Je, tabia njema hujengwa na malezi bora, dini au ni hulka asilia ya mtu?

Je, tabia njema hujengwa na malezi bora, dini au ni hulka asilia ya mtu?

yuzazifu

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2018
Posts
5,108
Reaction score
9,436
Salaam wakuu,

Nimeuliza hili kwa sababu kuna watu wamepata malezi bora, pia wazazi wana dini lakini wao wanatabia mbovu but kuna wengine hawakupata malezi bora bt wana tabia njema sana.

Je, kwa upande wako tabia njema inajengwa na malezi bora, dini au ni hulka asilia ya mtu?
 
Hiki kizazi cha katuni na kadhalika. Mungu atusaidie sana utalea vizuri, dini na mawaidha lukuki. Aiseeee utaletewa kesi kidume chako kinampanda kidume cha mzee fulani na wamekamatwa nyekundu mkononi (red handed). Hakika utajiuliza siku ina masaa mangapi 24 au 28?
 
Malezi bora ni yapi?
Mimi naamini tabia ya mtoto inategemea sana na namna wazazi wake wanavyoishi.
Mtoto anaangalia na anaiga kutoka kwao.
Una watu nawafaham wazazi wao walevi, hawana maadili yoyote, hawana care yoyete kwa watoto wao bt watoto wapo na tabia njema sana tofaut na wazazi wao.
 
Umeuliza swali zuri sana.

Naanzia hapa,watu wengi sijui huwa wanatumia vipimo gani kujua familia fulani ina dini au la ?

Kadhalika sijui huwa mnatumia vipimo gani kujua malezi mazuri, wengine huku kwetu huchukulia ya kuwa malezi bora ni mtoto kupata anachotaka kwa wakati, yaani maisha mazuri ya mboga saba.

Jibu la swali lako ni kuwa DINI ndiyo inamfunza mtoto kuwa na tabia njema. Baadhi ya wakati mtoto kuwa na tabia mbaya,huo huwa ni mtihani wanao pewa wazazi kwa watoto wao bali na mtoto mwenyewe.

Kadhalika, tabia njema hufundishwa yaani somo ni maalumu, kama fulani anavyosomea utabibu na mfano wake, ila somo hili halina cheti.

Mwisho kabisa hakuna mja anae muongoa mja mwingine, bali sisi sote tunafanya juhudu ya kufanya yaliyo mazuri.

Shukrani.
 
1. Wazazi na familia uliyozaliwa(tabia za wazazi na marafiki zao)--mf kama wazazi na circle yao ni wagomvi/walevi---very likely utakuwa hivyo
2. Mazingira(Hasa kuanzia miaka 0 hadi 11)--hii inahusisha nchi uliokulia,shule,majirani,marafiki,na uhusishwaji katika dini na shughuli za maisha
3. Dini na Utamaduni.
 
Inategemea kwa kweli.

Kuna ndugu ninaowafamu wamezaliwa na kukuzwa na wazazi wao. Wako 6 ila Kati yao 2 kwa kweli wana tabia ambayo kila awaone huwahukumu ya kuwa Wana tabia mbaya.

Mfano mwingine Ni Mimi binafsi Ni melelewa na Bibi alikua mzee Tena asie ona. Lakini tabia yangu kila ninaekutana nae awe ananijua ama hanijui anasema ni njema.

Nilipona mdogo chini ya malezi ya yule Bibi nilikua na fursa zote za kua na tabia mbaya ama uhuni, lakini imekua Ni kinyume chake.

Hivyo Kuna mchango wa walezi na pia mtu husika anachangia kua na tabia mbaya ama njema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Malezi bora ni yapi?

Mimi naamini tabia ya mtoto inategemea sana na namna wazazi wake wanavyoishi.

Mtoto anaangalia na anaiga kutoka kwao.
Ni kweli kabisa mtoto huiga kutoka haswa kwa mzazi , mfano wakati fulani kwenye nyumba za kupanga hizi ambazo Zina kutanisha familia nyingi ama Kaya nyingi, wanapokutana watoto ndio kila mmoja huonyesha yanayosemwa chumbani kwa wazazi wao.

Kuna wengine walikua wanatukana matusi yale magumu kabisa kiasi ambacho wewe unaesikia unaziba sikio! Lakini ajabu yule mtoto hajui maana yake ni nini. Ila tu amesikia kwa baba na mama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vyote vitatu ni nguzo za tabia njema malezi bora, dini na hulka asilia ya mtu.
 
Kamwe mtoto wa kenge hawezi kuwa mjisi
 
Malezi bora na hulka ya mtu
 
Watoto hatujifunzi kwa kuambiwa na wazazi. Ila tunajifunza kwa Yale tunayoyaona wazazi wakiyatenda mbele yetu.

Unaweza ukanilea vyema & vizuri ila nikawa na tabia zako za umalaya.
 
1. Hulka ya mtu.

Mimi naamini kila mtu hua anazaliwa na personality yake ambayo baadae hua inakuja ku determine huyo mtu atakua mtu wa aina gani.

Ndio maana mtoto anaweza ukamuona tangu akiwa mchanga kwamba huyu ni mtundu/mpole nk.

Kuna tabia ambazo mtu anaweza kuiga kutoka kwa jamii lakini mwisho wa siku hulka yake ndio itaamua kama jamii itambadilisha au la.
 
Una watu nawafaham wazazi wao walevi, hawana maadili yoyote, hawana care yoyete kwa watoto wao bt watoto wapo na tabia njema sana tofaut na wazazi wao
Ni mambo anuai yanayopelekea tabia njema. Kwa mfano huo hapo wa wazazi walevi, ni kwamba tabia hiyo inawafedhehesha na kuwadharaulisha watoto. Kwa vyovyote hawatataka kuishi maisha ya kishenzi kama hayo. Ila usishangae akitokea mmoja atajayeangukia huko. Ni busara na uelewa wa mtu,vinamfanya ajiweke vipi katika maisha yake.
 
Salaam wakuu,

Nimeuliza hili kwa sababu kuna watu wamepata malezi bora, pia wazazi wana dini lakini wao wanatabia mbovu but kuna wengine hawakupata malezi bora bt wana tabia njema sana.

Je, kwa upande wako tabia njema inajengwa na malezi bora, dini au ni hulka asilia ya mtu?
Yote ya yote kila kumbe (binadamu) ana chemistry yake !!
FYI, wazazi wema hupata watoto chakaramu!
Na wapo wazazi ovyo hupata watoto Angel's watiifu...
Hidaya (uongofu) ni wake Mwenyezi Mungu..
 
Salaam wakuu,

Nimeuliza hili kwa sababu kuna watu wamepata malezi bora, pia wazazi wana dini lakini wao wanatabia mbovu but kuna wengine hawakupata malezi bora bt wana tabia njema sana.

Je, kwa upande wako tabia njema inajengwa na malezi bora, dini au ni hulka asilia ya mtu?
Asili ya mtu ndio mtu mwenyewe
 
Back
Top Bottom