ZirlovimovicZirkov
JF-Expert Member
- Sep 3, 2025
- 358
- 575
Wakuu heshima kwenu.
Baada ya muda mrefu kuwepo nje ya jukwaa Leo nimeamua kurudi kutoa maoni yangu na kushirikiana na wanajukwaa katika kujenga na kukosoa yale yasiofaa.
Kama kichwa Cha habari kinavyouliza hapo juu, Wakuu, Je! tumeamua kumfuga huyu chatu na KUMRUHUSU atawale ndani ya nyumba yetu?. Kichwa changu kimeshindwa kupata majibu ikanibidi nirudi kwa wanajukwaa ili nipate japo wasaa wakujiuliza pamoja na ndugu zangu waishio katika hii nyumba.
Katika nyumba hii Kuna wale ndugu wanaompenda chatu kwa kuwa hapewi vichwa vya watoto wao kama chakula, Pia kuna wale wanaompenda chatu kwa kuwa wanapata ujira kwa kukamata watoto wanaotangatanga na kwenda kumlisha chatu, Pia kuna hawa ndugu zangu namimi ambao hawampendi chatu na wanahofia siku wakiisha watoto wanaotangatanga watakuja kuchukuliwa wao au watoto wao ili wakawe chakula Cha chatu, Mwisho Kuna hawa ndugu zetu pia walioponyoka mdomoni mwa chatu wengi wao wameikimbia nyumba, wanapaza sauti wakiwa mbali kwamba ndani ya nyumba yetu Kuna chatu na Sasa Kila mwanafamilia anajua kwamba ndani ya nyumba yetu Kuna chatu. Swali ni Je! Tumeamua kumfuga chatu?
Kwa taarifa fupi niliyonayo nasikia jumanne kutakua na usafi wa wanafamilia katika nyumba ili kujua kama kweli chatu yupo ndani ya nyumba yetu. Na hapa ndipo msingi wa swali langu ulipo.
Baada ya wanafamilia wa ndani na hata wale waliokimbilia nje ya nyumba kupaza sauti sana juu ya huyu chatu nikasikia tahadhari inatolewa na mlinzi mkuu wa nyumba kwamba Hali yoyote ya kutaka kumtafuta chatu ni kutaka kuichafua nyumba, kutapanya vyombo na hata kuingiza uchafu ndani.
Baada ya taarifa hiyo ya mlinzi mkuu nikipata wasaa wa kutafakari juu ya kauli yake na mambo yaliyotokea hapo kabla, Je! Mlinzi mkuu hajui kwamba mwaka jana Kuna vijana zaidi ya 580 walipotea katika nyumba yetu na inasemekana chatu ndio aliwameza? Je! hata ile ripoti ilipotoka haikutoa majibu juu ya miili ya Hawa vijana Iko wapi? Sasa inakuaje Leo akataze wanafamilia kufanya usafi wa nyumba Yao?
Wakuu hiyo kauli ya mlinzi mkuu wa nyumba yetu ndio imenileta kwenu, tujadili je! ni kweli tumeamua kumfuga chatu ndani ya nyumba yetu? Au mlinzi mkuu nae ni wakala wa kumpelekea chatu chakula?. Je! Tufanyaje kumuua huyu chatu? Tuanze kuumua chatu? Anaempelekea chakula chatu? au anaemlinda chatu?
Naamini katika haya matatu tutafanikiwa kuilinda nyumba yetu. Tukimuua chatu, walinzi na wanaopeleka chakula watakosa kazi hivyo nyumba itakua salama, tukiwaua wanaomlinda chatu chatu atakosa usalama atakimbia au tutamuua kwa urahisi.
Karibuni wanajukwaa tujadili.