Je, teknolojia ya roboti wanaoongea ilikuwepo wakati wa Musa na Haruni kama Kurani?

Quran. imeweka wazi unabii Upo kwenye torati sahihi na injili sahihi sio hizi zenu ambazo wakina yohana waliamua kwamakusudi wachague vya kuandika na vile wanavyoona wao aviwafai waviache hata kama alifanya yesu

1. Ni Torati ipi na Injili ipi, ambayo ndiyo haijaharibiwa?
2. Mumezihifadhi wapi matini za Torati hiyo na Injili hizo na mbona hamzitoi hadharani ili wakristu waumbuke?Zimwageniu humu tujionee,basi

3. Torati na Injli ziliharibiwa lini? Ziliharibiwa wakati Muhammad amezaliwa au angali bado kuzaliwa?
 
mkuu acha hasira
sometimes mtu anaonekana mjinga kuamini tu unachoambiwa
hivi mtu anaanzaje kukwambia kaongea na mungu pangoni akiwapeke yake na wewe unaamini!!!!!

Umegonga kwenyewe mkuu! Eti, mashahidi wa Muhammad katika kisa hicho cha pangoni ni mende,mijusi,panya, sisimizi, kenge, popo na nyenyere pekee! Na katika kitu cha kushangaza baada ya kutoka huko Pangoni, akaenda kwa mchungaji wa Kinestorian,aliyeitwa Waraqahal,mjomba wake na Khadija kwenda kupata uthibitisho iwapo kweli aliyeonana naye alikuwa ni Malaika.Kwani kasisi yule ndiye alikuwa Mungu hata Muhammad aamue kusadiki?
 
Kuhusu swala la robot kuran haijasema yule ndama alikuwa robot. Viumbe hai au visivyo hai vikiwezeshwa na Allah vinaweza kuongea. Rejea mawe yaliyokuwa yakimwambia Nabii Daudi 'Nichukue mimi nikamuue Goliath'.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuhusu swala la robot kuran haijasema yule ndama alikuwa robot. Viumbe hai au visivyo hai vikiwezeshwa na Allah vinaweza kuongea. Rejea mawe yaliyokuwa yakimwambia Nabii Daudi 'Nichukue mimi nikamuue Goliath'.

Sent using Jamii Forums mobile app

1. Hakuna anayehoji uwezo wa Mungu bali hoja ni kwamba Msamaria anayedaiwa kulitengeneza roboti hilo, alikuwapo wakati wa enzi za Musa na Haruni?

2. Je,mtume Muhammad alikuwapo wakati wa Musa na Haruni hata atajwe kwamba alishikwa unyayo na msamaria katika mchakato wa kuunda hiyo roboti ya ndama?
 
Kati ya wanajamiii small minds wewe ni mmoja wao..ukiambiwa uprove hlo utaprove au utaongea kw ushabiki

Sent using Jamii Forums mobile app

1. Baadhi ya matukio katika Kurani ndiyo proof yenyewe kwamba Muhammad alikuwa ana-desa mambo kutoka sehemu mbalimbali na kuyafanya kama yeye ndiye original source wakati sivyo.Mojawapo ni hili la sanamu ya ndama kuelezwa kwamba ilitengenezwa na msamaria wakati ukweli wa kihistoria ni kwamba sanamu ya ndama ya walioiabudu waisraeli itengenezwa na Haruni.


2. Tukio ni sanamu ya ndama na waliotengenezewa ni waisraeli.Tofauti katika kisa hicho: Mosi, ni nani alitengeneza sanamu(roboti hilo).Pili, sifa za sanamu yenyewe.Kurani inasema sanamu ilikuwa inatoa sauti,kwa maana ya kuongea.Tatu, kwamba kulikuwapo mtume aliyeshikwa unyayo na msamaria wakati wa kutengeneza sanamu hiyo. Haya mambo hayo matatu ndiyo yanabatilisha ukweli wa simulizi wa Muhammad katika Kurani, mintarafu uundwaji wa sanamu kwa ajili ya waisraeli.
 
Wach nkusany data thn ntakufat ili uone namn ulivyo na akili ndogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
usije huku kama unataka kuujua uislamu,nenda MADRASA ,pia fahamu ya kwamba mungu hashindwi na jambo lolote
 
Chochote ambacho kinakwenda nje ya misingi ya QURAN hicho ni fake na haliwezi kuwa fundisho la kufuata kwenye UISLAMU mfano
19:88-89
"; Na(makafiri) husema: Mwenyezi Mungu) mwingi wa rehema amejifanyia mtoto .bila shaka mumeleta jambo lichukizalo kabisa (kwa kusema hivyo)...

Hivyo chochote kile kinachokwenda nje ya QURAN sio ,taurat sahihi ,wala injili sahihi ata kama mtatoka mishipa kuvitetea na mengine mengi kama lile la bikira Maria mama wangu inashangaza kweli
 
Hii akili au matope nani kakwambia kila SAUTI ni maongezi ? leta hilo andiko uthibitishe kweli sanamu liliongea na liliongea lugha gani?
 

Ukisoma 1 Wakorintho 13:1-13, utajifunza mengi . Uwepo wa Dini na imani zingine duniani Mungu ameruhusu ili UTUKUFU wake uonekane . Huna haja ya kupambana kwa nguvu kubwa kukosoa maandiko wanayoamini wengine wakati hakuna mkamilifu duniani hapa. Onyesha kwa matendo utukufu wa Mungu ulio ndani yako na watu wataona .Giza halimalizwi kwa giza zaidi bali kwa Mwanga.
 

1. Ninakuomba jambo moja tu (na mimi mwenyewe nitakuombea) kwamba uwe na uhai tele.Kuna wanazuoni wa kiislamu mahiri sana ambao sasa wanakiri kwamba Muhammad alipotoshwa na matini za kiyahudi na za baadhi ya wakristu wa mwanzo(mfano wa akina Waraqahal) kudai kwamba Biblia(Torati na Injili) zimeharibiwa.Nitaleta uzi siku pamoja na rejea kamambe na nadhani utashangaa sana.

2. Kuna mambo yatakuja siku zijazo katika uislamu ambayo yatakushangaza sana.Na dalili zimeshaanza tayari.Nakusihi ujivue koti la kung'ang'ania uelewa ambao Muhammad alipotoshwa tu na sasa uupatie jicho jingine ukweli wa mambo.
 
Hizi si ngano tu kaandima Matayo? Ni maneno yake Mungu mwenyewe haya?
Hii ni story tu kaandika Matayo.

Sent using my NOKIA torch
 
Ndugu yangu umejitahidi kujenga hoja lkni zote hazna mashiko kwnza ukizsoma aaya za sura hiyo 20:80-96 apo amezungumzia mtu anaeitwa samiri ten c pekeyke bali wamezungumziwa watu watatu samiri farao pmj na haman kwhyo unaposema samiri moja kw moj ni mtu anaetokea ktk kabila la msamaria unakosea ten huu n uwongo wa kiwango cha dgree mana hakuna aya yyt ktk kuran au hadithi iliyosema samiri n mtu wa kabla la msamaria ndani ya vitabu vya kislamu..ila nlchogundua huujui uislamu ila uliyasoma maandiko juu juu ili tu ujenge hoja zako mbovu.historia y watu wa kale wanasema mtu ambye aliwadanganya waezraili kwmba samiri n mtu wa kabila mmasari n padri anaejulikana km padri dale,sasa uislamu na padri wapi na wapi?mm nkushauri ili nkusaidie kujibu maswali yko uchwara njoo na ushahidi wa aya iliyomo ndani ya qurani inayoeleza samiri mtu tajwa ktk hzo aya ni msamaria man umeuliza maswali kwa waislamu kwhiyo tuongee ushahid utakaouona ndani y qurani..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu acha hasira
sometimes mtu anaonekana mjinga kuamini tu unachoambiwa
hivi mtu anaanzaje kukwambia kaongea na mungu pangoni akiwapeke yake na wewe unaamini!!!!!
Muhammad hakuongea na Mungu pangoni. Period. Una swali lingine?

Sent using my NOKIA torch
 

1.Nguvu kubwa ni ipi? Umeniona kwamba natembea na maspika mitaani kueleza haya ninayoyaeleza?

2. Mungu kuruhusu variations za dini ni suala ambalo halina uthibitisho wowote.Mungu anatuumba na utashi wa kuchagua jema au baya.Kwa hiyo, suala la kusema kwamba Mungu ndiye ameruhusu hata dini zinazompinga yeye katika nafsi zake ni kutaka kuonyesha kwamba Mungu ndiye anayeruhusu watu kufanya dhambi.

3. Hebu karibu tujadiliane zaidi.Mimi sio wa kwanza kuandika, kuchambua Imani ya Uislamu.Kama wewe ni mkatoliki,utafahamu kwamba tayari mtaguso wa II wa Vatican unaruhusu wakatoliki kuusoma Uislamu ili kuufahamu na waislamu wanaalikwa kuusoma Ukristu.Ni kwa kufanya hivyo ndipo majadiliano ya Kiekumene yatakapokuwa na maana zaidi.Nadhani pia huelewi mazungumzo hayo yana maana gani mbele ya safari. Rejea Mkutano wa Wakatoliki na Waislamu uliofanyika Libya mwaka 1976.
 
Muhammad hakuongea na Mungu pangoni. Period. Una swali lingine?

Sent using my NOKIA torch
even if you say it sarcastically
the fact is whoever believes in that laughable story/stories is a damn fool (and this includes bible stories)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…