Je, tunahitaji kufundisha shule za msingi na sekondari hizi Slave Trade na Colonialism?

Je, tunahitaji kufundisha shule za msingi na sekondari hizi Slave Trade na Colonialism?

Sunbust Band - Black is Beautiful


Sunburst Band a 1970's from Tanzania, East Africa
Source: Philipe Nole Canicule Tropicale
 
Leo nimeamua kufunguka na ninaomba Mungu sana Mh Waziri wa elimu na taasisi ya ukuzaji mitaala Tanzania isome hii comment yangu thread yangu, ni hivi, mimi ni mwalimu ( nina diploma ya ualimu na nimefundisha somo la historia kwa shule kadhaa za sekondari O and A level kwa miaka kadhaa na nina BA ya Mlimani na Masters ya Social Welfare ya ulaya! na ninaishi ulaya miaka kadhaa now! iko hivi huku ulaya hawasomi kuhusu historia ya Afrika kwenye level za chini ni hadi ufike University ndo unaanza kusoma habari za Afrika! wanajua umuhimu wa historia zao na mila na tamaduni zao! watu wengi hawajui kwa undani kuhusu Afrika zaidi ya jina tu! kuna wazee wa kizungu ukiwaambia unatoka Tanzania wanakuuliza hiyo nchi iko wapi! ninapenda sana kuanzisha mjadala wa kufuta Topics mbili za somo la historia kwa shule za msingi na za sekondari!

Ninapendekeza Topics za Slave Trade na Colonialism zifutwe kwenye mtaala wa shule za msingi na sekondari Tanzania badala yake zifundishwe at university level ambako kijana atakuwa tayari amejielewa na kujiamini.

Hizi topics ni miongoni mwa topics zinazoendeleza unyonge wa Mwafrika na kufuta historia ya Afrika na kuondoa kujiamini kwa mwafrika, zinapoteza kabisa mila na desturi zetu! tunafundishwa kuwa waafrika ni dhalili na hawana akili na kila kitu chao ni cha kishenzi na mtoto anashika vizuri na kujibu paper na kupata A!

Hizi topics zinamfanya mtoto mdogo washule ya msingi na sekondari anaposoma , kukua akijua wazungu na waarabu ni bora kuliko waafrika na wana nguvu na weledi kuliko mwafrika na kumfanya mtoto angali mdogo kutamani kila kitu cha ulaya! Mtoto mdogo ukimuuliza taja makabila kumi na machifu wao wa zamani hajui ila anamjua Messi, anajua Mazombi, anamjua Justine Bieber , Michael Jackson, Ludacris , Kim Kadarshian na Rihanna! na anatakuwa kuwa bongofleva, na wasichana anataka kuwa Miss Chalinze! kizazi chetu kimepotea, wapo wanaoona ukweli huu!

Hizi topics zinashusha thamani ya mwafrika na kumfanya kuabudu ulaya! ni topics zinazobeba sehemu kubwa ya somo la historia na kupoteza ufundishwaji wa historia yetu kama nchi na makabila yetu na mashujaa wetu na sayansi yetu na civilization ya yetu ya mwafrika!

Ukweli ni kuwa ulaya pia kuna shida nyingi na kuna wazungu wengi omba omba huku ulaya, na wanaomba kila mtu anaepita njia hata mwafrika!

Wakati umefika sasa tunahitaji kuwafundisha watoto wadogo mashuleni mila na desturi zetu na hayo ya slave trade na colonialism wakasome University wakiwa matured!

Ni vizuri pia tukisoma kwa kiswahili kuanzia msingi hadi chuo ili tuelewe tunachokisoma! ni hayo tu! naomba kuwasilisha!
@technically
 
Nilichosema si kufuta izo topics bali ni kuziondoa kwa watoto wetu huko msingi na sekondari wasipoteze kujiamini na tuzisome tukiwa wakubwa chuoni, matured! mimi ni muathirika wa hizo topics ndo maana nilipigana kufika ulaya! na sasa napigana kurudi nyumbani baada ya kuionja ulaya tunayoipigania kufika! naamini one day hizi topics zitafutwa na tutapata pure African scholars si kama sisi tulioumizwa na kutukuza uzungu!
Mimi nashauri ukamilishe mapigano ya kurudi nyumbani kwanza kisha tuanze haya ya kuondoa historia ya utumwa na ukoloni mashuleni. Kwa ufupi tumeshajifunza takataka nyingi sana huko mashuleni mpaka tumepoteza mwelekeo. Ni ushauri tu!
 
Back
Top Bottom