Siasa za Lissu ni confrotational haziwezi kudumu..na hivyo mtu anayeamini kwa mrengo huo asipopata wafuasi wanaofanana nae unakuwa ndio mwisho wa chochote anachofanya, kwa maana hiyo hawezi kuwa Mwenyekiti wa chama akafanikiwa sababu hao wafuasi wa kufanana nae sio tu CHADEMA hata kwa nchi nzima ni km hawapo, km wapo ni wachache sana..la pili kuwa Mwenyekiti wa chama cha siasa cha upinzani Tanzania si tu kujua kuongea na kuwa na elimu..inahitaji kujitoa sana kwa rasilimali zako mwenyewe pale inahitajika, mkionyesha hata chumba cha darasa moja tu alichojenga Lissu jimboni kwake wakati akiwa mbunge..niko tayari kufuta huu uzi..Lissu hana sifa ya kuchangia maendeleo kwa kutoa rasilimali toka mfukoni kwake, na kuwa Mwenyekiti wa chama upinzani ni kuwa MLEZI pia..hii sifa Lissu hana! Conclusion..pengine atafaa siku za usoni Mungu akimjalia afya! lkn si kwa sasa..!
kuna jambo jingine CHADEMA wanapaswa kufahamu na nadhani wanafahamu lkn wanachukulia poa..kuna kundi kubwa sana la vijana ndani ya chama ni mamluki..lengo lao ni kuleta fujo kuvuruga MAAMUZI..chama kijihadhari sana na maamuzi yanashinikizwa na vijana..lugha za jazba, ushabiki km wa ccm, matusi, kejeli na dharau na fujo zingine, mkiwafahamu watu hawa dawa ni kutojali sana wanachosema..bahati mbaya hawa ndio wanamsapoti Lissu agombee uenyekiti taifa, kwangu mimi bora kubaki 5 ndani ya chama kuliko kuwa na kundi la vijana 1,000 wa aina ya waliopo CHADEMA kwa sasa.