Je, toyota IST inafaa kwa safari za mkoani?

Je, toyota IST inafaa kwa safari za mkoani?

Habari wanajamvi,

Nimetokea kuipenda sana gari toyota IST. Kilichonifanya niipende ni ulaji wake wa mafuta, haina gharama kwenye mafuta. Sasa swali langu je mtu akiamua kusafiri na IST kutoka DAR kwenda Mwanza atatoboa?

Nisaidieni please. Kama kuna mwenye ushauri pia niambieni
Tuambie inakula lita ngapi kwa kilometa . Then Mwanza ni kilometa 120, na utueleze ujazo wa tank lako la mafuta, hapo ndo utajua kama utatoboa ama hutatoboa ukiweka mafuta kiasi gani. Kama ni masuala ya mechanical mcheki fundi kwanza akufanyie safari checkup. Otherwise sijui kama una uzoefu wa sfari ndefu pia.
Lakini la mwisho jiuluze hizo IST zilizopo mwanza zilibebwa ama zilipaa? Fikiri kabla hujauliza.
 
Ili kudumisha maisha ya Gari yako, nashauri pumzika Singida then Ingia Mwanza kesho yake utafika poa kabisa. Mi Ki Ipsum changu nilitoka Iringa nikalala Tabora kesho yake Mwanza tena Sengerema sikuona utofauti wowote mpaka sasa nadunda tu hapa Iringa.
yawezekana ukatoboa lkn life span yake itakuwa mashakani,gari hiyo ni ndogo sana kuhimili miles/km hizo kwa siku 1
 
Tuambie inakula lita ngapi kwa kilometa . Then Mwanza ni kilometa 120, na utueleze ujazo wa tank lako la mafuta, hapo ndo utajua kama utatoboa ama hutatoboa ukiweka mafuta kiasi gani. Kama ni masuala ya mechanical mcheki fundi kwanza akufanyie safari checkup. Otherwise sijui kama una uzoefu wa sfari ndefu pia.
Lakini la mwisho jiuluze hizo IST zilizopo mwanza zilibebwa ama zilipaa? Fikiri kabla hujauliza.
Mkuu angalia vizuri hapo kwenye umbali wa(kilometa 120) Dar to Mwanza.

Gari itafika salama,muhimu ni kufanya service vizuri na kuwa na mwendo wa kawaida(50km/h hadi 110km/h) badala ya kukanyaga kibati hadi injini inung'unike.
 
Cc ngap ndo zinaruhusiwa kufika mwanza frm Dar
uhalisia---sio kama hutafika lkn usalama wa gari yako kwa kwenda km /miles nyingi bila kupumzisha engine hilo ndo tatizo.nadhani hata vitu vyote vikiwa fine mfano coolant,water in radiator,oil nk nk baada ya distance dash board indicator ya heat itakuwa high
 
Kwani mkuu imeandikwa kweny user manual itembee km ngapi kwa Sikh 1
sina uhakika ila nina experience ya gari kama tatu hivi platz,ist na funcargo ambazo zilisafiri km nyingi non stop zilivyofika dar hazikuwa gari tena
 
Habari wanajamvi,

Nimetokea kuipenda sana gari toyota IST. Kilichonifanya niipende ni ulaji wake wa mafuta, haina gharama kwenye mafuta. Sasa swali langu je mtu akiamua kusafiri na IST kutoka DAR kwenda Mwanza atatoboa?

Nisaidieni please. Kama kuna mwenye ushauri pia niambieni
Inatoboa bila wasiwasi na consuption ya mafuta ipo chini sana cha muhimu ni kuzingatia service
 
Ushauri wa bure kwa gari ambayo injini capacity au wengine wanaita cc ni chini ya 1500 sio gari nzuri kwa safari ndefu. Na haswa ambazo zina kuwa na piston 3. Ndio hazifai kabisa. Ist ina cc 1400. Hivyo sio nzuri kwa safari ndefu. Unashauriwa uiitembeze maximum km 800 kwa siku tu. Na katika hizo km hakikisha unazigawa nusu km 400 unaiweka sehemu gari ipumzike ili oil ipoe ishuke kwenye sample na block ipoe Kwa 30 min. gari ikiwa inanguruma tu kisha ndio uendelee na safari. Hii inatokana na kuwa injini zote za gari za kisasa zimetengenezwa na cast na sio chuma kama injini za zamani na cast kwa kawaida ni madini ya udongo yakipata moto sana huwa yanapasuka ghafla hivyo kwa ist sio nzuri kusafiri nayo umbali mrefu wa km 120 ikiwa ni dar hadi mwanza. NB utafika mwanza ndio ila durability ya injini itakuwa imeshuka kwani injini itapata moto sana na oil italainika sana na kuwa kama maji kisha oil itapoteza ile lubriant yake ya kulainisha piston au itapoteza ile kilainishi chake kutokana na joto kali la injini kisha piston zitakuwa zinasagana na piston ringi kwenye block kwa haraka hutaona madhara ila ile combastion ya injini kwenye piston itashuka na utajikuta unapowasha gari yako kesho yake utasikia mlio tofauti kidogo kwenye injini yako kama ni msikilizaji wa mngurumo vizuri na hutaona tena maji yanayotoka kwenye exhaust nyuma ukiwasha gari yako ambayo ni ishara moja ya kuonyesha kuwa njini yako iko intact kwani kianzia kwenze nozel hadi kwenyw plug zikipata moto sana bila lupoozwa kwa wakati hupoteza ule ufanisi wake wa awali.ijapokuwa utaendelea kuitumia gari vizuri lakini durability inakiwa imeshapungua sana. Mwisho ni kuwa sio vyema kuendesha gari yenye cc chini ya 1500 kwa safari ndefu ya zaidi km 800 kwa siku .na zaidi kipimo cha kawaida kwa kama sio mtaalam wa gari ukitaka kujua kuwa inatakiwa uipumzishe gari sasa ni pale utakapoona feni za gari yako kwenye rejeta zinafungua kila saa na hazizimi kwa dakika 5 au zaidi unakuta feni zikizima ni sekunde 3 zinajiwasha tena. Jua unatakiwa kuipumzisha gari yako kwa nusu saa hadi uone feni zinajizima kama kwa dakika 5 au zaidi hapo unaweza kuendelea na safari. Kama hujaelewa nakaribisha maswali zaidi nitajibu
 
Back
Top Bottom