Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 376,316
- 871,876
Kwa kimombo tungesema! Did we mess up with wrong generation?
Jibu linaweza kuwa ndio ama hapana kulingana na mitazamo, fikra na maono! Ila kiuhalisia watoto wa mjini wanasema tumeingia cha city.. Sio cha kike!
Tulijisahau sana! Tukadhani wao ndio sisi na mawazo yetu ni yao! Hiki ni kikazi cha maamuzi ya ghafla na matokeo ya haraka! Ni kizazi cha Ku force hata visivyowezekana viwezekane! Kizazi chenye majibu ya matokeo hata kabla ya maswali.. Hiki kizazi kiko mbele ya muda sana!
Tanganyika iko kwenye mtikisiko mkubwa hata kaka hatuko tayari kukiri hilo... Hasara iliyopatikana na inayoendelea kupatikana wa kulaumiwa sio wao bali ni wale wote waliodhani tunaishi kipindi cha juma na Roza, wakati tuko miaka ya mbele mno!
Achana na hasara za miundombinu na mali wakati wa MO 29
Kuna hasara kubwa za kiuchumi
Kuna hasara kubwa za kiusalama! Migawanyiko, kuvuja kwa taarifa nyeti, mivurugano na madhaifu yaliyowekwa wazi juu ya vyombo vyetu vya ulinzi na usalama
Kidiplomasia.. Tumeharibu vibaya sana kwenye hili eneo..hasa taswira ya nchi kimataifa
Umoja na mshikamano.. Hili eneo limetikiswa pia.. Kama sio maamuzi ya haraka ya gen Z ya kufubaza hili tungejikuta kwenye migawanyiko mikubwa ya kiimani
Tunaingia mwezi wa pili sasa nchi ipo kama haipo, yanayoendelea nyuma ya pazia ni mengi na mabaya na mengine yanatisha sana!
Walisema wazi wanataka kusikilizwa! Tena wakaomba kwa unyenyekevu mkuu.. Tutakomaza mafuvu tukawadharau.. Waliahidi wata paralyze uchumi na mifumo ya nchi wasiposikizwa! Ona kinachotokea sasa kwenye utalii
Mambo mengi yamesimama, badala ya kuchukua hatua za haraka tuliokoe na kuliponya taifa kutoka maanguko mengi bado tumedinda na kutaka kushindana nao!
Tukumbuke hawa hawana chochote cha maana cha kupoteza
Hawana familia binafsi
Hawana wategemezi
Hawana kazi nzuri
Hawana vitu vizuri
Hawana.. Hawana. Hawana!
Wanaona option waliyo nayo ni ama kusikilizwa ama kuchukua maamuzi binafsi
Tayari harakati zao za ukombozi zimesha tudhoofisha sana.. Athari zake zitaonekana mwakani
Wamefanikiwa kufubaza mpaka mamlakani kabisa! Mpaka sasa haijulikani nani ni nani na nani na nani wako wapi! Kina ho trend ni rumors za kila aina.. LA uongo la ukweli la kuzusha yote yako kapu moja
Kwa namna moja wametangaza ushindi mkubwa na sasa wanakabia juu
Wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa kuhamisha hofu toka kwao kwenda mamlakani...
Ile boldness ya watawala haipo tena!
Ukisema Gen Z hawajafanikiwa kufubaza mifumo na kuhamisha hofu basi unaweza kukana hata kivuli chako