Je, Tanzania ipo tayari kuwa Mwenyeji wa Taasisi ya Fedha Ya Afrika Mashariki (EAMI)?

Je, Tanzania ipo tayari kuwa Mwenyeji wa Taasisi ya Fedha Ya Afrika Mashariki (EAMI)?

Hussein Massanza

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
1,016
Reaction score
2,195
Ndugu WanaJF,

Kuna taarifa njema hapa.

Kuelekea uanzishwaji wa Sarafu ya Pamoja na Benki Kuu ya Afrika Mashariki, Waziri wa Fedha amepigia chapuo Taasisi ya Fedha (East African Monetary Institute - EAMI) iliyoanzishwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki iwepo Arusha na Tanzania ipo tayari kuwa nchi Mwenyeji.

Ikumbukwe tayari Makao Makuu ya Afrika Mashariki yapo Tanzania, hivyo hii taasisi ya EAMI kuwepo nchini ni uamuzi sahihi endapo wajumbe wa nchi wanachama watakubali pendekezo hili la Waziri.

Mimi nafikiri Tanzania ina uwezo ukiangalia organs nyingi za EAC zipo hapa na zinafanya vizuri sana, nyie mnaonaje wakuu?
---

TAARIFA KWA UFUPI

Tanzania imewasilisha pendekezo la kuwa Mwenyeji wa Taasisi ya Fedha ya Afrika Mashariki (EAMI) katika kikao cha Kamati ya Uhakiki na Tathmini kilichofanyika jijini Arusha tarehe 20 Machi, 2022.

Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ameieleza kamati na wajumbe wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa Tanzania iko tayari na imeshaandaa rasilimali za kutosha kuiwezesha EAMI kuanza kazi zake haraka, endapo itapatiwa fursa hiyo.

EAMI ni miongoni mwa taasisi muhimu zilizoanzishwa kuelekea lengo kuu la kuanzishwa Sarafu ya Pamoja na Benki Kuu ya Afrika Mashariki.

"Kwa kuzingatia umuhimu wa EAMI kama mtangulizi wa Benki Kuu ya Afrika Mashariki inayotarajiwa, ni muhimu taasisi hii iwepo Arusha - Tanzania, ambako ndiyo Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki." alieleza Dkt. Nchemba
.

IMG-20220320-WA0034.jpg
 
Ukiwa mwenyeji unafaidikaje kiuchumi?

Kwamba sisi ni wenyeji wa mahakama ya haki ya EAC kwa hiyo imeongeza haki kwa Watanzania?

Tuwe wenyeji au tusiwe ni sawa tuu.
 
Ukiwa mwenyeji unafaidikaje kiuchumi?

Kwamba sisi ni wenyeji wa mahakama ya haki ya EAC kwa hiyo imeongeza haki kwa Watanzania?

Tuwe wenyeji au tusiwe ni sawa tuu.

Mbona huulizi kuhusu ufanisi wa EAC Secretariet, IMF East AFRITAC na EAC HQ kwa ujumla? Hizo zote zimeonesha mafanikio na hata Nchi Wanachama zinakiri hilo.

Let's focus on the good.
 
Mbona huulizi kuhusu ufanisi wa EAC Secretariet, IMF East AFRITAC na EAC HQ kwa ujumla? Hizo zote zimeonesha mafanikio na hata Nchi Wanachama zinakiri hilo.

Let's focus on the good.
Haya uliyoandika ndio majibu ya hoja yangu?
 
Ukiwa mwenyeji unafaidikaje kiuchumi?

Kwamba sisi ni wenyeji wa mahakama ya haki ya EAC kwa hiyo imeongeza haki kwa Watanzania?

Tuwe wenyeji au tusiwe ni sawa tuu.
Multiplier effect Cash floor staff na wadau kufuatila huduma.
 
Ukiwa mwenyeji unafaidikaje kiuchumi?

Kwamba sisi ni wenyeji wa mahakama ya haki ya EAC kwa hiyo imeongeza haki kwa Watanzania?

Tuwe wenyeji au tusiwe ni sawa tuu.
Ajira baba ajira! Ukiwachia hizo kubwa ambazo zitakuwa za ushindani, unadhani mfagiaji na muhudumu atatoka nchi jirani?

Wenzetu Kenya wametuwahi zamani ndiyo maana utakuta mashirika makubwa mengi yalikuwa na makao makuu Nairobi.
 
Naam
 
Back
Top Bottom