Je, toyota IST inafaa kwa safari za mkoani?

Hahahah mkuu chombo kikiwa na engine..unaenda nacho popote usiogope kikubwa service..halafu unatembea mwendo laini wa 50-80kph unafika vizuri tu. Pikipiki inatoboa mwanza vizuri tu(kitachomchosha devera ni makalio kuwaka moto kutokana na umbo la kiti cha pikipiki) sasa gari inashindwa vipi.
 
Mi huwa natoka nayo DAR to Kampala DAR gari yeyote inafika ila Sema siku zinaongezeka dar kampala huwa natumia siku tatu nikitoka Kampala asubuhi nalala tinde then napumzika kuepuka tochi naondoka tinde jion kuitafuta Dom obvious nafika usiku mnene then nalala Dom to DAR masaa kumi tu Kampala dar ni Wastani km 1800 IST ulaji wake wa wese inakwenda km 13-16 kwa Lita
 
Upo sahihi kabisa
 
Mimi nilisafiri na Passo Piston3 kutoka Dar mpaka Mwanza nilitoka Dar saa 9 kama na nusu nikaingia Mwanza saa 2 usiku wala sikupata tatizo lolote njiani wala sikupigwa Tochi ilikuwa mwaka jana mwezi wa 10 na niliendesha mwenyewe muda wote wa safari.
Kabisa woga wao tu vits piston 3 nimepiga nayo singida na kurudi tu vizuri,hakuna hata kugusa maji sijui wala oil imepungua na speed nzuri tu 100 max 120 nimefika vizuri na siku ya kurudi nimetoka 12 asubuhi nimefika dar 10 jioni na iko shwari tu sijaona hayo maswala ya feni kuzingua
 
Iyo gari inafika hata south africa ukitaka. Mbona kuna gari kibao (In transit) kama IST, Noah, na nyinginie kbao zinasafiri toka Bongo hadi zimbabwe, Zambia, Malawi, DRC, Rwanda na Burundi. Sasa itakuwa hapo Usukumani
 
Duh... hizi shule za siku hizi si mchezo....
 
Kuna tofauti kubwa sana kwenye uzimaji wa gari kwa engine za petroli na za dizeli zinapokuwa zimetembea mwendo mrefu....

Sijui kwanini watu hawapendi kujifunza...
 
Inatembea hadi mwanza cz natokaga na it Dar saa 12 jioni saa 9 usiku naingia tinde
 
Kabisa mkuu well saidi, uwoga wake tuu ! Hizi machine zipo vizuri kabisa.
 
Nimetoka na kavitz kangu Arusha to Dar halafu nikarudi Arusha.Hakuna kupumzika ni mwendo tu.
 
Ist ni gari ya kwenda sokoni mkuu! Kwa safari ndefu utakua unaionea
 
Gari yoyote yenye piston 4 na kuendelea unaenda nayo popote unapofikiria kwenda. Nilitumia siku mbili tu kutoka dar paka kigali na hio ist bila hata kufungua bonet.
 
Wakuu hebu nisaidieni uwezo wa Toyota Pro box
Unajua nimegundua watanzania wengi ni wageni kwenye hii taluuma ya magari.
Toyota probox ni mashine hasa ,usikaone kadogo hako kagari .Unaweza kusafiri nako km 1600 huku kamebeba kg450 kwenye buti na abiria watano.
 
Unajua nimegundua watanzania wengi ni wageni kwenye hii taluuma ya magari.
Toyota probox ni mashine hasa ,usikaone kadogo hako kagari .Unaweza kusafiri nako km 1600 huku kamebeba kg450 kwenye buti na abiria watano.
Wengi wetu hatufahamu mkuu, humu ndio sehem y kujuzana n kupata maarifa zaidi, nmeona hii story nikaogopa maana unaweza ua gari kwakua tuu huelewi, shukrani mleta huu uzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…