Je System imeamua kumu expose Samia?

Je System imeamua kumu expose Samia?

Kwanza hiyo system haimtaki Toka aliporithi.system ilitaka kupindisha katiba ili huyu asirithi maana mafaili yake yalionesha huyu hakuna kitu hadi jeshi wakatishia kuichukua Nchi Kwa mtutu ndiyo ponapona yake.Kwa yanayotokea Kwa Sasa nchini kwetu inaonesha kabisa system waliona mbali mita 200 na walikuwa sahihi 100%

Ndomana kuna kitu kamanda Mobeyo enzi za uongozi wake alitaka kuongea ila akakausha tu.
 
Kwa yanayoendelea kuhusu kutajwa moja kwa moja mtoto wa Rais kuhonga wanasiasa wanaoonekana kuleta ushindani kisiasa dhidi ya Rais (Mama yake) swali kuu tunalopaswa kujiuliza ni;

Je System imeamua kumu expose Samia?

Je System imemchoka Samia?

Niliwahi kusikia huko nyuma kuwa System ina njia nyingi sana za kufanya kazi:

Kwanza wanaweza kukuletea taarifa na ushauri tu! Endapo wakiona husikilizi ushauri watatumia watu wako wa karibu kukushauri! Na endapo utazidi kukaza shingo basi wata ku expose ili umma ujue mambo yako na uwe kwenye wakati mgumu.

Kwa wanaoangalia siasa kwa jicho la kawaida hawawezi ona maana halisi ya mabishano ya Lissu na Wenje huku akitajwa moja kwa moja mtoto wa Rais.

Kwa tunaoangalia siasa kwa macho yote ya ndani na nje hii ni alert kubwa sana kwa Samia maana inaonekana sasa ameanza kuchokwa na dola.

Sio hivyo tu ni ishara kuwa hata CCM wameanza kuchokwa na dola.


Tuzidi kuomba haya yazidi kuendelea maana kupitia haya inawezekana Tanzania ikaja kupata ukombozi wa kweli.
Muongo sana wew!! Kwani mtoto wa Rais katajwa na system au huyo bwana wako anayeitwa Lissu? Hivi wew ulimjuwaje Abdul kama si kiherehere cha Lissu?! Au system uloikusudia ni Lissu??
 
Kwanza hiyo system haimtaki Toka aliporithi.system ilitaka kupindisha katiba ili huyu asirithi maana mafaili yake yalionesha huyu hakuna kitu hadi jeshi wakatishia kuichukua Nchi Kwa mtutu ndiyo ponapona yake.Kwa yanayotokea Kwa Sasa nchini kwetu inaonesha kabisa system waliona mbali mita 200 na walikuwa sahihi 100%
Kwanini hawakuiacha Jeshi lichukuwe nchi? JWTZ inaheshimiwa na wananchi wote. Saa hii tungekuwa tumenyooshwa na kuwa na nidhamu. Na uchawa usingekuwepo. Uchawa ni dhambi!
 
wanasahau kwamba raisi samia alivyochukuwa power akina tundu lisu &co. walifurahia sana, raisi samia moja ya safari zake za kwanza ilikuwa ubelgiji na alikutana na tundu lisu na sijui akampa passport huo usanii wote ulikuwa live hapa, hata tundu lisu kusema sijui kurudi “nyumbani” na kupokelewa kama mfalme yote ni wa raisi samia leo hii iweje awe mbaya? tundu lisu kuna mambo waliahidiana labda kwenye kushare power sasa kutimiziana imeshindikana na sasa imekuwa mwaga mboga nimwage ugali kama tusemavyo waswahili lkn hakuna chochote hapo ni usanii tu, besides kuna sababu kwa nini tundu lisu anaweza ongea chochote bila ya chochote kumpata, labda anajua mengi lkn nafikiri kuna mpaka pia ngoja tusubiri …
We ndio Abdul😅😅
 
Back
Top Bottom