SI KWELI Je, TSC Imesitisha Uhamisho wa Walimu wa Primary kwenda Junior Secondary?

SI KWELI Je, TSC Imesitisha Uhamisho wa Walimu wa Primary kwenda Junior Secondary?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Waraka unaosambaa mitandaoni unadai kuwa Teachers Service Commission (TSC) imesitisha mara moja mpango wa kuwahamisha walimu waliohitimu kutoka shule za msingi kwenda Junior Secondary School (JSS).

Waraka huo, wenye tarehe 8 Septemba 2026, una kichwa “Discontinuation of the Teacher Deployment Process” na unadai hata walimu waliokwisha kufanya verification ya vyeti vyao hawataendelea na mchakato huo. Africa Check

Verdict: FALSE - Waraka huo ni Fake​

TSC imesema haikutoa waraka huo na imewataka walimu kuupuuza.

Mnamo Septemba 10, TSC iliutaja waraka huo kama “FAKE”, ikisema taarifa kuhusu kusitishwa kwa deployment ni ya kupotosha.

Jambo muhimu zaidi ni kwamba portal rasmi ya TSC ya kuomba deployment kutoka Primary kwenda Junior Secondary bado iko active, na inaendelea kuwaalika walimu wanaokidhi masharti kutuma maombi.
 
Tunachokijua
Mpango wa kuwahamisha baadhi ya walimu kutoka Primary kwenda JSS ni mpango halisi wa TSC, unaolenga kutumia walimu wenye qualifications zinazofaa kusaidia mahitaji ya staffing katika Junior Secondary.

Portal rasmi inaeleza kuwa walimu wanaohudumu kwa Permanent and Pensionable terms katika public primary schools na wanaokidhi qualifications wanaweza kuomba deployment kwenda JSS.

Mwaka 2026, TSC pia iliendelea kurekebisha masharti ya qualification. Africa Check ilibaini kuwa Mei 2026 commission ililegeza baadhi ya academic requirements, ikishusha minimum KCSE mean grade kwa baadhi ya walimu wenye secondary-option degrees kutoka C+ hadi C.

Waraka unaosambaa pia unarejelea “Circular No. 18/2026”, lakini uchunguzi haukupata circular hiyo kwenye official communications za TSC

Attachments

  • 802700553_1376200151353629_3162813503765579390_n.jpg
    802700553_1376200151353629_3162813503765579390_n.jpg
    70.2 KB · Views: 12
  • 802700556_1376200278020283_8672930532634005512_n.jpg
    802700556_1376200278020283_8672930532634005512_n.jpg
    33 KB · Views: 11
Back
Top Bottom