Uchaguzi 2020 Je, Tanzania tuna upinzani makini, upinzani wa kweli wa kuing'oa CCM madarakani au bado sana? Nilichoshuhudia leo uzinduzi CHADEMA, kiukweli...

Mkuu Nguruvi3, kama kuna mtu anaunga mkono kitendo kilichofanywa na TBC kwa namna yoyote ile, mimi namhesabu kama mpuuzi waahed asiyelitakia mema taifa letu, period. Ni heri hata wasingetangaza au hata kuhudhuria huo mkutano wa Chadema kuliko kitendo walichofanya TBC ambacho mimi nakiita cha hujuma katika siku muhimu kama hiyo kwa Watanzania na wana Chadema popote waliko.

TBC ni ya wote na si chombo cha CCM cha kuhujumu mikutano ya vyama vya upinzani. Kwa muda wote toka awamu hii iingie madarakani TBC imekuwa mshiriki wa serikali inayoundwa na CCM ikitetea vitendo vyake vya ukatili dhidi ya Watanzania wanaoikosoa. Kwa maneno mengine, TBC imetumika kuhalalisha utekaji, uteswaji na mauaji yaliyotokea katika kipindi hiki dhidi ya Watanzania wasio wana CCM.

Kama kuna baadhi ya Watanzania wenzangu ambao nimeanza kuwachukia, wako makundi matatu...wanafiki, wachonganishi na ndumilakuwili. Bila kumung'unya maneno TBC wanawakilisha makundi hayo yote matatu, ni wanafiki, wachonganishi na ndumilakuwili. Kilichowapeleka kwenye mkutano wa uzinduzi wa chama cha Chadema ni kufanikisha njama hizo wakisahau kuwa TBC ni chombo cha Umma.

CCM kama chama kikishambulia kwa hoja chama cha upinzani na hata kutafuta namna ya kukidhoofisha kwa mikakati inyoruhusiwa kikatiba hiyo ni rukhsa. Lakini chombo kama TBC, polisi, TCRA na vingine kama hivyo vinapotumika kukandamiza demokrasia na kuwaumiza wasiokubaliana nao, hiyo si rukhsa. TBC badala ya kulialia, iwaombe radhi Watanzania na wapinzani kwa ujumla wao na watende haki kwa wote.
 
TBC walichokuwa wanafanya pale ni hujuma, sasa kama ukimkuta kibaka anazurula kwenye eneo lako utamkaribisha ndani au utamfukuza tena kwa kumpigia kelele za mwizi. TBC walifanya hujuma mchana kweupeeeeee.
Ndio maana hata wakina YESU walitangaza injili kwa hekima mtu alikupiga shavu la kulia mgeuzie na la kushoto
Maneno yenye hekima na busara yanambadilisha mtu kuuona ukweli
Lakini kibuli kama cha CDM kinawabomoa wenyewe
Juzi mlipokea ujumbe kutoka Baraza la wahariri MCT
leo mnafanya tena utoto tena utoto huo anaufanya mwenyekiti mwenyewe wa chama
Mkipata kura zikizidi mil 3 fanyeni sherehe ya mwezi mzima
Lakini kwa ile jana CDM mpo uchi katika fikra na matumizi mazuri ya demokrasia
 
. Nani kakunyanyasa
 


Mkuu sindano imeingia hii, ukiona reaction basi ujue wamekula hii dawa

1.mbowe kakurupuka, hajagundua impact yake
2.kafuata mkumbo
3.kama TBC walifanya ili afanye alichofanya wamefanikiwa sana, hii ni ile unamtemea mate kijanja adui yako uwanjani au kumtusi aki react kwa kukupiga ngumi ndio anaonekana na kupewa kadi nyekundu, kama tes tka fail

4. Same scenario CCM wataibeba na kuutangazia umma wa nje ya nchi, hakuna atakayejua kuwa yalikatwa katwa? How? Kwani kila mmoja kaona?

It was good baada ya hapo alalamike kuwa TBC walikatakata then angesubiri next time!!!!!


Sawa hawa vipofu wa humu ambao kwao mbowe ni saint hawana akili yako ya kuona haya

Pia ndio ujue tuna wengi IQ ya reality ni ndogo mno japo wana degree, diploma na nafasi nzuri makazini mwao. Kwao emotion imetawala brains zao

Ndio hawa ambao wanaamini kabisa Lissu anashinda urais? Then upate shida nao? Huzunika kama unakuwa challenged na watu wenye upeo kama wako

Keep on smiling
 

Zikizidi laki tatu

Sio 3m
 
Kiukweli jana nimesikitika sana kwa kitendo cha TBC kufukuzwa na Mweneykiti wa Chadema Mh. Mbowe. Nilijitahidi kutoka kazini mapema ili nipate wasaa mzuri wa kuwashuhudia Chadema wakifanya uzinduzi wa kampeni zao ili niweze kupata ushawishi wa kuwachagua lakini nilichoambulia kukisikia ni kufukuzwa kwa TBC kutoka hapo viwanjani ikabidi nibadili ratiba nikagonge bia tu. Leo ni siku ya CCM tutawasikiliza na tutaendelea kuwasikiliza. Technically kwa picha ya jana ya Chadema kuwafukuza TBC imejenga taswira mbaya sana dhidi yao toka kwa wapiga kura, hata wale waliokuwa pale viwanjani Mbagala wengi wali-withdraw usikivu kwa viongozi wa Chadema na kuanza kuwaangalia TBC wakiwa wanajiandaa kuondoka wakati huo matangazo yakiwa LIVE. Kwa kweli niliboreka kwa kile alichokifanya Mbowe.
 
Anajua yote tena vizuri sana ila kaamua kujitoa ufahamu ili akidhi vigezo vya kuwa mwanaccm
 
Njaa yako ilikuletea uoga, uoga wako ukakufanya mnafiki.
Unafiki umekufanya mtumwa.
Inabidi uendelee kushangilia chochote kitokacho kwa 'BWANA', hata kama ni kibaya vilevile na hata kuzidi alichotufanyia MKOLONI mweupe.
 
Amueleze Mkurugenzi ili matangazo yarudiwe au iweje! Ile mkutano umekwishapita na TBC wametimiza lengo lao waliloendea na CCM itawapongeza, ila tuliokuwepo kwenye mkutano TBC hatuwapendi wala hamhitajiki kwenye mkutano ya Chadema, Mhe. Mbowe nawe haukufanya busara kuwapa muda mrefu vile wa kuondoka, dakika zisizozidi kumi zingewatosha na hizo waya zao wangekwenda kunjia ofisini kwao.
 
Nilidhani kuwa huu ndio mtazamo wako.
'You are not supposed to be so blind with patriotism that you can't face reality. Wrong is wrong no matter who says it'. Malcom X
Hivi hii 'quote' inaendanaje na uliyobwabwaja juu?
 
Professor Baregu sijui anafanya nini muda wote aliokuwa chadema ameshindwa kuwafundisha siasa za kistaarabu au amewafundisha lakini hawamsikilizi wakati wa kampeni wananchi wanataka kujua mtafanya nini swala la wabunge linaweza kufatiliwa huku kampeni zinaendelea na sio kulazimisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…