Je, tumejichanganya na kizazi kisicho sahihi?

Je, tumejichanganya na kizazi kisicho sahihi?

Kwa kimombo tungesema! Did we mess up with wrong generation?
Jibu linaweza kuwa ndio ama hapana kulingana na mitazamo, fikra na maono! Ila kiuhalisia watoto wa mjini wanasema tumeingia cha city.. Sio cha kike!

Tulijisahau sana! Tukadhani wao ndio sisi na mawazo yetu ni yao! Hiki ni kikazi cha maamuzi ya ghafla na matokeo ya haraka! Ni kizazi cha Ku force hata visivyowezekana viwezekane! Kizazi chenye majibu ya matokeo hata kabla ya maswali.. Hiki kizazi kiko mbele ya muda sana!
Tanganyika iko kwenye mtikisiko mkubwa hata kaka hatuko tayari kukiri hilo... Hasara iliyopatikana na inayoendelea kupatikana wa kulaumiwa sio wao bali ni wale wote waliodhani tunaishi kipindi cha juma na Roza, wakati tuko miaka ya mbele mno!
Achana na hasara za miundombinu na mali wakati wa MO 29
Kuna hasara kubwa za kiuchumi
Kuna hasara kubwa za kiusalama! Migawanyiko, kuvuja kwa taarifa nyeti, mivurugano na madhaifu yaliyowekwa wazi juu ya vyombo vyetu vya ulinzi na usalama
Kidiplomasia.. Tumeharibu vibaya sana kwenye hili eneo..hasa taswira ya nchi kimataifa
Umoja na mshikamano.. Hili eneo limetikiswa pia.. Kama sio maamuzi ya haraka ya gen Z ya kufubaza hili tungejikuta kwenye migawanyiko mikubwa ya kiimani
Tunaingia mwezi wa pili sasa nchi ipo kama haipo, yanayoendelea nyuma ya pazia ni mengi na mabaya na mengine yanatisha sana!

Walisema wazi wanataka kusikilizwa! Tena wakaomba kwa unyenyekevu mkuu.. Tutakomaza mafuvu tukawadharau.. Waliahidi wata paralyze uchumi na mifumo ya nchi wasiposikizwa! Ona kinachotokea sasa kwenye utalii

Mambo mengi yamesimama, badala ya kuchukua hatua za haraka tuliokoe na kuliponya taifa kutoka maanguko mengi bado tumedinda na kutaka kushindana nao!
Tukumbuke hawa hawana chochote cha maana cha kupoteza
Hawana familia binafsi
Hawana wategemezi
Hawana kazi nzuri
Hawana vitu vizuri
Hawana.. Hawana. Hawana!

Wanaona option waliyo nayo ni ama kusikilizwa ama kuchukua maamuzi binafsi
Tayari harakati zao za ukombozi zimesha tudhoofisha sana.. Athari zake zitaonekana mwakani
Wamefanikiwa kufubaza mpaka mamlakani kabisa! Mpaka sasa haijulikani nani ni nani na nani na nani wako wapi! Kina ho trend ni rumors za kila aina.. LA uongo la ukweli la kuzusha yote yako kapu moja
Kwa namna moja wametangaza ushindi mkubwa na sasa wanakabia juu
Wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa kuhamisha hofu toka kwao kwenda mamlakani...
Ile boldness ya watawala haipo tena!
Ukisema Gen Z hawajafanikiwa kufubaza mifumo na kuhamisha hofu basi unaweza kukana hata kivuli chakoView attachment 3514118
Kinachofurahisha ni kuona sasa tumejua madhara ya fujo, wizi na uharibifu wa mali. Sasa tuendelee kujutia matendo yetu. Tutaendelea kuuma meno na kusaga meno.
.
Huwa nakumbusha sana ule msemo wetu 'mchuma janga hula na wa kwao' Huu ni mwanzo tu; athari zitaanza kuonekana kuanzia mwakani.

Wale waliokuwepo wakati na baada ya vita vya Uganda watalielewa hili.

Kusudi haiambiwi pole.
 
"Ukisema GUen Z hawajafanikiwa kufubaza mifumo na kuhamasisha hofu basi unaweza kukana hata kivuli chako" Hasara ya Juzi askari kuzunguka juani siku nzima. Gharama za mafuta na helicopter. Magari kutokutembea nchi nzima...
Leo maisha yanaendelea kama kawaida huko mtaani. Jeshi kushinda barabarani ni sehemu ya kazi zao. Wanashinda wanatembea maili nyingi huko maporini hakuna cha ajabu kusimama juani karibu na kipita shoto cha katikati ya jiji.

Ulinzi una gharama zake na kadri siku zinavyokwenda huwa zinaongezeka.
 
Kinachofurahisha ni kuona sasa tumejua madhara ya fujo, wizi na uharibifu wa mali. Sasa tuendelee kujutia matendo yetu. Tutaendelea kuuma meno na kusaga meno.
.
Huwa nakumbusha sana ule msemo wetu 'mchuma janga hula na wa kwao' Huu ni mwanzo tu; athari zitaanza kuonekana kuanzia mwakani.

Wale waliokuwepo wakati na baada ya vita vya Uganda watalielewa hili.

Kusudi haiambiwi pole.
Mwenye kiranga haambiwi pole.
 
Wewe mhamasishaji mkubwa wa maandamano hebu pumzika na hizi threads za *******.

Kwa heshima yako kwenye jukwaa hili ulipaswa utoe ushauri ambao utajenga umoja na amani ya Taifa. Lakini 24/7 uko kuwajaza ujinga hao mnaowaita GenZ ili waone wanadhulumiwa. You are despicable and desperate oldman.
Bwahabwahabwahabwahahahahaaaaa!!!!
 
Unasema hivyo kwa kuwa ulikuwa sebuleni kwako ukiangalia TV. Ile mob ulikuwa huwezi kui control kwa mabomu ya machozi. Risasi za moto ndiyo zimeleleta heshima na utulivu huu tulionao leo
Sio kweli, waliouwawa wengi walikua majumbani kwao. Wale madogo wa mwanza walikua kwenye banda la mpira wanachek game ya Arsenal. Samia aliamua kuua Muandamanaji na asiekua Muandamanaj, so long as ni kijana.
 
KWA MUJIBU WA KATIBA YETU HII YA MWAKA 1977, INASEMA MAMLAKA YA NCHI IKO KWA WANANCHI, YAANI WANANCHI NDIO WENYE NCHI,

KWA LUGHA NYEPESI WAO NDIO WANAAMUA NANI AWE KIONGOZI WAO KWA NIABA YAO KWA MUDA WALIOMPA KUYAENDEA MAENDELEO,

NA HUYO MTU AKIFIKIRI ANAWEZA KUYACHUKUA MADARAKA TOKA MIKONONI MWA WANANCHI NA KUWAWEKA CHINI YA UDHIBITI KWA MTUTU WA BUNDUKI AU MAJESHI ANAJIDANGANYA!

NENDA GOOGLE KAANGALIE SERIKALI INAINGIZA BEI GANI KWA SIKU KUTOKA VYANZO VYOTE? UTAKUTA NI MABILIONI YA PESA,

HUWEZI KUNIAMBIA NCHI KUSIMAMA KIUCHUMI KAMA DESEMBA 09 NA 10 KWA JIJI KAMA DAR ES SALAAM, DODOMA, MWANZA, ARUSHA NA MBEYA, HASARA YAKE NI NDOGO KWA SERIKALI, SEKTA BINAFSI NA HATA KWA PATO LA MWANANCHI WA CHINI WA GENGE, UWAKALA WA PESA, DUKA NAKADHALIKA!

PESA NYINGI SANA IMEPOTEA,
HASARA KUBWA YA MABILIONI IMETOKEA,

LAKINI YOTE HAYO NINYI HAMJALI, MNAONA NI KAWAIDA KULIKO KUWAPA WANANCHI WANACHOTAKA- YAANI HAKI AMBAZO ZILISHATAJWA TANGU OKTOBA 29, NA MMEZIONA KWENYE MABANGO YA DESEMBA 09 MITANDAONI NA POST ZA WAPIGANI HAKI (ITA WANAHARAKATI),

DESEMBA 25 WANARUDI TENA,
WANAKUJA KUDAI YALEYALE AMBAYO MLIYAPUUZA OKTOBA 29, NA KUYAZUIA KWA BUNDUKI NA LOCKDOWN DESEMBA 09,

ISSUE NI JE, MTAWEZA KUSHIKILIA BOMBA KWA MIAKA 5 MFULULIZO IKIWA MWEZI MMOJA TU WA KWANZA UMEKUTANA NA MOTO MKUBWA HIVI?

HABARI NJEMA: TANZANIA MPYA IMESHAKUJA NA HAKUNA WA KUIZUIA KWA NAMNA YOYOTE ILE
 
1765476031851.jpg
 
WEWE JAMAA MCHOCHEZI SANA , ENDELEA NA UGANGA BROTHER. YANI UNAPENDA VIBE ZA MAUGOMVI. NDIMI YAKO INENE MEMA. PUNGUZENI CHUKI, NDIO MAANA UNAPENDA UCHAWI , SISHANGAI
Swali amechochea nn hapo??
Tisaidie ambao hatijaelewa maana ya uchochezi?
 
Gen Z naona mnawaonea bure. Vijana wanatumika kama silaha tu na Master minds hasa wapo behind kuwa pump, ili kufanikisha malengo yao.

Nafikiri Gen Zer wenye hoja nzuri na logical reasoning wapo wachache sana ila wengi ni influence ya kundi rika tu (Mkumbo), na kutaka majibu ya haraka kwenye maswali waliyonayo, ambayo ni hali ya kawaida kwa umri wao.

Binafsi sioni kama ni sahihi pia kukwepa majukumu na kuwabebesha Gen Z matatizo ambayo tumeyatengeneza wenyewe sisi wa generation zilizopita.
 
Ni vzuri Wadau Jamii na serikali ikajua namna ya Kudeal na hiki kizazi kipya Yaani Gen Z.

Hata sisi tunajua tunachangamoto, ila sasa ndo Tupo na nyie hapa na Dunia/Nyakati hazirudi Nyuma.

If there is no Country for US there is no country for you also.
 
Ni vzuri Wadau Jamii na serikali ikajua namna ya Kudeal na hiki kizazi kipya Yaani Gen Z.

Hata sisi tunajua tunachangamoto, ila sasa ndo Tupo na nyie hapa na Dunia/Nyakati hazirudi Nyuma.

If there is no Country for US there is no country for you also.
Hakuna namna mpya, maana nyie sio special group.

Ni swala la kufeli kwa malezi tu na ustaarabu wa dunia, ambao unawakumba watu wote. Maana kama ilivyo kwa uwepo wa watoto wa kisasa; kuna wazazi wa kisasa na wazee wa kisasa vile vile.

Sababu hasa ni mabadiliko makubwa ya teknolojia pamoja na mwingiliano mkubwa wa cultural practices ikichochewa na social networks
 
WAMECHUKUA PICHA ZA 2019 ILI TU WADANGANYE KUNA WATALII ZANZIBAR,

HAWA JAMAA NI WEHU GUYSSSSSS

HAWA JAMAA NI VICHAA GUYSSSS.

HAWA JAMAA NI WENDAWAZIMU GUYSSSS

SASA MNAMDANGANYA NANI?
ILI IONEKANE MNAINGIZA PESA WAKATI UTALII UMEFARIKI?
ILI MUIONESHE JUMUIYA YA KIMATAIFA KWAMBA TANZANIA KUNA USALAMA WAKATI MNAANIKA JWTZ BARABARANI KAMA MISHIKAKI YA KISINIA RESTAURANT?

KWA MWENDO HUU HAMJASEMA BADO, HATA MABUBU WATANENA KWA LUGHA,

HAMUWEZI KUPINGA NAMNA HII 😆😆

HABARI NJEMA: TANZANIA MPYA IMESHAKUJA NA HAKUNA WA KUIZUIA KWA NAMNA YOYOTE ILE
1765562596778.jpg
 
Back
Top Bottom