Je, tuendelee kuamini Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini?

Je, tuendelee kuamini Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini?

Kwani mleta mada isiponyesha wewe unapata hasara gani na ikinyesha ulitegemea utapata faida gani?
Mleta mada ni muuza juice ya miwa. Ilipotilewa tahadhari na TMA akaamua kuachana na biashara ya juice ya miwa kwa kuwa wakati wa mvua biashara hii haifanyi vizuri. Na qkaanza kuokota makopo.
 
Una haraka sana.....

Hili joto kali hujui linaashiria nini ?!?? [emoji15][emoji15][emoji1787]

Kweli shule ulikwenda kutembea....
Hebu tueleze wewe uliyekwenda shule, uashirio wa hilo joto ukoje na linahusika vipi na ujio wa mvua.

Mambo mengine mnajipa ujuaji tu bila ya kujua kitu chochote!

'Seriously', tueleze hapa sayansi yake kama unavyoielewa wewe.
Tutakupa sifa stahiki kwa hiyo shule uliyonayo wewe.
 
Katika siku za karibuni tulipewa taarifa na Mamlaka ya Hewa kuwa kutakuwa na mvua ya el Nino na hivyo wananchi wachukue tahadhari zote kuhusiana na mvua hizi. Walitutahadharisha kuwa mvua hizi zingeanza mwanzoni mwa Oktoba mwaka huu. Leo ni tarehe 8 Oktoba, 2023 na kuna joto kali sana na hakuna dalili ya kunyesha kwa mvua. Ninachouliza Je, tuamini taarifa zenu?. Kama kuna kasoro kwenye taarifa zenu za awali kwa nini msitujulishe tena sisi wananchi?.
Kutakuwa na mvua za hapa na pale..... Yaani Hawa sio wakuwaamini
 
Back
Top Bottom