Uchaguzi 2020 Je, Tanzania tuna upinzani makini, upinzani wa kweli wa kuing'oa CCM madarakani au bado sana? Nilichoshuhudia leo uzinduzi CHADEMA, kiukweli...

Bwana Paskali, wewe ni kada wa CCM uliyajaribu kuwania ubunge ukagaragazwa katika hatua za awali tu. Pengine hilo tu linatosha kuku-disqualify kumjadili, let alone kumhukumu, kiongozi wa kisiasa kitaifa kama Mbowe. Ni sawa na mwanasoka wa timu ya iliyopigwa knockout kombe la mbuzi kujadili UEFA champions league.

Wewe ni mwanahabari kitaaluma. Unajua bayana jinsi TBC ilivyoihujumu Chadema kwa miaka mitano mfululizo. Najua huwezi kuipongeza Chadema kwa kuwa brutally honest kwa sababu most of you wanahabari wa Tanzania don't have word honesty in your vocabularies, lakini hiyo haizuwii mtu yeyote mwenye akili timamu sio tu kufahamu kwanini Chadema walichukua hatua hiyo bali hata kukipongeza chama hicho kwa kuwa wakweli.
 
Eti Censorship kwenye habari Tanzania !
Hebu tuache ujinga TBC wanarushaga habari Hasi kwa CHAdema hamsemi,!
Leo mnalalma
Kulikuwa na shida gani kwa mgombea Ubunge wa Ilala aliposema Magufuli hajaongeza mishahara kwa miaka 5 kwani uongo!Au mkeo aliongezewa!
Kwa Nini wakate matangazo kwa Jambo la wazi Kama Hilo kwa kisingizio Cha kuchambua!
Kumbuka hakuna nchi iliumbwa Ina amani au vurugu!
Kesho hamuijui mjue!
 
Huyu anahitaji ushauri wa njia mbadala atakayoweza kujikimu ili kuhudumia familia yake.

Maana huyu inaonekana ameshanaswa na mdomo wa mamba na hana jinsi ili aishi ni lazima afuate maelekezo.

Angalau mwenzanke Mzee Mwanakijiji kwakuwa anaishi Marekani imemsaidia kutokuwa mateka wa moja kwa moja, ila Pasco kuna sehemu amekwama, muda ni mwalimu mzuri.
 
..I felt like breaking my TV kwa upuuzi waliokuwa wakifanya TBC.

..wao wangetangaza tu, na kama CDM wamevunja sheria wangechukuliwa hatua na vyombo vya dola.
 
Nasema tena kujenga chama imara sio lelemama. Inatakiwa kujitoa kwa hali na mali kwenye nyanja zote ili kupata rasilimali wanachama wenye nia ya dhati na mali za kujenga na kuboresha chama, imani na muda. Mitandao inasaidia kupashana habari za chama lakini mikutano inasaidia zaidi kuamsha ari, mapenzi kwa chama, umoja na imani kwa chama na Kati ya wanachama
Chadema kamati kuu leo ndio mjue kwamba kwa idadi hii ndogo ya watu mkutanoni mashabiki wenu ni mashabiki wa kwenye raha tuu sio raha na shida.
 

Nakukumbusha tu ndugu Pascal Mayalla , kusoma hukumu mbalimbali kwa Mwanasheria ni kitu cha msingi ama cha lazima kabisa.

Katika kesi ya ATTORNEY GENERAL AND TWO OTHERS v WALID KABOUROU (1996) TLR 156 Mahakama ya Rufaa ya Tanzania chini ya Jaji Mkuu Nyalali, na majaji wengine wawili, Kisanga (JJA) na Mfalila (JJA) ilifuta matokeo ya uchaguzi mdogo wa Ubunge wa jimbo la Kigoma mjini kwa sababu mbalimbali, moja ikiwa ni upendeleo wa chombo cha Taifa, Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD)kumpendelea mgombea wa CCM kuliko wa vyama vingine katika kipindi cha uchaguzi.

Sehemu ya hukumu ilisema hivi, “RTD ni redio ya serikali, katika kufanya uchaguzi uwe wa haki, ilikuwa na wajibu wa kutoa muda sawa wa hewani kwa vyama vyote vya siasa na kuviacha viutumie vitakavyo. Mahakama imejiridhisha kuwa jambo hilo halikufanyika na hivyo CCM ilipata muda mwingi hewani kuliko vyama vingine, na hilo likachangia katika kukipa ushindi CCM.

Tuliangalie sasa tangazo la RTD lililotumika kama sehemu ya ushahidi kuonesha upendeleo wake kwa CCM na mgombeawake, lilikuwa hivi,

“Ukweli wa kwanza na wa dhahiri kabisa ni kwamba CCM bado ni chama chenye nguvu kubwa sana na chenye wapenzi wengi walio wanachama na wasio wanachama. Tunasema CCM ina wapenzi ambao hata siyo wanachama wake kwa sababu kuna baadhi ya watu wanafanya makosa kwa kufikiria tu kuhusu namba ya wanachama wa CCM wenye kadi na kupiga hesabu zao zote za kisiasa kwa kuzingatia nambari hiyo ambayo haijafikia hata milioni tano.”

Likaendelea,

“Kosa jingine kubwa wanalofanya ni kudhani kwamba WATANZANIA wote wasio wana-CCM lazima watavipigia kura vyama vingine. Hiyo siyo kweli hata kidogo...., CCM tokea awali imekuwa chama cha Umma badala ya wateule wachache. Tena imekuwa na sera nzuri ambazo zimeitikia matakwa ya wananchi wote kwa wakati wote ambao imekuwa katika uongozi.”

.............

Zingatia hilo mkuu litakusaidia sana kutoonekana kituko
 
Paskali,mmh haya bwana.
TBC waendelee kama walivyokuwa wanafanya muda wote hawa waropokaji wawaachie youtube channels.
 
Hoja ujibiwa kwa hoja sio matusi , ni kweli TBC awatendi haki lakini ni sahihi kuwafukuza.

Labda nadhani mwenyekiti angemwambia Ayoub lyoba hicho unachofanya si haki kwa nini unakata kata matangazo.

Labda Ayoub anacho cha kujitetea lakini Sasa unapeleka ujumbe kwa media zingine waone katika mikutano ya CDM Usalama hakuna
Leo mmewafukuza ipo siku mtawapiga kabisa waandishi wa habari msiowataka.

Hapa CDM mmejibomoa wenyewe kwa jazba zenu

Japo najua mwenyekiti uwenda alipiga ile chupa ya faru John,,
 
Lakini kiukweli....
mipasho na utu uzima huu kha?!
Kawe karibu gwaboy anaishiwa pumzi waambie wakuteue kimkakati uambulie kura hata tano inatosha
 
Kaka andiko lako umeliandika kishabiki saana vingenevyo ulikuwa umeanza vizuri. Pengine ungejivua UCCM ungeaandika kitu kizuri saana. Baadhi ya kauli zako tata zilizokuponza ni hizi "huku unajua kabisa watu wa type yao ni wasemji wa namna gani!, huku Mbowe, huku Lissu, huku Lema, na bado TBC ikakubali kuwapa live, hatua hii pekee, inastahili pongezi." Hao woote uliowataja sijawahi kuwasikia wakisema "nani anataka kupanuliwa" au "barakoha ni kama sidiria za wanawake|", au misemo ya kejeuri kama ya akina msukuma , Ndugai na Lusinde..lakina bado hukuwahi kuwalaumu TBC kwa hilo. Labda kukusaidia jambo ambalo nadhani unatakiwa kuwa unalifahamu kama mwandishi nguli wa habari ni kwamba TBC hawana tena "impact" au mvuto kwenye tasnia ya habari nchii hii hivyo kauli yako ya kwamba Chadema kupoteza fursa waliopewa na TBC haina mashiko pengine sana sana wangekuwa AZAM TV hapo kidogo ungesema kuna tatizo kwani hata hiyo kesho kwenye ufunguzi wa kampenii za CCM zaidi ya asilimia 95% ya watanzania watakuwa wanaangalia AZAM TV na sio TBCCM.
 
kama upinzani ni mediocre kihivyo kama unavyosema, kwa nini CCM inaogopa kwenda kushindana nao kwenye ballot box?
 
Pascal Mayalla,
Hakuna upinzani wa maana ndiyo maana tulishasema CCM itaendelea kutawala hata miaka 50 ijayo. Sasa wewe unaona kabisa Chadema mgombea wake ni Mwanaharakati. Uliona wapi duniani Mwanaharakati anakuwa Rais?!!
 
kama upinzani ni mediocre kihivyo kama unavyosema, kwa nini CCM inaogopa kwenda kushindana nao kwenye ballot box?
Sasa kama mnapewa nafasi tu ya kujieleza mnashindwa? Huko kwenye ballot box nani atawapa kura? Tena mmeshindwa kutumia nafasi hiyo huko Mbagala huku kwetu Mbezi Beach mtaweza kweli?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…