Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Kuna tuhuma kwamba wachezaji wa mpira wa miguu wa Singida Big Stars wamepewa uraia wa Tanzania kukwepa wasilipe vibali vya kufanya kazi Nchini. Naamini hii ni skendo kubwa na Mamlaka ya NIDA au Uhamiaji zinapaswa kujibu la sivyo taarifa hizi zinaleta uchonganishi kwa serikali.
Sheria ya Uraia inataka mwombaji wa Uraia ajadiliwe na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya na Mkoa, mwombaji awe anafahamu Kiswahili na awe amekaa nchini muda wa miaka kumi kihalali. (PITIENI SHERIA YA URAIA YA TANZANIA UTAONA MASHARTI YALIVYO MAGUMU)
Soma, Pia: Singida Black Stars yawabadilisha Uraia wachezaji wanne wa Kigeni na kuwa raia wa Tanzania ili Kukidhi Kanuni
Lakini pia gharama zinaonyesha si chini ya milioni kumi na mbili kwa mwombaji mmoja. Je, hawa wachezaji wakipewaje huo uraia? Ukiangalia sheria na ukafuatilia wanachojadili wanamichezo utabaini wazi kwamba Mashambuzi wa michezo hawana muda wakusoma na kutafuta taarifa sahihi.
Lakini pia sheria inataka anayeomba Uraia atangazwe kwenye gazeti la serikali, je ni wapi hao wachezaji walitangazwa ili sasa wananchi watoe maoni kuhusu tabia zao?
Kwa vigezo hivi
1. Kujua kiswahili
2. Kukaa Tanzania muda mrefu
3. Kuwa na tabia njema
4. Kuwa mzalendo
5. Kulipia dola 5000 kama gharama za Uraia
6. Kutangazwa kwenye gazeti la serikali watu waseme kama wanapingamizi na maombi hayo
7. Kupitishwa na kamati za ulinzi na usalama wilaya na mikoa
8. Aukane uraia wake wa asili - lini tuliona hao wageni wakiukana uraia wao? Wanaanzaje kwanza? Taifa lao litakubali?
Nataka niwaambie waandishi wa habari za michezo waache ukanjanja la sivyo waseme utaratibu ulipindishwa na watuambie anaweza kupindisha suala nyeti kama la uraia huyo kiongozi ni Mtanzania? Kwamba kucheza mpira tu unapewa uraia? Wapi sheria imesema ukicheza mpira Tanzania ni kigezo cha Uraia?
Kama kuna kitu kama hiki upo umuhimu mkubwa wakukipiga vita na upo uwezekano wapo wageni wengi wanapewa uraia kama njugu hapa nchini kwa sababu tu kiongozi ameamua.
Na hii ndiyo hoja ya mkuu wa majeshi kwamba tunao wakimbizi wengi wanavitambulisho, nadhani kama kuna mwanya huu upo uwezekano hata wagombea ubunge na udiwani wakaandaa RAIA wa kigeni kwa kuwapa uraia ili wapate kura.
Mimi kwa namna nilivyoipitia sheria ya uraia japo sijui imetungwa mwaka gani ila naamini ilitungwa wakati wa mwalimu na ilihusisha wazalendo. Japo sheria hiyo imesema waziri wa mambo ya ndani anaweza kumpa uraia mtu yeyote anayeona inafaa ila siamini kwamba wageni wanapewa uraia wacheze mpira kisa hawana sifa zakulipia vibali. No
Kama uraia ni mwepesi hivi kwanini tunawakataa watanzania DIASPORA? Yaani tuwakatae Watanzania then ardhi yetu tuwape wageni? Kwamba DIASPORA siyo wazalendo ila wachezaji ni wazalendo? Tupeni haki yetu kama mnavyowathamini wageni.