1.Sijakuelewa wewe na wenzio mnaolilia niweke nukuu ya aya husika hapa wakati mnayo Kurani mnamaanisha nini.Kama mnaona nimesema uongo kwa nini ninyi hamuiweki nukuu hiyo ili uongo wangu ubainike.
2. Nimeshaelewa ni kwa nini mnang'ang'ania sana niiweke aya hiyo hapa.Na sasa umeweka na condition ya version ya Kurani yenyewe.Niseme tu kwamba mimi ninayo Android App ya Kurani katika simu yangu na hivi simu yangu siku ya Post ilikuwa inasumbua nikashindwa kui-link na PC yangu.Hata hivyo, ili kuonyesha kwamba nina uhakika na nilichokiandika ninakuwekeeni aya hiyo kuanzia 85-96 na aya ambazo zina maeneo ya kubishaniwa nimezi-bold:
"85. (Mwenyezi Mungu) akasema: Sisi tumewatia mtihani watu wako baada yako, na Msamaria amewapoteza.
86. Musa akarudi kwa watu wake kwa ghadhabu na kusikitika. Akasema: Enyi watu wangu! Kwani Mola wenu Mlezi hakukuahidini ahadi nzuri? Je, umekuwa muda mrefu kwenu au mmetaka ikushukieni ghadhabu ya Mola wenu Mlezi, ndio maana mkavunja miadi yangu?
87. Wakasema: Sisi hatukuvunja miadi yako kwa khiari yetu, lakini tulibebeshwa mizigo ya mapambo ya watu, basi tukaitupa. Na hivyo ndivyo alivyo toa shauri Msamaria.
88. Na akawaundia ndama, kiwiliwili chenye sauti. Na wakasema: Huyu ndiye mungu wenu, na mungu wa Musa, lakini alisahau.
89. Je! Hawakuona kuwa hakuwarudishia neno, wala hakuweza kuwadhuru wala kuwafaa?
90. Na hakika Harun alikwisha waambia kabla yake: Enyi watu wangu! Hakika nyinyi mmetiwa mtihanini tu kwa kitu hiki. Na kwa yakini Mola wenu Mlezi ni Arrahmani, Mwingi wa Rehema. Basi nifuateni mimi, na t'iini amri yangu!
91. Wakasema: Hatutaacha kumuabudu mpaka Musa atapo rejea kwetu.
92. (Musa) akasema: Ewe Harun! Ni nini kilicho kuzuia, ulipo waona wamepotea,
93. Hata usinifuate? Je, umeasi amri yangu?
94. Akasema: Ewe mwana wa mama yangu! Usinishike ndevu zangu, wala kichwa changu. Kwa hakika naliogopa usije sema: Umewafarikisha Wana wa Israil, na hukungojea kauli yangu.
95. (Musa) akasema: Ewe Msamaria! Unataka nini ?
96. Akasema: Niliona wasiyo yaona wao, nikashika gao katika unyao wa Mtume. Kisha nikalitupa. Na hivi ndivyo ilivyo nielekeza nafsi yangu.
97. (Musa) akasema: Basi ondoka! Na kwa yakini utakuwa katika maisha ukisema: Usiniguse. Na hakika una ahadi kwako isiyo vunjwa. Na mtazame huyo mungu wako uliye endelea kumuabudu - Sisi kwa hakika tutamchoma moto, kisha tutamtawanya baharini atawanyike."