Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,236
- 10,774
Disclaimer:
Uzi huu ni mawazo ya mwandishi pekee na wala hauna nia ya kuharibu biashara yoyote ya mtu bali kuelezea jamii kuhusu hatari ya kemikali katika vyakula
Katika pitapita zangu nilikwenda kumpa hai rafiki yangu maeneo fulani hapa mjini, nilipata mwaliko wa sikukuu ya Idd hivyo niliona ni jambo jema nikaungana naye katika siku hii. Basi nikafunga safari na kwenda kwake.
Lakini nikiwa pale nyumbani kwake kuna jirani yake ni Mama mtu mzma kiasi miaka kati ya 40 na kitu hivi, alikuwa akiandaa biashara yake ya ubuyu. Nilimpa hai na alinijibu akiwa na uchangamfu mkubwa sana, na kwakuwa tulikuwa nje pale alitumia nafasi hiyo kutangaza biashara yake kuwa anauza ubuyu, akachukua kopo moja ambalo yeye anauza elfu moja na kutupatia ili tuweze kufahamu ubora wa bidhaa yake.
Kiukweli ulikuwa ni ubuyu mtamu sana nikamsifia kuwa anajua kutengeneza bidhaa zake vizuri, ila dakika 20 baadaye nilibadilisha kauli kwani niliona kwa umakini akiwa anaandaa viungo na kemikali ambazo huzipika kisha ndo anaweka ubuyu ili uwe na rangi fulani aidha, Njano, Kijani ama Zambarau.
Kwa haraka haraka niliona akichana mifuko midogo midogo zaidi ya 20 kisha aliweka na maji na kuvichemsha. Hapo nikamuuliza je wateja wake wakubwa ni kina nani? Alinijibu kuwa watoto wa shule ndo huwa wanakula huu ubuyu kwa kasi sana.
Nafahamu kuwa kuna kemikali ambazo zimeruhusiwa zitumike kwenye kuandaa vyakula, mfano, Sodium Benzoate, Sodium Nitrite, Sorbic Acid , Sulfites (Sulfur Dioxide) pamoja na Sodium Metabisulphite.
Pia kuna matumizi ya kemikali za kuongeza ladha kama vile, Citric Acid, Adipic Acid, Sodium Chloride, pamoja na Ethyl Carbamate. Ila hofu yangu ni kuwa je kemikali hizi zina madhara kiasi gani haswa kwa watoto wetu? Mfano, mchanganyiko ambai unawekwa kwenye ubuyu mtamu?
Watoto wanakula barafu (ice cream) ambazo pia zinawekwa kemikali hizi, je usalama wa afya zao umekaaje?