Je, tutegemee Ridhiwani kuvaa viatu vya baba yake au bado hana ukomavu wa kisiasa?

Je, tutegemee Ridhiwani kuvaa viatu vya baba yake au bado hana ukomavu wa kisiasa?

Kama Mwinyi JR aliweza huyu Kikwete JR hawezi shindwa, CCM mzee wako akiwa na jina una nafasi ya kupata cheo siku za usoni.
Tusishange Chadema ikaja ikachukua nchi kiaina maana imekwisha tanguliza watu wazuri CCM kama akina Kafulila na akina Dr Kitila Mkumbo. hawa wanauwezo wa kutawala nchi. yangu Macho
 
Ni kweli wengi wanakuwa chawa ila akiwa professional kwa kuajili watu ambao ni competent based on their ability na siyo based on kujuana watamsaidia. Bashe ni mjanja alitumia professional kipindi cha Dkt Magufuli wakawa wanamsaidia kuchambua na hatimaye Dkt Magufuli akamuona. Kinachotakiwa kwa Ridhiwani ni kujibambanua awe peke yake ajipange
Ridhwan Hana charisma na baba yake aliharibu mno kipindi chake watanzania wanaiangalia hiyo familia kwa jicho tofauti. kipindi kijacho ni cha wakristo
 
Ndugu zangu, Jana usiku tumepokea taarifa kupitia ukurasa wa Ikulu mawasiliano juu ya Utenguzi na Uteuzi. Habari kubwa ni kuhusu kutenguliwa kwa aliyekuwa waziri wa mambo ya nje ndg January Makamba pamoja na Ndg Nape Nnauye aliyekuwa waziri wa mawasiliano na teknolojia ya Habari.

Sasa wengi wamejielekeza kuhusu utenguzi huo, Mimi naomba tuangalie kwa jicho la tatu tunamuona aliyekuwa naibu waziri Mh Ridhiwani Kikwete sasa anakuwa waziri ofisi ya Waziri mkuu kwake hii ni promotion.

Kwakuwa mtoto wa nyoka ni nyoka, je tumtegemee Mh Ridhiwani kuvaa viatu vya baba yake au bado hana ukomavu wa kisiasa? Je, January anastahili nafasi nyingine? Au tumsapoti huko AU?

Je tutegemee mvurugano ndani ya chama tawala au ni mipango inasukwa?

Karibuni wanabodi
Baba yake mwenyewe kaacha viatu vya mchuchumio au laizoni unataka vimuangushe
 
Ridhwan Hana charisma na baba yake aliharibu mno kipindi chake watanzania wanaiangalia hiyo familia kwa jicho tofauti. kipindi kijacho ni cha wakristo
Mkuu, tangu lini watanzania wakachagua si wanaletewa majina tu?
 
Kwa sababu anatupiga bila kelele kwenye media ndio iwe sababu ya kumpatia ofisi za juu bila kujali makando kando yake na familia anayotoka!
Ni kama akili za watanzania zimefubaa sasa hivi hatujui wapi tunakwenda na nini tunataka.
Mungu pekee ndiye atatutoa kwenye huu mkwamo.
 
Tupe tathmini yako mkuu
 
Back
Top Bottom