na washenzi wale.
 
Mkuu hizo nukuu hazijawekewa rejea vyanzo vyake watu wakathibitishe ukweli wake.
 

Unasema Nyerere hakuanzisha nchi, aliikuta nchi.

Nchi gani?

Nyerere alizaliwa 1922.

Mwaka 1922 kulikuwa na nchi inaitwa Tanzania?
 
Unasema Nyerere hakuanzisha nchi, aliikuta nchi.

Nchi gani?

Nyerere alizaliwa 1922.

Mwaka 1922 kulikuwa na nchi inaitwa Tanzania?
Nyerere aliikuta nchi inaitwa Tanganyika na alikuta imeshaanzishwa. Na hii Tanzania hakuanzisha bali alibadilisha tu jina yeye na Karume baada ya kuunganisha nchi zao. Mtu anaanzisha kitu ambacho hakikuwepo sasa Tanganyika ilikuwepo na Zanzibar ilikuwepo yeye kaanzisha nini hapo?
 
Nyerere hakuanzisha nchi inayoitwa Tanzania, kwa kuiunganisha Tanganyika na Zanzibar, na kutengeneza Muungano wa Tanzania, pamoja na Karume?

Unasema mtu anaanzisha kitu ambacho hakikuwepo. Na Nyerere kaikuta nchi inaitwa Tanganyika.

Tanzania ilikuwepo kabla ya Muungano wa 1964?

Nyerere aliikuta nchi inayoitwa Tanzania alivyozaliwa 1922?

Unaelewa hata unachoandika mwenyewe?
 
"Ikumbukwe kwamba wakati anaondoka kwenda Dodoma Marehemu Sokoine alisema maneo ya mwisho yafuatayo:Nikimaliza kuwatumbua majipu mawaziri wangu, basi napanda juu nikamtumbue majipu Mwalimu Nyerere kwa vile anaonekana siyo msafi"
Twende bungeni ... Kama hayo yalisemwa kweli na sokoine. Hilo la kumtumbua nyerere ni uongo halikusemwa. Nakumbuka vema niliisikia hotuba hiyo sokoine akihutubia bunge.
 
[emoji3525] utapeli huu
 
Kuna reference yoyote kupata hizi direct quotations? Maana umeandika kma vile ni fact sio speculation au hearsay.
 
Shukrani sana mkuu
 
"Ikumbukwe kwamba wakati anaondoka kwenda Dodoma Marehemu Sokoine alisema maneo ya mwisho yafuatayo:Nikimaliza kuwatumbua majipu mawaziri wangu, basi napanda juu nikamtumbue majipu Mwalimu Nyerere kwa vile anaonekana siyo msafi"
Huu utakuwa ushuzi kama mashuzi mengine tu
 
Kwanza ni wazi muandishi hamfahamu vyema Shaba. Prof. Shaba alikuwa pathologist (bingwa wa kupasua maiti) na siyo surgeon.
Pili ni kweli Prof. alikuwa mnywaji mzuri lakini alikuwa na weledi na maadili ya hali ya juu sana. Baada ya ajali hii Prof alikuja kikazi kwenye taasisi yetu. Akiwa na rafiki yake kipenzi Prof alikataa kata kata kujibu swali lolote kuhusu ajali hiyo hata pale alipokiwa ameutwika sawa sawa na tulikuwa nae kwa takribani wiki moja. Na kila siku tulipiga maji nae kwenye club ya taasisi. Hivyo simuoni Prof akiyasema hayo ya risasi 18.
 
Naweza kuamini kwa sababu Kambarage alikuwa hana pesa ya kulipa mishahara ,na alikuwa hataki mikopo worldbank na Imf
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…